ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

Waandishi wa habari zaidi ya 10 wakiwa wanatekeleza majukumu yao katika ile shule ya Lucky Vincent Arusha wametiwa mbaroni eti kwa kufanya mkusanyiko bila kibali.

Alikuwemo pia Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro na viongozi wa TAMONGSCO na wakuu wa shule mbalimbali wakitoa rambirambi zao.

Waandishi wamefikishwa kituo kikuu cha polisi na kuhojiwa. Bila shaka wataachiwa. Inasemekana katika mazungumzo yaliyokuwa yakifanyika pale shuleni, moja ya ajenda ilikuwa ni lile sakata la RAMBIRAMBI.

Kwahiyo ndugu waandishi , be careful, watch it........
 
hali ikiendelea nahisi hata kwenye mikusanyikoya misiba, nyumbani au makaburini itabidi vibali viombwe, manake nayo ni mikusanyiko isiyo halali,
 
Huyo Meya mchochezi tu, hata senti moja hakuchangia anataka kuchafua amani ya mkoani hapo na nchini kupitia mgongo wa misiba.

Kabisa hana la kufanya bali kulalamika, pesa inaelekea alikuwa anezitamani sasa ile zaidi ya 59m iliyobaki inamuuma haswa.

Awamu ya tano hii
 
Hata ingekua ni mimi nisingekubali mtu aoteshe rambi rambi mbawa kirahisi rahisi namna hiyo.
[HASHTAG]#ULAJI[/HASHTAG] wote huo unipite hivi hivi.
Hapana kwakweli mnaweza kuficha rambi rambi lakini noti tuzati eksitenti.
 
Usiniambie kama watu wa kubwa waliohudhuria walikuwa wanahudumiwa! Huenda walilipwa na night? Kwani walienda kufanya shughuli ya kitaifa au waliguswa na msiba wanapenda kutoa pole?
 
Wamiliki wa shule binafsi Jijini Arusha na waandishi wa habari kumi pamoja na Meya wa jiji hilo waliokuwa wameenda kutoa rambirambi katika shule ya msingi Lucky Vincent wamefikishwa kituo cha Polisi kwa kosa la kufanya mkusanyiko bila kibali. Waandishi hao pamoja na wamiliki wa shule binafsi wamefikishwa katika kituo hicho huku ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa katika kituo hicho ili kuweza kuzuia genge kubwa la watu ambalo limekusanyika kwa ajili ya kushuhudia kinachoendelea. [ 30 more words ]
 
Usiniambie kama watu wa kubwa waliohudhuria walikuwa wanahudumiwa! Huenda walilipwa na night? Kwani walienda kufanya shughuli ya kitaifa au waliguswa na msiba wanapenda kutoa pole?

Kwenye siku zote za misiba majumbani mwenu huwa hamlishi watu wanaokuja kutoa pole!?
 
Sijui kosa lao ni lipi masikini wakati wameenda kuwafariji wafiwa!
ni vitendo vipi visivyovumilika? una maana viongozi waliochaguliwa na wananchi kwenda kuwapa pole wananchi waliowachagua? (kweli maradhi ya akili yako ya aina nyingi, dah!)

Unajua ni vigumu sn kumuelewesha mtu wa kaliba yako, huyo kiongozi unaemsema majuzi tu hapa alikuwa anaongea shombo kwenye vyombo vya habari juu ya hzo rambi rambi so ni wazi alienda pale akiwa anajua kbsa anachokifuata ..... afu meya hachaguliwi na wananchi kijana
 
ile pesa haikuwa ya vyakula, ile ilikuwa ni ya rambi rambi, kwanini mlipie gharama za vyakula kwa pesa ya rambi rambi, hivi cocochanel unaenda msikitini au kanisani wewe, kweli kweli watu watu, mashirika yanachangia nyie mnapeleka ati zimegharamia vyakula na malazi kweli, serikali si huwa ina mfuko wa maafa, na kwanini mayor asipewe ufafanuzi, kwani kuna tabu gani, yani pesa ya maafa au rambirambi ndio mtumie kwenda kulipia gharama za wageni kweli, inakuingia akilini, daah, inahuzunisha sana
 
Da hata kama kutumwa sio kijinga ivo kuna shida mahali 🙁
 
'#BREAKING Waandishi zaidi ya 8 waliokamatwa Arusha leo ktk utoaji rambirambi kwa Lucky Vicent wameachiwa, Polisi wawaambia waliwapa lift tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…