DOKEZO Arusha: Wanafunzi almanusura wasombwe na maji wakivuka mto kuelekea shule

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari Lemara pamoja na shule ya msingi Lemara zote za serikali wamenusurika kusombwa na Maji ya mto Themi wakati wakienda shule.

Mwaka jana wanafunzi watatu wa shule ya msingi Lemara waliokolewa baada ya kuzidiwa na maji wakati wakivuka mto huo kwenda shule.

Mto huo unaotenganisha kata ya Sinoni, Themi pamoja na Kata ya Lemara hauna kivuko tangu kivuko cha awali kusombwa na Maji zaidi ya miaka mitano iliyopita.

Msimu wa mvua baadhi ya vijana hujenga kivuko cha muda na kutoza wananchi pamoja na wanafunzi kiasi cha shilingi 200 kuvuka kwenda upande wa pili wa mto.

Kwa maelezo ya wananchi wa maeneo hayo ni kuwa suala hilo la kivuko ni Miaka mingi wanapiga kelele kwa viongozi lakini hakuna mabadiliko yoyote.

Hi ni hatari sana, kwani kadri wanavyozidi kuvuka ndio nguvu ya maji pengine inavyoongezeka..btw ujumbe umefika.
 
Watoto wanateseka hivi Alf kuna watu Wanaiba Mabilioni ya Fedha za wananchi Dah Haki Ya Mungu Wanasiasa watachomwa Moto wa Luminous-Flame huko jehanamu.
 
Tunasubiri maafa yatokee alafu tutoe Press ya Pole na rambirambi🙆‍♂️

Kama umesema wakati wa Masika baadhi ya Vijana hujenga Kivuko na kutoza shilingi 200 inaonesha hicho kivuko hakizidi gharama ya shilingi 3,000,000 kukijenga.

3,000,000 ni fedha ndogo ambayo inaweza kutolewa na Halmashauri au Mbunge kupitia Fedha za Mfuko wa Jimbo.

Wakati mwingine, kuwa kiongozi ni lazima uwe na uwezo wa kujiongoza. Ina maana jambo dogo hilo linamhitaji hadi Rais wa Nchi aje alifanye? Hao wasaidizi wake akina DC, DED, RC wanafanya kazi gani?
 
Duu,hii ni hatari sana aisee,halafu unasikia mafisadi wanavyochota fedha za umma bila huruma!kwa kweli hii nchi kuna watu watakuja kupata laana ya milele wao na vizazi vyao!
 
Hao watoto wametumika kama specimen
 
Hao watoto wametumika kama specimen
 
Yakitokea yakutokea hapo....itaundwa tume kuchunguza chanzo.
 
Watu wako buzzy na kupinga ushoga, huku wengine wakikwapua fedha za umma,

Maendeleo ya miundo mbinu sio kipaumbele chetu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Basi angalau viongozi waweke kamba
Wavuke huku wanaishika

Ova
 
Wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari Lemara pamoja na shule ya msingi Lemara zote za serikali wamenusurika kusombwa na Maji ya mto Themi wakati wakienda shule.

Mwaka jana wanafunzi watatu wa shule ya msingi Lemara waliokolewa baada ya kuzidiwa na maji wakati wakivuka mto huo kwenda shule.

Mto huo unaotenganisha kata ya Sinoni, Themi pamoja na Kata ya Lemara hauna kivuko tangu kivuko cha awali kusombwa na Maji zaidi ya miaka mitano iliyopita.

Msimu wa mvua baadhi ya vijana hujenga kivuko cha muda na kutoza wananchi pamoja na wanafunzi kiasi cha shilingi 200 kuvuka kwenda upande wa pili wa mto.

Kwa maelezo ya wananchi wa maeneo hayo ni kuwa suala hilo la kivuko ni Miaka mingi wanapiga kelele kwa viongozi lakini hakuna mabadiliko yoyote.

Ripoti ya CAG
 
Hilo daraja mbioni kujengwa mwaka huu chini ya mradi wa Tactic so wavumilie.
 
Back
Top Bottom