Kama ni mkutano wa uchochezi ni sawa tu. Meya kaumbuka kwa kudai serikali imekula pesa, sasa wanataka kutumia siasa kufanya maajabu juu ya ajali iliyogusa wengi.
Mlianza mitandaoni kutishia kutumi nguvu kuichafua serikali, hiyo haikubaliki kabisaaaa.
Ni bora muweke sera zenu mbele zijulikane tho hamna, kuliko kudandia majambo kutafutia kiki.
Mengine tuheshimu dola itupe maelezo zaidi.
Sasa cocochanel, mumetangaza kuwa mumewapa wafiwa pesa ya rambi rambi mil3.8 kumbe mumewapa 1 na kuwaahidi nyingine mtalipa baadae, kuna pesa ya chakula mumetumia m4, watu wanauliza hivyo vyakula wamekula wapi, haya kwa msaada wa mama samia, hawa vijana wasingepelekwa nje kutibiwa kwani serikali ilishasema ingewatibu hapa hapa, hebu kuweni na huruma jamani, mnakuwa kama hamna watoto, nchi sio ya kijani, nchi ni yote sote, hamna hati miliki inapotokea maafa kama haya watu siasa muache ili tuwahudumie wahanga, nyie kweli mpaka rambi rambi mnameza kweli?
Daah, na yatajulikana mengi tu, hizi pesa tutaziacha hapa hapa na hakuna atakayezikwa nazo, mie kwangu nasema kuweni na utu, litakuja kutokea jambo kubwa sana na watu, mashirika yatagoma kutoa kwa huu ukiritimba wenu, mnajitahidi sana kujenga chuki katika jamii tuonane wabaya, lakini sie tumeshikamana na hatutachukiana kamwe upendo aliotuachia Nyerere tutazidi kuuenzi,
Katu hatutatengamana, ila tu chuki itatengenezwa kati ya viongozi na wananchi na sio wananchi kwa wananchi