Hii nchi ina baadhi ya viongozi wenye uwezo mdogo sana wa kufikiri! Yaani kwa akili zao wanaamini wanafunzi walioshindwa kukariri masomo kuliko wanafunzi wengine, basi hawana akili! Jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo.
Kwanza Serikali inatakiwa kuachana na mambo ya kuingiza siasa kwenye elimu! Hii sera yao ya kuruhusu wanafunzi wote kuhitimu kidato cha nne, halafu masomo yenyewe ni ya kukariri tu, na yasiyo na mchango wowote ule kwenye maisha yao! ni sera ya hovyo kupitiliza.
Serikali inatakiwa kuanzisha vyuo vya ufundi stadi kila Kata! Kama ilivyofanya kwenye shule za Kata. Halafu wanafunzi wote wanaopata alama za chini na za kati, wanapekekwa huko kwa ajili ya kusomea cheti katika fani mbalimbali kama vile ufundi, upambambaji, michezo, maigizo, nk. Na baadaye kupata sifa ya kujiendeleza katika ngazi ya stashahada, shahada, nk.
Na wale wanafunzi wenye uwezo wa kukariri masomo (wenye akili) ndiyo wangepata nafasi ya kuendelea na masomo ya Sekondari na Chuo katika mfumo uliopo sasa. Haya mambo ya kulazimisha watoto kukariri masomo, ndiyo huchangia sana kufeli kwao, na mwisho wa siku lawama zinapekekwa kwa walimu!
Serikali ingeboresha elimu ya VETA nchini (Mfano kunzisha vyuo hivyo katika ngazi ya kila kata), naamini kwa kiwango kikubwa tatizo la ajira kwa vijana lingepungua sana. Kuwadhalilisha watu kwa makosa ya watu wengine, siyo sawa hata kidogo.