Huyu anayepigwa hapa si jambazi. Ni mfanyabiashara aitwaye Ally Asaad Ajirin, anayemiliki duka la Shaahidi Stores lililopo Barabara ya Nyamwezi jirani na Soko Kuu, Arusha. Anapigwa na aliyekua DC wa Hai, Lengai Ole Sabaya pamoja na mabaunsa wake. Sabaya ndiye anayeongoza kipigo hicho.
Asaad alipigwa hadi kuzirai. Alizinduka akiwa hospitalini ameumizwa sehemu mbalimbali za mwili wake. Wakati kipigo kikiendelea wananchi walisikia kilio ndani ya duka hilo wakampigia simu Diwani wa Sombetini Bakari Msangi, ambaye ni rafiki yake Asaad. Msangi alipofika aligonga mlango akafunguliwa lakini nae akaunganishwa kwenye kipigo.
Walivuliwa mashati na kupigwa kwa nyaya za umeme mgongoni. Walifungwa mikono na miguu na kupigwa kwa rungu, mikanda na kukanyagwa na buti. Msangi aliharibiwa kabisa sikio lake moja na hadi sasa halisikii kabisa.
Kwanini Sabaya na mabaunsa wake walifanya ukatili huu?
February 09 mwaka huu, Sabaya akiwa na genge lake la mabaunsa walienda Arusha katika duka la Assaad na kumtuhumu kwamba anafanya biashara ya kubadili fedha za kigeni kinyume cha sheria. Assaad akakataa na kusema hajawahi kufanya biashara hiyo.
Sabaya alimtaka ampe 100M ili asipewe kesi ya uhujumu uchumi. Lakini akakataa na kuhoji iweje DC wa Hai, aende Arusha akatafute maduka yanayobadilisha fedha, wakati Arusha kuna vyombo vya ulinzi?
Sabaya kusikia hivyo, akaona jamaa ana kiburi kwahiyo akakaagiza milango ifungwe na ndipo wakaanza kumshushia kipigo. Walimpiga wakitaka aoneshe mahali alipoficha pesa za kigeni. Kadri alivyojitetea kuwa hana pesa hizo, ndivyo kipigo kilizidi kuongezeka hadi kuzirai.
Sabaya na wenzake waliyafanya hayo wakirekodiwa na camera za CCTV lakini wala hawakujali. Walijua hakuna lolote wanaloweza kufanywa maana walikua wanalindwa na mfumo.!
Credit: Malisa GJ
My Take
Haya yalifanyika chini ya urais wa Magufuli. Au urais wa wanyonge ulikuwa na maana hii?