Arusha: Wananchi walia na kituo cha mabasi makubwa ya abiria ya kwenda mikoani

Wananchi jijini Arusha pamoja na abiria wanaotumia stand kubwa ya mabasi wamailalamikia uongozi wa jiji la Arusha kuwa wameshindwa kuwaletea mabadiliko kwa kuwajengea stand nyingine mpya ya kisasa tofauti na iliyopo sasa ambayo ipo tangu kabla ya uhuru hadi sasa.

Kutokana na udogo wa kituo hicho cha Mabasi umefanya baadhi ya makampuni kushusha na Kupakia abiria katika sehemu mbalimbali na wengine katika ofisi zao zilizopo sehemu tofauti tofauti jijini hapo na hivyo kuleta usumbufu kwa abiria na wageni kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Mfano gari za kwenda Namanga kuna ambazo zinapaki stand kubwa na. Nyingine nje ya uwanja wa mpira wa. Abeid karume.

Magari ya Kwenda Dar es Salaam kuna machache yanapaki ndani ya kituo hicho, mengine stand ndogo na. Mengine yamekuwa yakipakiza na kushusha abiria katika ofisi zao

Za kwenda karatu nazo kuna ambazo zinapaki ndani ya kituo na nyingine mbali na kituo hicho maeneo ya Sabena

Kituo hicho kikubwa cha mabasi hakina sehemu ya kusubiri abiria wala Wasindikizaji.

Hakuna sehemu ya kuwakinga na Mvua wala jua.

Na. Pia Usalama ni mdogo usiku na. Mchana kutokana na miundombinu ya kituo hicho cha mabasi na hivyo Kuwa na. Idadi kubwa ya vibaka, wezi, wavutaji wa madawa yote na vijana wa mitaani ambao ni tishio kwa wageni na abiria.

Wananchi wa jiji la Arusha wamekuwa wakilalamika miaka Nenda miaka rudi lakini hawaoni mabadiliko yoyote hadi sasa,kituo cha mabasi kilichopo hakiendani na hadhi ya jiji kwani jiji hili limekuwa likipokea wageni wengi ndani Na Nje ya nchi hivyo kituo hicho ambacho hakina uwezo hata wa kupaki mabasi (10)kumi kwa wakati mmoja, kinaharibu taswira ya jiji.

E4669E2C-523A-4496-A7E0-9701A3A140BF.jpeg
 
Eneo la stendi lilishatengwa pale Kiserian mahali pazuri kabisa. Mrisho Gambo akiwa mkuu wa mkoa akawapa rushwa madiwani wakapinga ili wapeleke kule Oljoro Bondeni city kwenye shamba la rafiki yake muhindi aliempa rushwa ili alipwe fidia baada ya shamba kumshinda. Hapafai Na ni kushoto Kwa kila kitu.
CCM 2025 toa Mrisho Gambo weka Binamu Bananga
tumekusikia binamu ila hilo sahau kabisa
 
Nilimaanisha Moshi road... yanaweza kuwa yametoka Tanga, Dar, Mombasa, nk.
Sidhani kama kuweka stendi sehemu ina maana magari yote yaishie pale.
Kwani Dar na Mwanza wanafanyeje??
Zinaweza kuwepo daladala za ruti ndefu na basi za kuunga kutoka Moshi Babati/Karatu n.k
Ukitaka maendeleo na mji upanuke kwa haraka fanya maamuzi ya kupeleka huduma mbali mbali za kijamii.
Urahisi wa connection ni nadharia pana sana na tofauti kwa kila mtu.
Changamoto zitajitokeza lakini binadamu yupo kuzitatua... Usiogope!!
dar kuna stendi ngapi ndugu za mikoani??
 
Watajenga wapi stand mji umejaa migomba ya ndizi na mapori
 
Ili mji wa Arusha upanuke na ukue kwa haraka wahusika wazingatie yafuatayo:
1. Ondoa stendi na masoko yale pale mjini kati.
2. Stendi mabasi ya kutoka Dodoma road inatakiwa iwe Kisongo. Weka soko huko.
3. Stendi mabasi kutoka Moshi road iwe USA au Chekereni. Weka soko huko.
4. Stendi magari kutoka Nairobi iwe Ngaramtoni ya Juu. Weka soko huko.
5. Stendi magari kutoka Simanjiro/Kiteto iwe Oljoro. Weka soko huko.

NB: Lakini msije mkalalamika kuwa stendi na masoko yako mbali!
Sasa maana ya stendi kuu Ni nini. Kwahiyo nashuka oljoro napanda daladala kwenda kisongo ili niende karatu, nashuka USA napanda daladala hadi kisongo ili niweze kwenda karatu.

Wazo zuri lisilofaa na lisilo na maana ya stendi kuu.

Stendi kuu maana yake inakonekti gari zote zinazoingia na kutoka.
 
Ili mji wa Arusha upanuke na ukue kwa haraka wahusika wazingatie yafuatayo:
1. Ondoa stendi na masoko yale pale mjini kati.
2. Stendi mabasi ya kutoka Dodoma road inatakiwa iwe Kisongo. Weka soko huko.
3. Stendi mabasi kutoka Moshi road iwe USA au Chekereni. Weka soko huko.
4. Stendi magari kutoka Nairobi iwe Ngaramtoni ya Juu. Weka soko huko.
5. Stendi magari kutoka Simanjiro/Kiteto iwe Oljoro. Weka soko huko.

NB: Lakini msije mkalalamika kuwa stendi na masoko yako mbali!
dah ni bonge la akili pia mji utatanuka pande zote...ngara itatanuka kuelekea oldonyo sambu,usa itatanuka kwenda kikatiti ,kisongo itatanuka sana kuelekea duka bovu pia oljoro itatanuka kuelekea mirongoine pia si mbaya wakiweka stand maeneo ya kiserian ili kutanua mji zaidi na zaidi
 
Mchakato wa stend mpya uliishia wapi
Tatizo la viongozi wetu huwa wanafanya maamuzi kwa maslahi yao.

Awali stand ilikuwa ijengwe eneo la SADC baada ya kutoka Tengeru kuelekea Moshi, wajanja wakapiga pini....mara inapelekwa kwenye eneo linalomilikiwa na CCM, Magu akakataa, mwishoni mpango ukawa sijui iende huko moshono au kwa morombo!!
 
Wananchi jijini Arusha pamoja na abiria wanaotumia stand kubwa ya mabasi wamailalamikia uongozi wa jiji la Arusha kuwa wameshindwa kuwaletea mabadiliko kwa kuwajengea stand nyingine mpya ya kisasa tofauti na iliyopo sasa ambayo ipo tangu kabla ya uhuru hadi sasa.

Kutokana na udogo wa kituo hicho cha Mabasi umefanya baadhi ya makampuni kushusha na Kupakia abiria katika sehemu mbalimbali na wengine katika ofisi zao zilizopo sehemu tofauti tofauti jijini hapo na hivyo kuleta usumbufu kwa abiria na wageni kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Mfano gari za kwenda Namanga kuna ambazo zinapaki stand kubwa na. Nyingine nje ya uwanja wa mpira wa. Abeid karume.

Magari ya Kwenda Dar es Salaam kuna machache yanapaki ndani ya kituo hicho, mengine stand ndogo na. Mengine yamekuwa yakipakiza na kushusha abiria katika ofisi zao

Za kwenda karatu nazo kuna ambazo zinapaki ndani ya kituo na nyingine mbali na kituo hicho maeneo ya Sabena

Kituo hicho kikubwa cha mabasi hakina sehemu ya kusubiri abiria wala Wasindikizaji.

Hakuna sehemu ya kuwakinga na Mvua wala jua.

Na. Pia Usalama ni mdogo usiku na. Mchana kutokana na miundombinu ya kituo hicho cha mabasi na hivyo Kuwa na. Idadi kubwa ya vibaka, wezi, wavutaji wa madawa yote na vijana wa mitaani ambao ni tishio kwa wageni na abiria.

Wananchi wa jiji la Arusha wamekuwa wakilalamika miaka Nenda miaka rudi lakini hawaoni mabadiliko yoyote hadi sasa,kituo cha mabasi kilichopo hakiendani na hadhi ya jiji kwani jiji hili limekuwa likipokea wageni wengi ndani Na Nje ya nchi hivyo kituo hicho ambacho hakina uwezo hata wa kupaki mabasi (10)kumi kwa wakati mmoja, kinaharibu taswira ya jiji.
Ukweli stand ya Arusha ni ndogo sn
 
Tatizo la viongozi wetu huwa wanafanya maamuzi kwa maslahi yao.

Awali stand ilikuwa ijengwe eneo la SADC baada ya kutoka Tengeru kuelekea Moshi, wajanja wakapiga pini....mara inapelekwa kwenye eneo linalomilikiwa na CCM, Magu akakataa, mwishoni mpango ukawa sijui iende huko moshono au kwa morombo!!
Bora iwekwe Kisongo
 
Eneo la stendi lilishatengwa pale Kiserian mahali pazuri kabisa. Mrisho Gambo akiwa mkuu wa mkoa akawapa rushwa madiwani wakapinga ili wapeleke kule Oljoro Bondeni city kwenye shamba la rafiki yake muhindi aliempa rushwa ili alipwe fidia baada ya shamba kumshinda. Hapafai Na ni kushoto Kwa kila kitu.
CCM 2025 toa Mrisho Gambo weka Binamu Bananga.
Kweli kabisa. Gambo alitutendea uhuni kuhamisha stendi kutoka Kiserian kupeleka kwa Mhindi huko!
2025 atajua kuwa hajui

Arusha haina stendi wala masoko ya hadhi yake
 
Back
Top Bottom