Arusha: Ukikutwa umevaa Suruali ya kubana, Sketi fupi Faini Tsh. 50,000

Arusha: Ukikutwa umevaa Suruali ya kubana, Sketi fupi Faini Tsh. 50,000

Hbr za jioni ndugu.

Awali kabisa naomba niwapongeze wote kwa ufuatiliaji wa mijadala ya jamii.

Aidha, niseme kuwa, mimi binafsi sitaona aibu kusema kuwa nimewapongeza jamii hiyo kwanza kwa uthubutu tu wa kubaini kuna changamoto na kuketi pamoja kama jamii ya rika zote kujadili na kukubaliana wao.

Hii kwangu ni ishara kwamba, sasa kumbe jamii yetu imeanza kubaini changamoto na kuzimiliki na kuzijadili na Sasa kinachofuata ni msaada wa kitaalamu Ili mijadala yao isikinzane na sheria mama za nchi na uhuru wa haki za binadamu. Mm nimelitazama hivyo.

Sasa kwa kuwa nyie mmelitazama tofauti, haki yenu kujadili katika jicho lenu. Ila sisi huu ni mwanzo mwema wa jamii Sasa kuanza safari ya mabadiliko ya fikra kwamba wao ndiyo injini ya kujadili changamoto zao na sisi ni wa kupeleka msaada wa kitaalamu Ili wafike salama safari yao pasipo kuathiri sheria kuu zote.

Ruksa kuniona mm siko sawa ila niwaombe tu pia kuwa, ziko Mila au sheria za kijamii huko kwenye maeneo yetu ambazo zina athari kiafya, zinaua na kuleta ulemavu, ningependa pia zianzishiwe mjadala kwani ni dharura.

Ahsanteni sana, tupo pamoja na mawazo tunapokea. Mbarikiwe.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Sawa Mh.

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
 
Mbona hawatoi dozi kwa wauza bangi
Kumbuka Miaka mitano nyuma kuna eneo linaitwa Mtaa wa Mavi pale mianzini ambapo ndipo kitovu cha madawa ya kulevya...ukienda unakuta vijana wamejidunga na wamelala kuanzia asubuhi hawafanyi kazi yoyote

Polisi waliwashindwa wale vijana kwasababu wakienda wanahongwa

Lakini Jamii ya hawa watu walijiorganise wakaenda na fimbo mwezi mzima wakaanza kuwachapa vizuri wenye nyumba wanaowafuga hawa wahuni, hii ni baada ya kuambiwa wawaondoe baadae wakaanza kuwachapa hawa vijana viboko vya kutosha.

Leo hii pale pako shwari kabisa

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
 
wanasema eti ni sheria ndogondogo, na waziri kaunga mkono kabisa eti.
Hbr za jioni.

Mimi nimepongeza Sana hatua za jamii Sasa kuketi chini na kujadili mambo yanayowahusu. Na hapo sisi kazi ya wizara ni kwenda kuwaongoza Ili hatua zao zisikinzane na sheria mama zilizopo na hatimaye kufikia mabadiliko chanya kwa ustawi wao na maendeleo yao. Sasa nitakuwa mnafiki Sana kuhamasisha jamii imiliki ajenda zao kwa ufumbuzi wa changamoto zao, halafu wanaanza mdogomdogo, badala ya kwenda sasa kuwasaidia wasafiri salama, natoka nasema HAPANA ACHENI... sawa na ulipokuwa mdogo unajaribu kuinuka utembee unaanguka halafu wanakucheka na kukupiga, sijui kama ungefika hapa ulipo.

Kifupi, tujifunze kuruhusu jamii zetu zinapoanza safari tuzipe moyo kisha tuziongoze. Tutoke humu jukwaani tukutane saiti tupeleke mawazo chanya. Tusiwe wa kujua Kila kitu halafu wa kwanza kuuliza je tulifikaje hapa.

Ahsante Sana. Tuendelee kujadiliana kwa utulivu Ili tupate elimu chanya.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: ITR
Na watalii nao mtawapiga faini au ni Sisi kwa Sisi.

Hii nchi imekosa viongozi wenye AKILI
Ngoja nikuelimishe kama nitaweza.

Ziko nchi fulani hapa ukipanda ndege tu unaruka takribani saa tano tu. Huko kuna Mila zao na desturi zao ambazo, nilipofika nikakuta mambo ambayo mm sikutarajia. Tukiwa semina nikauliza, kulikoni haya mambo huku? Wakasema, huu ni mji wa kibiashara ambapo Kila mtalii anakuja anaacha hela lakini hajawahi ambukiza watu wa huku Mila mpya, Wana yao na kanuni zao na watalii Wana yao na wanaondoka nayo.

Nirejee Sasa kwenye swali lako, kwani Kila mtalii akija tubebe yake tubaki nayo? Au Kila mgeni aliyeenda nje ya nchi akibeba ya huko akaja nayo sisi tuyabebe?

Tujadili tu. Ahsante Sana ubarikiwe

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Hawataweza.

Hawataweza ng'oo

Huo muda Kwanza wametoa wapi wa kujadili mavazi ya mtu hizi ni dalili za kukosa Kazi za kufanya.

Maisha yakikaza hata muda wa kuvaa hovyo hawawez kuwaza
Hakuna kitu duniani kimewekwa kikawezekana asilimia mia moja. Hakipo kabisa. Mambo mengine huwezekana kwa watu wachache kulingana na ukubwa wa nguvu ya hekima yao katika kutafsiri mambo na kubaini hili lafaa au lah. Wao watakuwa wametimiza wajibu na wameonesha umuhimu wa jamii kumiliki ajenda zao jambo ambalo ni muhimu kwani, kupitia SPIRIT hiyo hata wakija wezi kwenye jamii yao wataketi pamoja kujadili. Kikubwa ni Spirit ya mabadiliko na matokeo hutegemea mambo mengi Sana.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Ushamba unawasumbua, pamoja na kuvaa vizuri tumegundua nini cha ajabu kuwazidi wazungu wakaa uchi
Unadhani hao unaowasema Wana Kila kitu chema? Pekua taarifa zao za stress uone.... unaweza kuendelea na Kila kitu lakini amani ya moyo haipo kabisa na unakoelekea ni kwingine kabisa.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Miongoni mwa yaliyopitishwa ni pamoja na kupiga marufuku wasichana au wanawake kuvaa suruali za kubana au sketi fupi 'vimini', kijana wa kiume kusuka nywele au kunyoa pembezoni mwa kichwa na kuacha nywele katikati 'kiduku', kuvaa hereni au kuvaa suruali inayoonyesha makalio na adhabu za makosa hayo ni faini Sh50,000.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa kijiji hicho, Mtendaji wa Kata hiyo ya Kimnyak, Joshua Mollel, aliwasilisha sheria hizo kwa niaba ya mtendaji wa kijiji hicho, ambazo zilipitishwa na mkutano huo.
Kwahiyo vijana wanaanza kuhamia vijiji jirani maana hapo pamewaka moto
 
Waache ujinga hao viongozi
Sidhani kama ni ujinga huo. Maana Iko siku itawahitaji kwenye jambo lingine ambalo utapenda kuona wanakaa pamoja kama vile kulijadili, utakuwa umeshaua hiyo spirit, na hapo ndiyo jamii zetu zinapojikuta hata jambo la kawaida ambalo wao kuanzia ngazi ya familia wangemaliza hawamalizi maana hatuoni hata kwamba, jamii ikikaa pamoja kujadili jambo, basi huo ni mwanzo wa uwezekano wa kuingiza uongozi Ili waelekee kwenye matokeo chanya. Hili huwa hatuoni.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Nimeipenda hii kuna uzi nilipendekeza humu ndani kua iwepo sheria ya kudhibiti hawa wahuni wahuni wanaotembea uchi tena hii iwe nchi nzima

Sent from my TECNO PR651H using JamiiForums mobile app
Ww ni kati ya wale waliobarikiwa neema ya kuamini kuwa, tunaweza kuendelea huku tukitunza Yale ambayo yanatutofautisha na wanyama. Hii ni neema. Maana Dunia ya leo inakoelekea ni kukosa macho ya rohoni na kujielekeza kwenye taasisi ya wanyama wa porini kabisa ingawa nao naona wanazo akili. Maana wanajua mnyama gani ni nani na kiuongo chake kipi Kiko kwa matumizi gani.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: ITR
Hao ni wajinga tu ushindwe kulea kijana wako vizuri alafu uje uweke faini watu wanafikiri na makalio sio bure
Tatizo lingine ni hili sasa ambalo haya hatujui nani ataenda kulisemea maana wengine humu hata hawajulikani kwao wapi. Hivi kwani kuongea lazima utie na kaneno katusi fulani hivi? Malezi haya tunayosema kwa nyakati za sasa kweli ni neema tu.

Ndiyo maana wengi wamekosa hiyo neema sasa na tunasikia kauli ambazo chochote ambacho huwezi kukisema na kumwambia mtu kwenye nyumba ya Ibada hicho ni ukosefu wa maadili.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Jamhuri ya ovyo; limtu linaamka linajiamulia tu; no kufuata sheria linajiamulia tu na umaskini wetu Upo pale pale; hawa watu bila kuchinja mmoja kwa mmoja baada ya mwingine no change will come
Jamani hbr za jioni. Limtu tena? Kazi ipo.
Haya sasa wao wamekaa wameamua, sisi hata hatuishi huko, kumbe si ndiyo tungewapa ushauri tu kuwa; ndugu hongereni sana kwa Nia yenu njema. Ila sasa je, hamuoni moja mbili tatu? Mnaonaje iwe hivi ?

Sasa tena matusi ndiyo yatawasaidia? Au yatatufanya sisi tuwe sawa wao hawako sawa? Si wote sasa hatuko sawa na huenda sisi tunakuwa zaidi? Mungu wa mbinguni atutee. Sijui tuanze wapi na vita ya maadili, maneno yetu? Mavazi yetu au matendo yetu. Mwe

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom