LGE2024 Arusha: Vurugu zaibuka, wafuasi CHADEMA wataka kunyukana

LGE2024 Arusha: Vurugu zaibuka, wafuasi CHADEMA wataka kunyukana

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Hakuna mamluku hapo kweli? Kuna kitu kimejificha hapo si bure.
 
CHADEMA WAZICHAPA HADHARANI, LEMA AKIDAIWA KUJIMILIKISHA CHAMA ARUSHA.

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini Bw. Godbless Lema anatuhumiwa na baadhi ya wanachama wa Chama hicho Mkoani Arusha kwa kuongoza kwa Ubabe na kupandikiza watu anaowataka yeye kwenye Nafasi mbalimbali zinazowaniwa kwenye Uchaguzi wa kuchagua Viongozi mbalimbali wa Chama hicho Kanda ya Kaskazini.

Lema inadaiwa kuwa amekuwa akiwaweka wagombea anaowataka yeye kwa nguvu akijaribu kupanga safu yake kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2025, akitumia Vijana wa Hamasa kuwapiga wale wanaompinga kwenye teuzi hizo za ndani ya Chadema pamoja na kuwasimamisha Viongozi wanaopishana naye mawazo.

Aidha wanachama hao kadhalika wameonesha kusikitishwa na maandalizi ya CHADEMA kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 pamoja na Uchaguzi Mkuu wa 2025, wakishangazwa na namna ambavyo Chama chao kimeshindwa kusimamisha wagombea kwenye maeneo mengi kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa.
 
Attachments

  • fa4a72e1-62b9-49d7-a348-14b8f0a046fc.mov
    27.8 MB
CHADEMA na CCM ni fisi na ngiri wamekutana mwituni nchi hii ni kama Ina laana Kila anayepata kakitengo hataki kuachi anataka ale hapo milele

Mbowe Yuko tayar chama kife kuliko yeye kuachia madaraka

Wamachame ni watu wa ajabu sana
 
CCM huwezi kufanya hayo maana Samia ni Mungu, Nchimbi ni Yesu, Makalla ni Malaika Gabriel.
chedema kuna watu lazima wakosolewwe na wasemwe kama kuna mahali they have messed up!
Rekebisha sema sa100 ni mungu
 
Mpo salama wanajukwaa?

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha wamejikuta wakiingia kwenye mgogoro mkubwa uliosababisha kurushiana maneno makali na hata ngumi, muda mfupi baada ya mkutano kati ya Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama hicho Benson Kigaila na waandishi wa habari uliofanyika katika Ukumbi wa Golden Rose, Novemba 13, 2024.

Mashuhuda wameripoti kuwa vurugu hizo zilianza majira ya saa 12:30 jioni na ziliendelea kwa takribani saa moja. Wanachama hao walionekana wakirushiana lawama huku wakidai kuwa walishambuliwa na vijana wa hamasa wa chama hicho.

"Tumeshambuliwa na vijana wa hamasa bila sababu yoyote ya msingi," ameeleza mmoja wa wanachama, ambaye alisisitiza kuwa tukio hilo limeleta mgawanyiko ndani ya chama.

Mbali na malalamiko ya kupigwa, baadhi ya wanachama hao walimtupia lawama nyingi Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, wakimtuhumu kuwa na mienendo inayowakatisha tamaa ndani ya chama. Wamesema kuwa mienendo hiyo imekuwa chanzo cha migogoro na kutokuelewana miongoni mwa wanachama.

Pia soma: Wanachama wa CHADEMA Katavi wachapana makonde, Mbowe ashutumiwa kugawa pesa kwa wajumbe

Chanzo: Jambo TV
hapo chanzo itakuwa ccm waliingia kwenye mkutano huo chadema hawawezi kugombana hata siku mo9ja hao ni malaika
 
hapo chanzo itakuwa ccm waliingia kwenye mkutano huo chadema hawawezi kugombana hata siku mo9ja hao ni malaika
Kwa kweli ni Malaika hata yule mwizi wa Magari nae anajiita Nabii alieshindwa kutabiri ujio wa Lowassa (2015)
 
Kwaiyo mambo yalikuwa kama hivi

Oya jambilaa mnalala huko ofisini nakula ruzuku hamuwasaidii wagombea kujaza fomu mpaka wanakosea ngoja tuwashenyente kwanza.
lcimg-b030e1e5-52df-40e9-80c9-1ee9e40175f0.jpeg
 
Sio kama Lema Mkuu.
Uliishia level gani? Ulisoma wapi ? Bora lema aliyekimbia umande lakini mkweli na kuliko wewe uliyekariri ukapata dv 3 na ukaishia kuwa mbeya na mzushi usiyejua nyeupe na nyeusi
 
Uliishia level gani? Ulisoma wapi ? Bora lema aliyekimbia umande lakini mkweli na kuliko wewe uliyekariri ukapata dv 3 na ukaishia kuwa mbeya na mzushi usiyejua nyeupe na nyeusi
Mangi ,nasisitiza kuwa Lema alikimbia umande ndio maana hajui afanye nini;mfanyabishara?mwanasiasa?Nabii? {Pathetic)
 
Mangi ,nasisitiza kuwa Lema alikimbia umande ndio maana hajui afanye nini;mfanyabishara?mwanasiasa?Nabii? {Pathetic)
Wewe hujakimbia umande uliishia level gani na unafanya nn?
Wewe hujakimbia umande unajulikana wapi na kina nani?
Lema amekimbia umande sawa ila leo tunamjadili kwa jina lake wewe na mm tunatumia majina fake. Nani kamzidi mwenzie
 
Mangi siwezi tumia jina fake au unataka kunipachika jina la ukoo wenu? Lema anajadiliwa kwa upuuzi wake ambao unatia aibu jamaii ya KICHAGA.
 
Mangi siwezi tumia jina fake au unataka kunipachika jina la ukoo wenu? Lema anajadiliwa kwa upuuzi wake ambao unatia aibu jamaii ya KICHAGA.
Bado hujasema upuuzi wa lema ni upi. Bado hujasema kama hujakimbia umande uliishia ngazi gani ya elimu ili tujue wewe unacho cha kumzidi lena???
 
Godless Lema amejikuta katika wakati mgumu leo ambapo Wanachadema wengi wamelalamika jinsi anavyoendesha Uchaguzi.

Ngumi zimefumuka.

CHADEMA wamepigana ngumi huko Arusha leo katika kikao cha kumchagua Mwenyekiti wa Mkoa.

Pia soma
- LGE2024 - Arusha: Godbless Lema awatimua Maofisa wa TAKUKURU kwenye semina ya Wagombea wa CHADEMA, adai Wameacha uozo ufanywe kwenye Uandikishaji
Napenda upinzani ukue, lakini kwa bahati mbaya kinachoonekana ni kudhoofika kwa upinzani.
Godbless Lema, aka mropokaji, hawezi na hana sifa za kuwa kiongozi ndani ya CHADEMA.
CHADEMA haijajiandaa kwa uchaguzi wowote ule, wa ndani wala wa serikali za mitaa. LISSU YUKO SAWA.
CHADEMA iswaongopee wananchi, haina umaarufu wa kuchukua Dola, pengine 2050.
 
Bado hujasema upuuzi wa lema ni upi. Bado hujasema kama hujakimbia umande uliishia ngazi gani ya elimu ili tujue wewe unacho cha kumzidi lena???
Lema hupenda sana Press C. Sijui kwanini bado hajaita Press C. kujibu tuhuma hizi. Tunamsubiri.
 
Bado hujasema upuuzi wa lema ni upi. Bado hujasema kama hujakimbia umande uliishia ngazi gani ya elimu ili tujue wewe unacho cha kumzidi lena???
Upuuzi wa Lema;
1:Ugali ni chakula cha maskini
2: Angekuwa Rais hakuna kujenga hoteli prorin
3: Kule Canada kuna caffe late kila mahali
4: Mimi ni Mchagga

5: Boda Boda ni Laana
6:Anoambea watu wapate majanga (wafe)🙆‍♂️🙆‍♂️
7: Mke wake ni bora kuliko wanaweke wengi(post kibao kuhusu mke wage instagram)
8: Yeye hataki ubunge kama kazi ila 24/7 anaota kuhusu ubunge

Endeleza mkuu,
 
Back
Top Bottom