Arusha: Vibaka wameanza kuwavamia hadi wanafunzi wadogo na kuwapora vitu vyao. Mdogo wangu ni miongoni mwa walioporwa

Arusha: Vibaka wameanza kuwavamia hadi wanafunzi wadogo na kuwapora vitu vyao. Mdogo wangu ni miongoni mwa walioporwa

hermanthegreat

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2021
Posts
1,274
Reaction score
3,282
Wanafunzi wengi akiwemo mdogo wangu wa mwisho aliye form 1, Iliboru wamevamiwa na kuporwa vitu vyao wakati wakielekea stend kupanda magari baada ya kufunga shule.

Wengine wamevamiwa walipokuwa nje ya shule kwa manunuzi kidogo , wamenyang'anywa kila walichokuwa nacho kuanzia kadi ya benki hadi daftari.

Inaonekana vibaka wanaosifiwa na jamii kwa kuwaita wadudu walikuwa wamejiandaa na kuwalia timing wakifunga shule. Hii si ishara nzuri kabisa.

Tunaweza kuliona hili kama jambo dogo lakini taratibu Arusha itakuja kuwa chanzo cha magaidi watakaotowesha amani kabisa, kuna haja serikali ikaangalia hili suala mapema na kuridhibiti kuliko kuishi kwa wasiwasi na tahadhari kubwa kwenye nchi yako mwenyewe.
 
Arusha kuna ushamba mkubwa sana wa hao wadudu na kuendekeza kwao pombe na bangi kunaleta madhara kwa jamii
 
Wenyewe wanajiita machalii wa R wapuuzi sana wanachojua ni kula mirungi,kuvuta bangi na visungura kazi hawataki kufanya ni kutembea na visu tu..
Arusha ina vijana wapumbavu sana..
 
Kosa kumruhusu kijana aende wakati unajua taratibu zote za ajira.

Wamepakiwa kwenye bus, wamevuka Tabora, simu hawana tena, shida inaanzia hapo.

Kwakuwa imeshafikia hapo, endeleeni kumlilia Mungu ili awaokoe.

Hao sasa ni mateka. 😭😭😭
 
Back
Top Bottom