Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Wananchi jijini Arusha pamoja na abiria wanaotumia stand kubwa ya mabasi wamailalamikia uongozi wa jiji la Arusha kuwa wameshindwa kuwaletea mabadiliko kwa kuwajengea stand nyingine mpya ya kisasa tofauti na iliyopo sasa ambayo ipo tangu kabla ya uhuru hadi sasa.
Kutokana na udogo wa kituo hicho cha Mabasi umefanya baadhi ya makampuni kushusha na Kupakia abiria katika sehemu mbalimbali na wengine katika ofisi zao zilizopo sehemu tofauti tofauti jijini hapo na hivyo kuleta usumbufu kwa abiria na wageni kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Mfano gari za kwenda Namanga kuna ambazo zinapaki stand kubwa na. Nyingine nje ya uwanja wa mpira wa. Abeid karume.
Magari ya Kwenda Dar es Salaam kuna machache yanapaki ndani ya kituo hicho, mengine stand ndogo na. Mengine yamekuwa yakipakiza na kushusha abiria katika ofisi zao
Za kwenda karatu nazo kuna ambazo zinapaki ndani ya kituo na nyingine mbali na kituo hicho maeneo ya Sabena
Kituo hicho kikubwa cha mabasi hakina sehemu ya kusubiri abiria wala Wasindikizaji.
Hakuna sehemu ya kuwakinga na Mvua wala jua.
Na. Pia Usalama ni mdogo usiku na. Mchana kutokana na miundombinu ya kituo hicho cha mabasi na hivyo Kuwa na. Idadi kubwa ya vibaka, wezi, wavutaji wa madawa yote na vijana wa mitaani ambao ni tishio kwa wageni na abiria.
Wananchi wa jiji la Arusha wamekuwa wakilalamika miaka Nenda miaka rudi lakini hawaoni mabadiliko yoyote hadi sasa,kituo cha mabasi kilichopo hakiendani na hadhi ya jiji kwani jiji hili limekuwa likipokea wageni wengi ndani Na Nje ya nchi hivyo kituo hicho ambacho hakina uwezo hata wa kupaki mabasi (10)kumi kwa wakati mmoja, kinaharibu taswira ya jiji.