Arusha; Walioiba na kuchoma Moto kituo cha mafuta cha Panone Oktoba 29 waanza kufa mmoja baada ya mwingine

Arusha; Walioiba na kuchoma Moto kituo cha mafuta cha Panone Oktoba 29 waanza kufa mmoja baada ya mwingine

Sio kweli na kwanini ukikataa kuamini haya mambo watu huwa wana kasirika kabisa?🤔
Hawataki kabisa kuachana na hizo mambo za kuamini uchawi na majini Yaani hata Jambo liwe wazi kabisa kwamba hapa hakuna uchawi ukisema wanakuwa wakali balaa 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Vijana ambao wengi ni boda boda na wengine wasio boda boda katika Wilaya ya Arumeru wameanza kufa Kwa vifo vya ajabu ajabu hususani kupasuka vichwa ghafla na vifo vingine visivyoeleweka.

Tukio hilo linajiri baada ya mmiliki wa kituo Cha mafuta Cha Panone kilichochomwa moto na kuibiwa vitu mbali mbali katika super market yake iliyopo hapo hapo kituoni wakati wa vurugu za October 29 kuonana na uongozi wa kata na Kijiji ili kuwasihi vijana wao warudishe vitu walivyochukua la sivyo wasilalamike Kwa lolote lile litakaowapata vijana hao .

Hata hivyo uongozi wa kijiji na kata ya Ambureni umeambulia kupata mitungi miwili mitupu ya gesi na masufuria machache kutoka Kwa vijana haokwa ajili ya kumrudishia mwenyewe .

Hata hivyo ndani ya muda wa mwezi Mmoja tangu mmiliki huyo wa kituo kutoa tngazo Hilo vijana zaidi ya sita wamekufa vifo vya ajabu ajabu ikiwemo kupasuka vichwa na hata Sasa abiria wanaogopa kupanda boda boda za vijana huko Arumeru wakihofia lolote laweza tokea wakiwa Barabarani
Nakumbuka miaka ya nyuma bodaboda waliochoma gari ya mpemba mbezi beach ,aisee walianza kudanja mmoja mmoja leo boda kaingia chini ya scania ,kesho mwingine kaingia chini ya fuso ,kesho kutwa mwingine kaingia chini ya semi ,walivyoona wanapukutika ikabidi wengine warudi mkoa waache boa...kijiwe kizima wakaacha wengine wakafa.
 
Mmiliki wa hiyo kampuni
Anaitwa nani?

Ova
 
Hao vijana WA Arusha wakisikia vichwa vinauma waende hospital kabla havijapasuka!
😅😅umenichekesha!

Ishi vizuri na watu uwe mwema usije kufikia hizi hatua, mnapukutishwa wewe na vizazi vyako!
 
Nakumbuka miaka ya nyuma bodaboda waliochoma gari ya mpemba mbezi beach ,aisee walianza kudanja mmoja mmoja leo boda kaingia chini ya scania ,kesho mwingine kaingia chini ya fuso ,kesho kutwa mwingine kaingia chini ya semi ,walivyoona wanapukutika ikabidi wengine warudi mkoa waache boa...kijiwe kizima wakaacha wengine wakafa.
Propaganda...


Cc: Mahondaw
 
Mbongo akifika chuo kikuu, akasoma filosofia na ethics kidogo anajifanya amebadilika kifikra...

Anasahau uchawi upo...

Wengi wanaosema uchawi ni Imani potofu walikalilishwa kwenye tamthiliya za Kiswahili na Kiingereza...

Nawahakikishia hao madogo wataisha wote...

Huo uchawi ni mbaya kishenzi...

Endeleeni kusema Imani potofu huku madogo wanayeya...
Wewe tenda mema kwa binadamu wenzako ili uishi kwa amani, ila haya mambo yapo na yanafanya kazi sana tu!!
Nimeona huko vijijini mtu anaibiwa ng'ombe, anatoa tangazo, baada ya mda wanakata moto hadi pale waliobaki watakapoomba radhi. Wanaweza kufa hata watu kumi.
Nilishaona watu wameiba mahindi ya msukuma mmoja amepeleka mpakani mwa tz na kenya yavushwe kwa piki jamaa wakashirikiana mtu tano wakauza sacks 3 za kilo 108 each. Msukuma akawambia warudishe tena akiwabembeleza jamaa wakapuzia msujuma akaenda zake. Baada ya miezi mitatu hiyo squad ya mtu 5 walianza kufa mmoja baada ya mwingne alibaki mmoja tu na yeye kilicho msaidia ni baada ya kusema ukweli alivoshirikishwa huo mchongo ila msongo wa mawazo umempga kwel kawa kama chz vile na wa mwisho kufa aliugua gonjwa ambalo lilishnda wote yaan mtu anaugu hadi anaanza kuchomoka vidole vyote bila kukatwa. So hayo mambo yapo sishangai mimi.
Hii nimeipata juzi asee ni kweli maana aliyeniambia ni ndugu wa muhanga

Kumbe jamaa alitoa mpaka lipa namba vijana warudishe miamala vijana wakakaza fuvu 🤠🤠

Wameru kiherehere kimekwisha 😂😂
Niliwahi kusikia na baadhi ya watu niliona wakifa kwa kile kiitwacho kuvunja jungu. Kuhaa mma" lakini bado sinaimani na teknollojia hiyo
 
Mbongo akifika chuo kikuu, akasoma filosofia na ethics kidogo anajifanya amebadilika kifikra...
Watu wanashindwa kuelewa: Rais wa nchi anasimikwa na machifu wa kila mkoa.Umewahi kujiuliza hao machifu huwa wanamilki nini?? Kwa nini serikali ikubali mkuu wa nchi afanyiwe hivi??
 
Vijana ambao wengi ni boda boda na wengine wasio boda boda katika Wilaya ya Arumeru wameanza kufa Kwa vifo vya ajabu ajabu hususani kupasuka vichwa ghafla na vifo vingine visivyoeleweka.

Tukio hilo linajiri baada ya mmiliki wa kituo Cha mafuta Cha Panone kilichochomwa moto na kuibiwa vitu mbali mbali katika super market yake iliyopo hapo hapo kituoni wakati wa vurugu za October 29 kuonana na uongozi wa kata na Kijiji ili kuwasihi vijana wao warudishe vitu walivyochukua la sivyo wasilalamike Kwa lolote lile litakaowapata vijana hao .

Hata hivyo uongozi wa kijiji na kata ya Ambureni umeambulia kupata mitungi miwili mitupu ya gesi na masufuria machache kutoka Kwa vijana haokwa ajili ya kumrudishia mwenyewe .

Hata hivyo ndani ya muda wa mwezi Mmoja tangu mmiliki huyo wa kituo kutoa tngazo Hilo vijana zaidi ya sita wamekufa vifo vya ajabu ajabu ikiwemo kupasuka vichwa na hata Sasa abiria wanaogopa kupanda boda boda za vijana huko Arumeru wakihofia lolote laweza tokea wakiwa Barabarani
....Wewe unawafahamu binafsi walioiba Vitu Hapo Panone ? Na unawafamu rasmi mareemu Boda Boda SITA waliofariki Kwa Mkwara huo wa Panone? Una Hakika kuwa ni Panone amefanya. Vitu vyake?? Tujizuir Kusambazs Imani Potofu
 
Back
Top Bottom