Yy Kwan kaaacha kula gomba?Akihojiwa Asubuhi ya Leo katika Moja ya Radio jijini Arusha mtia Nia ya udiwani wa kata ya ngarenaro almaarufu dogo janja ambae pia ni mwanamuziki amesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa Diwani wa kata ya ngarenaro Basi atahakikisha Vibanda vyote vya pombe haramu, Bangi na mirungi vitaondolewa .
Dogo janja amesema hayo baada ya kujibu swali aliloulizwa na msikilizaji ambae ni mkazi wa kata ya ngarenaro Kuwa endapo atachaguliwa Kuwa Diwani wa ngarenaro atachukua hatua Gani kwenye Vibanda vya pombe haramu na madawa ya kulevya vilivyoota kama uyoga katika kata hiyo ambapo Hadi wanafunzi ni wateja wakubwa wa Bangi na gongo katika Vibanda hivyo.
Dogo janja ameeleza Kuwa endapo atachaguliwa kuwa Diwani basi habari ya kusafiri safiri kwenda Dar hatokuwa nayo tena.
atapita na atakomesha kweli ivyo vitu maana mkuu wa mkoa wa sahivi KENANI ni mshikaji wake,fanyeni uchunguzi ata kidogo kabla ya kuongea mi nimeanza kuona ushikaji wa dogo janja tangu 2021 KENANI akiwa mkuu wa wilaya ya ARUSHA mjini,ata siku KENANI anagraduate master yake pale IAA 2021 dogo janja alikwenda kwenye graduation yake,kwa iyo ni mmoja wa watu waliomshawishi kuingia kwenye siasa na watamsaidia kwenye connection ya kupata udiwani na watashirikiana kuinyoosha Ngarenaro maana KENANI ni zaidi ya MAKONDA nakumbuka aliwahi chapa viboko wezi wa madawati SINONI badala ya kuwaachia polisi majukumu yao.Makonda atamsaidia ashinde huyo dogo vinginevyo kura za wavuta bangi, wala mirungi na wanywa gongo atazikosa, vita kama hii huwa haitangazwi hadharani angesubiri ashinde ndio awashukie walevi hao