Pesanyingi
JF-Expert Member
- Apr 15, 2023
- 1,157
- 1,983
Habari wakuu.
Jiji la Arusha lina tatizo gani? Viongozi inabidi wajitafakari sijuwi ni wanafanya kazi kwa mazoea (kwa kukaa kituo kimoja cha kazi kwa muda mrefu) au hakuna ubunifu wa kiutendaji.
Hadi leo huu mkoa ni aibu na fedhea ya karne wameshindwa kujenga stand ya mabasi ya kisasa. Iliyokuwepo na inayotumika sasa nadhani ni tangu enzi za mkoloni. Yaani, Arusha inazidiwa hata na Wilaya ya Korogwe na zingine kwa upande wa stand za mabasi ya kisasa.
Arusha bado wanakimbizana na usafiri wa Toyota Hiace maarufu kama vi fodi (nadhani jina hili wamekopi tangu enzi magari aina ya Ford yakitumika kama magari ya kubeba abiria). Vigari vyenyewe vidogo siti kama za wanafunzi.
Arusha haina masoko ya kisasa yaliyokuwepo. Mfano, soko kuu ni aibu kwa mgeni anaweza asiamini. Soko la Kilombero nalo ni majanga matupu. Viongozi wa mkoa wa Arusha si vibaya kwenda kujifunza maeneo mengine waliofanyika mabadiliko kama Morogoro, Mwanza, Tanga, Dar, n.k. Kuliko kujifungia hapa hapa bila kuwa na mabadiliko.