Tunaambiwa habari ya kwamba Meya na madiwani,wane,mapadri na shehe mkuu mmoja wamekamtwa wa kwenda kuwapa pole wafiwa,wamefanya kosa gani hata ifikie hivyo???.Jeshi la Polisi limesema, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ndiye aliyetoa amri ya kukamatwa kwa walioenda kutoa salamu za rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent leo.
====
UPDATES:
Waandishi zaidi ya 8 waliokamatwa Arusha leo ktk utoaji rambirambi kwa Lucky Vicent wameachiwa, Polisi wawaambia waliwapa lift tu.
Huu ni uonevu,halafu ukisema,wapambe wa maonevu,wataingiza yao kipropaganda,kutaka ionekani ni jambo la kawaida,Tanzania I nakwenda katika kipindi kigumu cha ukiukwaji wa haki za kibinaadamu,kila ukiamka u,utasikia vyombo vya serikali,vinaendelea kuwatengenezea matatizo wananchi wake,halafu mnakuja kustaajabu mambo yanayotokea ukanda wa kibiti ,mkuranga,na rufiji,ikiwa raia hamuwatendei wema,mnategemea kuzalisha nini???,Rais anatakiwa apate msaada ama wakuu wastaafu,kama kikwete ambaye,aliiacha nchi katka hali ya watu kutegemea maendeleo zaidi na utulivu,Kama hakuna haki itayoleta amani,nayo maendeleo tunayoambiwa,yatakuja vipi?Leo nchi imerudi nyuma miaka 40 iliyopita,Amani nchi imekuweko muda wote,lakini katakana ukiukwaji mkubwa wa haki na sheria,Amani inafifia,suali tunajiuliza,haya mambo ya ukandamizaji huu yanafanywa kwa makusudi??,tusipoziba tutakuja juta,bado tunaipenda nchi yetu.
Mwenyenzi Mungu ibariki Tanzania.