Kizibo
JF-Expert Member
- Jul 3, 2018
- 4,033
- 8,805
HahahahaaaKiongozi Salama
Mimi Niko Nje Ya Mada Kidogo
Siku Hizi Avatar Yako Mbona Haitingishi T*k* Nini Kimetokea Ama
Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HahahahaaaKiongozi Salama
Mimi Niko Nje Ya Mada Kidogo
Siku Hizi Avatar Yako Mbona Haitingishi T*k* Nini Kimetokea Ama
Si mlishaambiwa MSIOE..Polisi wa kituo cha Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha wanadaiwa kumpiga risasi raia aliyetambuliwa kwa jina la Yohana Nasieli kwa kile kilichoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi kati ya mke wa marehemu na askari polisi.
Habari kutoka kwa ndugu na majirani wa marehemu zilisema kuwa tukio hilo limetokea aprill 12 mwaka huu majira ya saa 1.35 usiku katika mtaa wa sabasaba kata ya Monduli Tarafa ya Kisongo wilayani humo.
Vyanzo vilisema kuwa siku ya tukio ya marehemu alikuwana ugomvi na mke wake, Paulina Kiliani{37} na kumlalamikia mke wake kuwa sio mwaminifu katika ndoa akimtuhumu kuwa na mahusiano na askari polisi aliyefanya mauaji {jina linahifadhiwa} kuwa ndio mvunja ndoa yake.
Vyanzo vya habari viliendelea kusema kuwa siku ya mauaji marehemu na mke wake walikuwa na ugomvi mkubwa na kufikia hatua ya kupigana na mke alimpigia simu ya kiganjani askari polisi huyo na kumwelezea kupigwa kwake na mume wake na askari huyo akiwa na mwenza wakiwa na silaha walikwenda eneo la tukio.
Habari zilisema kuwa baada ya marehemu kumwona askari yule yule anayemtuhumu kufanya mapenzi na mke wake akiwa wa kwanza kufika eneo la tukio,marehemu kwa hasira huku akiongea kwa jazba kuwa wewe ndio niliyekuwa nakutafuta ghafla aliingia ndani ya nyumba yake na kuchukua panga kwa nia ya kumtishia askari huyo akiwa na mwenzake ili aondoke eneo la tukio.
Vyanzo vilisema kuwa kabla ya marehemu kufanya tukio la kutaka kumkata Askari huyo,ghafla askari huyo alifyatua risasi na kumpiga marehemu kifuani kushoto na mguuni na kufariki dunia papo hapo.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo alithibitisha tukio hilo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo imesema kuwa NASIELI alijeruhiwa kwa risasi upande wa kushoto wa mguu na kwenye bega la mkono wa kushoto baada ya kukaidi amri halali ya askari Polisi ya kukamatwa na kutaka kumkata askari panga alilokuwa nalo mkononi mwake.
Kamanda aliendelea kueleza katika taarifa yake kuwa marehemu alikuwa amewafungia watoto wake na mtoto wa jirani yake ndani ya nyumba kwania ya kuwadhuru na baada ya kutoa taarifa askari waliamua kwenda eneo la tukio kwa nia ya kuwaokoa watoto lakini pia kumkamata mtuhumiwa.
Taarifa ilisema baada ya kufika eneo la tukio walianza kugonga mlango uliokuwa umefungwa ili kuokoa watoto waliokuwa hatarini wakati wanaokoa watoto hao nje ya nyumba hiyo walimwona mtuhumiwa huyo akiwa amejificha akiwa ameshika panga Mkononi huku akiwa fuata askari hao kwa lengo la kuwadhuru.
Alisema baada ya hali hiyo ndipo alipoamua kumpiga risasi kwenye bega lake la kushoto hali iliyosababisha kuvuja damu nyingi na kisha kupelekwa katika hospital ya wilaya ya Monduli na mtuhumiwa huyo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu.
Ends...
Marehemu alikuwa ana kichaa cha mapenzi.Mtu ambaye hukumtoa bikra,ulimkuta akiwa na meno 32 yameshaota,huna undugu naye hata kidogo;Akiamua kuchukua 50 zake kwanini usiachane naye?Wanawake mbona wako wengi na kila siku wazuri wanaendelea kuzaliwa?Angeachana naye kiroho safi,sasa hivi angekuwa bado yuko hai,sanasana maumivu ya moyo angeyapata siku za mwanzo mwanzo,baadae maisha yangiendelea.Ona sasa uhai wake umepotea na mwanamke amemuacha anaendelea kuvinjari na madume mengine!Ndugu na majirani wanasemaje?
To be fair akae ndani Hadi upelelezi wa kesi hii utakapokamilika.Tayari polisi wamepindisha kesi kumlinda mwenzao na kesi ya mauaji. This world is not fair
Sure atavuna alichopanda kwa kipindi alichobaki nacho duniani, karma inamhusu sana neno furaha kwenye mahusiano litakuwa kitendawili.Lipi ni lipi? Tuamini majirani au kamanda wa mkoa?
Kama shida ni wivu kama walivyosema majirani, mke tayari amekosa mme, amebaki mjane, na huyo askari hatomuoa. Yani amekosa bara na Pwani na hii dhambi itamtafuna maisha yake yote.
Sure neno bora kuachana hivi hivi bila mtifuano inahitaji neema ya Mungu sana akujalie hekima na busara bila hivyo mwisho wake huwa sio mzuri.Hizi stori za bora kuachana uko nazo wewe ambaye haujakutwa na hilo balaa
Habari imeanza kwa kumtuhumu askari... Mwishoni mwa habari... Mtuhumiwa anatetewa na kupewa kesi MarehemuPolisi wa kituo cha Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha wanadaiwa kumpiga risasi raia aliyetambuliwa kwa jina la Yohana Nasieli kwa kile kilichoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi kati ya mke wa marehemu na askari polisi.