Arusha: Masheikh 6 wahukumiwa kunyongwa hadi kifo

Arusha: Masheikh 6 wahukumiwa kunyongwa hadi kifo

Nchi za kiislamu zinazoendesha serikali yake kwa kufuata vitabu vya dini zimetoa adhabu ya kifo kwa mtu ambaye ataukana uislamu (apostasy)

Kuna adhabu ya kunyongwa kwa watu wanaojihushisha na homosexual.

Kumbuka hao wote wanao hukumiwa sio tu kwamba hawajaua au kufanya jaribio la kuua bali hawajamjeruhi hata nzi.

Kama umeona hao masheikh hawakustahili kupewa adhabu ya kifo na kuona wameonewa kwasababu kwenye lile bomu hakuna aliyekufa, ebu fikiria hao watu wanaokatwa vichwa kwasababu tu ni mashoga au wameukataa tu uislamu?

Je walistahili kukatwa vichwa japokuwa hakuna mtu waliyemuua?

Nauhakika kwa upande wako adhabu hiyo unaiona ni fair kabisa kuona mtu anachinjwa kwakua kaukataa tu uislamu.

Utakuwa tayari kupeperusha bendera za ushindi na kutoa kauli za kumsifu Mungu wakati watu hao wakichinjwa.

Na pengine hata wewe tu unaweza kumuonea wivu yule mchinjaji ukatamani nafasi hiyo upewe wewe ukiamini kufanya hivyo utapata thawabu.

Type ya watu kama nyinyi ndio wale mnaotamani.watu wote tuwe waislamu, na sisemi kama ni jambo baya kuwa na wishfully thinking ya namna hiyo.

Ubaya ni njia unayochagua kuitumia ili kuwafanya watu wote tuwe dini yako baada ya mahubiri na mafundisho kushindwa kumshawishi mtu na hivyo kutumia mabavu na roho mbaya.
Mkuu unahamisha mada hapa tupo kwenye jamhuri ya mgaano wa Tanzania na tuna fuata katiba ya jamuhuri, sasa yale ya nchi za kiarabu unaketa za nini kwa kulinganisha adhabu tofauti tofauti.
 
Wasamehewe.
Kama walilipua kanisa na hakuna mtu aliyefariki hiyo ni hukumu ya Allah.

Waachie, miaka kumi wako kifungoni imetosha.

Yaani Rais amesaini hicho kitu?

Wale Waheshimiwa wawasaidie kukata rufaa.
Kisheria nnavyo jua wana hukumu kuanzia nia hovu adi tukio, mfano mzuri wale wanao tishiwa maisha ikibainika basi mtishiaji ana ukumiwa,

Tuje kwenye point yako, yaani kwa akili za kawaida mlipuke utokee katikati ya umati wa watu afu kusiwe na mahiti? Wapo waliokufa na wengine ni vilema wa kudumu mpaka leo,

Utetezi wako ni sawa mimi nije kwenu nilipue nyumba yenu (lengo ni kuuwa na kuleta uharibu wa nyumba) then sheria iniache huru utakubali?

hukumu inabidi iwe kali ili wengine waogope, hili swala tutumie uhalisia sio imani.
 
Mkuu kuhusudia kuua na kuua sio kitu kimoja na adhabu yake haiwezi kua moja.
Kwamba unaifahamu vizuri sheria kuliko Jaji na mawakili wa pande zote mbili za mashtaka na utetezi? By the way wanaweza kukata rufaa kuwa wameonewa kupewa adhabu ya kuua wakati wao walikududia tu kuua
 
Nipo hapa, hauawi mtu. So ninyi na waendesha mashtaki endeleeni kujifariji tu, mama samia hasaini.
Kunyongwa ni adhabu nafuu ikitekelezwa kwa wakati.

Kukalishwa jela tena selo za condemn, huku mawazo kibao na kutengwa ni adhabu Kali zaidi ya kitanzi.

Mkuu tusishabikie ubaya na kutetea dhilumati.
 
Ila wakati wa Kikwete sijui masheikh walipata mzuka gani...zanzibar nako kuliikuwa na shida sana kwa madhehebu ya Kikristu.....
 
Ugaidi hauna nafasi katika jamii yoyote iliyostaarabika.
Nakumbuka jinsi selikari ilivojitahidi kufanya tukio lionekane ni la kisiasa ili kutoharibu biashara ya utalii, wiki Moja baadae alitumwa mtu akatupa bomu kwenye mkutano wa kina mbowe,afu waandishi flani wakasema ni mtililiko uleule wa vurugu za kisiasa ,ila Hali Itakuwa shwali,,


i like propaganda
 
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

MASHEIKH SITA 6 WAHUKUMIWA KUNYONGWA ARUSHA LEO

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo tarehe 12/12/2023, imewasomea hukumu Masheikh tisa miongoni mwa wale wanaoshikiliwa na Serikali kwa zaidi ya miaka kumi katika Gereza Kuu la Kisonge Mkoani Arusha.

Masheikh hao wanatuhumiwa na Serikali kwa Ugaidi wa kulipua Kanisa Katoliki la Ole sita mkoani Arusha mwaka 2013.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Nkwabi aliwaachia huru Masheikh watatu ingawa mmoja miongoni mwao amerejeshwa jela kwa sababu ya kukabiliwa na tuhuma nyingine.

Walioachiwa huru ni: Abduli Humud Wagoba, Abdurahmani na Amani Mussa Pakasi (ambaye amerejeshwa gerezani).

Aidha Jaji Nkwabi alionesha kuridhishwa na ushahidi wa Polisi kwamba Masheikh sita katika shauri hilo akiwemo imamu mkuu wa Msikiti mashuhuri Masjid Quba Arusha, Sheikh Jaafar Hashim Lema waliripua Kanisa Katoliki na kusababisha madhara makubwa.

Kwa sababu hiyo Jaji Nkwabi aliamua kuwahukumu adhabu kali ya kunyongwa mpaka kufa.

Masheikh hao waliokaa gerezani kwa zaidi ya miaka kumi na hatimaye kuhukumiwa kifo ni:

1. Imam Jaafar Hashima Lema.
2. Yusuf Ali Huta
3. Ramadhani Hamadi Waziri.
4. Abdul Hassa Masta.
5. Kassim Idrisa. Na-
6. Abashari Hassan Omari.

Masheikh hao pamoja na wenzao kumi walio hukumiwa kunyongwa hivi karibuni mkoani Tanga, watanyongwa baada ya Rais Samia Suluhu Hassani kutia saini.

Pia, soma;

Mlipuko mkubwa watokea kwenye Kanisa Katoliki Arusha, watu kadhaa wajeruhiwa
Wanyongwe tu, hakuna kucheka na religius terrolist, ukiwapa nafasi hawa nchi inakuwa kama somalia
 
Back
Top Bottom