View attachment 2662639
MAHAKAMA Kuu kanda ya Arusha imewaachia huru Mashekhe tisa waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya jinai namba 63 ya Mwaka 2022. Kwa kudaiwa kujihusisha na matukio ya kigaidi mwaka 2014.
Washtakiwa hao waliodaiwa kurusha Mabomu katika Bar ya Arusha Night Park na kusabisha kifo cha Mtu Mmoja mnamo April 13, 2014 ni pamoja na Abdalla Athumani, Ally Hamisi, Abdalla Wambura, Rajabu Ahamed, Hassan saidi, Ally Jumanne, Yasin sanga, Shambani Abdallah, na Ibrahim Herman,
Mbali na Mashekhe hawa tisa walioachiwa huru Mashekhe wengine kumi n wawili wenye kesi za ugaidi wamesalia Magereza wakisubiri hatma yao.