Mpo salama wanajukwaa?
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha wamejikuta wakiingia kwenye mgogoro mkubwa uliosababisha kurushiana maneno makali na hata ngumi, muda mfupi baada ya mkutano kati ya Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama hicho Benson Kigaila na waandishi wa habari uliofanyika katika Ukumbi wa Golden Rose, Novemba 13, 2024.
Mashuhuda wameripoti kuwa vurugu hizo zilianza majira ya saa 12:30 jioni na ziliendelea kwa takribani saa moja. Wanachama hao walionekana wakirushiana lawama huku wakidai kuwa walishambuliwa na vijana wa hamasa wa chama hicho.
"Tumeshambuliwa na vijana wa hamasa bila sababu yoyote ya msingi," ameeleza mmoja wa wanachama, ambaye alisisitiza kuwa tukio hilo limeleta mgawanyiko ndani ya chama.
Mbali na malalamiko ya kupigwa, baadhi ya wanachama hao walimtupia lawama nyingi Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, wakimtuhumu kuwa na mienendo inayowakatisha tamaa ndani ya chama. Wamesema kuwa mienendo hiyo imekuwa chanzo cha migogoro na kutokuelewana miongoni mwa wanachama.
View attachment 3151765
Chanzo: Jambo TV