Arusha: Wazazi Shule ya St. Jude waandamana kwa RC, TRA yakausha akaunti ya shule

Na bado hiyo ni rasha rasha tu. Mvua kamili bado
 
duh. hapa mtihani kwa wazazi.
mwenye shule ungejitahidi kufata sheria ikiwemo kuomba kupunguziwa kodi.
 
Mkuu, unatumia maarifa gani kumtambua maskini kwa kuangalia picha ya mtu?!
Huo ni muonekano wa maskini wa kipato!!!

Hizi taasisi zinaweza kuwa na leo zuri lkn wanao ziongoza na wahusika wa kutambua walengwa haswa wa hitaji.. wengi huongozwa na tamaa. Fumbua macho utaona ukitaka.
 
Huo ni muonekano wa maskini wa kipato!!!

Hizi taasisi zinaweza kuwa na leo zuri lkn wanao ziongoza na wahusika wa kutambua walengwa haswa wa hitaji.. wengi huongozwa na tamaa. Fumbua macho utaona ukitaka.View attachment 1639038
Kuna yoyote hapo kwenye picha mwenye muonekano wa kustua?

Kwa taarifa yako hakuna watu wenye kujali mionekano yao kama maskini kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee wanaweza kufunika hali zao.
 
hiyo ndiyo awamu ya tano
 
TRA wanasimamia sheria. Wakuulizwa ni Serikali inayopeleka mswada Bungeni na Wabunge kupitia bila "CRITISISM" ya kutosha hivyo kuacha mianya ya watu kuumizwa
unasema Hivyo sababu hayajakukuta Ila TRA wana tatizo.
 
I see. Kukwepa kodi ni kosa la jinai. Imekuwaje badala ya wahusika kufikishwa mahakamani TRA ikaushe akaunti ya Shule? Kuna tatizo mahali
Mkuu,Katika kitu kilichonishangaza ni hiki.Hii shule ni Charitable.Sasa sijui nini kinaendelea ila hii nchi yetu ina matatizo sana.Kwamba shule zinatozwa kodi?
 
Hii shule ni Kama NGO inachukua watoto maskini sanawanasomeshwa happy mpaka form six na wengine mpaka chuo.kama kungekua na shida Serikali ingekaa nao Kwanza kujua tatizo liko wapi.tunakoelekea Hali itakua tete sana
Ni kweli mkuu.
 
hii shule mgogoro na TRA ulianza wakat ule magufuli amekuja arusha kuhudhuria kusimikwa kwa Askofu wa Katoliki..askofu aliomba shule ifutiwe madeni..magufuli akasema nimeambiwa kuna kesi kwa hiyo sowwz ingilia mahakama..magakama ikaamua pesa ilipwe..nasikia shule ikalipa..bado wakaendelea kudaiwa mikodi kibao..had kufunga akaunt na mwisho wamezihamisha..watoto wote wanasoma bure asilimia 100..serikali ikae na uongoz wa shule waone namna ya kuwasaidia watoto..
 
Naomba kuelimishwa ndugu zangu, TRA ina mamlaka gani ya kuchukua hela kwenye akaunti ya shule bila ya kutoa taarifa kwa wahusika??? Ina maana serikali ina mamlaka hadi kwenye akaunti zetu binafsi???

Mwenye kuelewa hili naomba anielimishe na mimi.
maji yalishakorogeka
 
acaha tunyoshwe tu maana TEC walionesha kuiamini tume ya uchaguzi pamoja na irregulaties Fr. Kitima alisema walipe kodi sasa TEC kila mtu ataguswa utawala wa sheria ni muhimu sana unachotaje hela kutoka kwenye account watoto wanasoma bure si waliomba msamaha siku ya kusimikwa Amani kwani hawajapewa msamaha tu?
 
Nilikuwepo kwenye hyo misa
Vicar General alisema shule inategemea mapato yake kutoka kw wafadhili wa Australia. Na hakuna mwanafunzi anaelipa ada, ni kwa ajili tu ya kusaidia watoto wanaotoka familia za kipato cha chini
Asa sijui kwa nn hadi misaada inatozwa kodi, wakati hamna faida wanayopata
 
Hii shule ni Kama NGO inachukua watoto maskini sanawanasomeshwa happy mpaka form six na wengine mpaka chuo. Kama kungekua na shida Serikali ingekaa nao Kwanza kujua tatizo liko wapi.tunakoelekea Hali itakua tete sana.
Yawezekana aliyesema kua wanaosoma hapo ni watoto wa wenye pesa akawa anao uhakika,sidhani kama ni NGO inayosaidia watu maskini,wangeshindwa kuelewana.Wewe uko huko Mtowisa,hujui ya Arusha,unajua ya Lwanji na Ng'ongo.
 
Kuna chalii yangu amesoma apo advanced level akamaliza 2019, kwanzia amemaliza amekuwa akijitolea kufundisha kwenye shule ya kata aliyosoma O-level na shughuli nyingne za kijamii, kama masharti ya shule yanavoelekeza kwa wanafunzi wake

Mwaka huu ameapply chuo kikuu cha KCMUco (KCMC) akapata nafasi, lakini hivi sasa Shule imeshindwa kumlipia ada ya Chuo kutokana na hii migogoro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…