Arusha ni tofauti na inavyozungumziwa kwenye mitandao

Pesanyingi

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2023
Posts
1,157
Reaction score
1,983
Habari wakuu.

Jiji la Arusha lina tatizo gani? Viongozi inabidi wajitafakari sijuwi ni wanafanya kazi kwa mazoea (kwa kukaa kituo kimoja cha kazi kwa muda mrefu) au hakuna ubunifu wa kiutendaji.

Hadi leo huu mkoa ni aibu na fedhea ya karne wameshindwa kujenga stand ya mabasi ya kisasa. Iliyokuwepo na inayotumika sasa nadhani ni tangu enzi za mkoloni. Yaani, Arusha inazidiwa hata na Wilaya ya Korogwe na zingine kwa upande wa stand za mabasi ya kisasa.

Arusha bado wanakimbizana na usafiri wa Toyota Hiace maarufu kama vi fodi (nadhani jina hili wamekopi tangu enzi magari aina ya Ford yakitumika kama magari ya kubeba abiria). Vigari vyenyewe vidogo siti kama za wanafunzi.

Arusha haina masoko ya kisasa yaliyokuwepo. Mfano, soko kuu ni aibu kwa mgeni anaweza asiamini. Soko la Kilombero nalo ni majanga matupu. Viongozi wa mkoa wa Arusha si vibaya kwenda kujifunza maeneo mengine waliofanyika mabadiliko kama Morogoro, Mwanza, Tanga, Dar, n.k. Kuliko kujifungia hapa hapa bila kuwa na mabadiliko.
 
Kuna watu wanaishi Dar zaidi ya Jehanam...nyumba zimezunguukwa na visiwa vya vinyesi ...una zalisha mabomu mchana usiku unayavurumishia nje....I think NEMIKI wangejikita huko.....

Arusha ni Geneva.....ngareroo Ostabeyii....teh teh....Mbauda uzunguni....Haf Landani Sekei....
 
Tuachie chuga yetu tunaielewa sisi wenyewe

Mbona wewe unajiita Pesanyingi wakati huna pesa nahatuja lalamika
 
Mie mwenyewe nashindwa kuelewa wanao usifia huu mkoa wanatumia kigezo gani hasa?

Barbara za rami zimechoka choka, wakati wa kiangazi vumbi kama lote, wakati wa mvua tope kama lote. yaani hakuna unafuu kwa vipindi vyote vya mwaka.

Masoko yote ya hovyo hovyo, stend zao ndo usiseme, vijana nao wako hoi.
Kiukweli Mimi Arusha hapana.
 
Binafsi swala la vifodi ni kero kubwa sana na vipanya wavipige marufuku hata kusimama huwez public transport arusha ni ya hovyo sana
 
Arusha siasa imezidi. Imagine mpaka Leo katikati ya mji Pana garage bubu, pombe zinauzwa hovyo, Moshi na moto vinawashwa.... Hayo mavijiwe Kuna watu walipwa na hao wachafuzi. Yaani Arusha Kuna mambo mengine mbunge anatetea upumbavu, mbunge apuuze siasa

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Mbunge wao ndio Chanzo Cha matatizo ya Jiji la Arusha.

Uzuri Jana kupitia kikao Cha halmashauri kuu ya CCM mkoa Moja ya azimio lililopitishwa ni pamoja na kuwadhibiti na kuwaadihimia wote wanaotoa Siri za chama bila kupitia kamati ya maadili.


Dawa ya mbunge imepatikana
 
Moshono,njiro,riksi,mbauda nk
 
Ongezea na mamigomba katikati ya hicho kimji.

Vibarabara vyembamba vumejaa vumbi na viraka
 
Arusha ni Pana mkuu nenda ngorongoro utakuja kutoa ushuhuda hata hivyo kinachonipa fraha Ina sehemu za bata kila maeneo
 
Huwa nikiangalia mikato na swag za masela wa A town sioni kabisa ni kwa namna gani hawa watu wanaweza kuwa na mipango ya maendeleo ya mji wao
Kuna mshikaji wangu wa Arusha alikuja Dar kwa issue zake,bahati nzuri akafikia kwangu ila nilimshangaa sana!

Hivi kwa hali ya joto la Dar unawezaje kukaa siku tatu bila kuoga wala kubadilisha nguo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…