ARUSHA: Mmoja akamatwa akituhumiwa kumfanyia ukatili Mtoto

ARUSHA: Mmoja akamatwa akituhumiwa kumfanyia ukatili Mtoto

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2026-04-16 at 16.15.23.jpeg
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia mtu mmoja aitwaje Johnson Jonas mkazi wa Matejoo Jijini humo kwa tuhuma za kumpiga mtoto mwenye umri wa miaka kumi na tatu kufuatia picha mjongea inayosambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii ikionesha tukio hilo.

Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo katika eneo la kanisa Jijini humo, ambapo wanakamilisha uchunguzi kwa hatua zaidi za kisheria.


 
Vizuri sana,lakini nawakumbusha polisi na nyinyi mkamatane kwa sababu mnapenda sana kukanyaga vichwa na kuvunja viungo vya watuhumiwa kinyume na sheria za jeshi la polisi.
 
Back
Top Bottom