Arusha: Wazazi Shule ya St. Jude waandamana kwa RC, TRA yakausha akaunti ya shule

Arusha: Wazazi Shule ya St. Jude waandamana kwa RC, TRA yakausha akaunti ya shule

Huo ni muonekano wa maskini wa kipato!!!

Hizi taasisi zinaweza kuwa na leo zuri lkn wanao ziongoza na wahusika wa kutambua walengwa haswa wa hitaji.. wengi huongozwa na tamaa. Fumbua macho utaona ukitaka.View attachment 1639038
Aisee, wewe umeona nini kikubwa hapa, au wewe unahitaji mtu ahe uchi ndio ujue hana kipato cha kutosha, nikufingue macho tu, masikini hata akiitwa kwenye kikao cha wazazi, ataoga na kuvaa nguo pendwa.
 
Mkuu unataka wavae magunia ndo ujue ni maskini?? Mitumba siku hizi imejaa nguo kuanzia buku (1000) unapata.
Wote wale wanapata milo mitatu (3). Maskini ni yule asiyemudu milo hat mlo mmoja kwa siku
 
Ila kwa St Jude wanajitahidi sana kulenga Watoto wenye uhitaji ila tatizo ni nyie Wabongo maana Wasimamizi wa hiyo Shule ni Wazungu sasa kama mnawadanganya wao watafanyeje?.

Wanaotakiwa pale ni Watoto wanaotoka familia masikini na wanaotakiwa kufanya huo uthibitisho ni jamii wenyewe, na kwa vyovyote nafasi haziwezi kuwatosha kila wanaohitaji.
Kwann wapelekwe private school na wakati elimu Ni bure nchi nzima? Hao watoto warudishwe shule za umma ambako elimu inatolewa bila malipo
 
Mfano mzuri

Mfano mzuri picha ya hapo juu. Wazazi maskini hao kweli!!
Wawe ni Masikini au la lakini hawalipishwi chochote, na jaribu kulinganisha na facilities zinazopatikana kwenye hiyo shule.

Nyie wenyeji ndio mnahusika kutambuana nani Masikini nani sio, Hao Wasimamizi si wanatoka nje sio Wenyeji.
 
Hiyo picha haina mtu maskin hata mmoja
Ni hatari sana.
ElmOZ0cX0AYmNPa.jpg
 
Naomba kuelimishwa ndugu zangu, TRA ina mamlaka gani ya kuchukua hela kwenye akaunti ya shule bila ya kutoa taarifa kwa wahusika? Ina maana serikali ina mamlaka hadi kwenye akaunti zetu binafsi?

Mwenye kuelewa hili naomba anielimishe na mimi.
Nadhani wanaweza kutoa instruction kwa benki ku freeze account kwa muda wakati wanafanya calculation zao ,au mpaka kodi fulani ilipwe, hawana uwezo kuchota hela kwenye account ila watafreeze mpaka ulipe hiyo kodi then account zitaachiwa
 
TRA wanakamata mali ikiwamo fedha taslimu kufidia wanachodai, mali zinapigwa mnada. Wahusika hutaarifiwa na wao wenyewe ndio hutoa orodha ya mali walizonazo au namba ya akaunti ya benki.
TRA wanakamata mali bila kibali cha mahakama?
 
I see. Kukwepa kodi ni kosa la jinai. Imekuwaje badala ya wahusika kufikishwa mahakamani TRA ikaushe akaunti ya Shule? Kuna tatizo mahali

Hiyo shule ni ya msaada kwa wanafunzi wenye vipaji na wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha kwenye shule za vipaji maalumu.

Wanafunzi hao hulipa zero school fees.

Body ya shule hiyo iliyoanzishwa. na mama raia wa Australia Gemma na mumewe Bob Rich ndio hutafuta ufadhili huko nje na pesa hizo hulipia gharama kama umeme, chakula, mishahara, vitabu vyote, madaftri, vifaa vya maabara ya kufundishia, usafiri na kadhalika.

Sasa kodi ipi inayopaswa kulipiwa?

Mtu anakusaidia kazi ya kufuta ujinga kwako for free then unamdai kodi?

Hata kama ni mimba inayotaka kodi ila hali hii imekuwa too much.

Kodi kodi kodi mpaka aibu.

Keshokutwa usishangae ukiona wamwfungasha na kuhamia nchi ingine ambayo iko willing and able kusaidiwa bila masharti kama hayo.

Kisa cha yote haya ni siku ya kampeni jijini Arusha, shule zote ziliambiwa zitoe watoto wavalishwe mavazi ya CCM na kwenda kwenye mkutano aliokuwa anagutubia JPM hiyo shule pekee ikakataa kwa kigezo kuwa wanafunzi walikuwa wanaendelea na masomo.

Kauli iliyofuata ni kuwa tutawaonesha!

Na kweli wamewaonesha
 
Nadhani wanaweza kutoa instruction kwa benki ku freeze account kwa muda wakati wanafanya calculation zao ,au mpaka kodi fulani ilipwe, hawana uwezo kuchota hela kwenye account ila watafreeze mpaka ulipe hiyo kodi then account zitaachiwa
Nikuulize swali rahisi tu.

Pesa zilizochukuliwa kwny yale ma bureau de exchange zilirudishwa?

Ukipata jibu la swali hilo ndipo utajua uwezo/mabavu ya TRA/govt agencies khs pesa zozote zile zilizoko ndani ya jamhuri.
 
Kosa la hii shule waligoma kuzoa wanafunzi na kuwavisha nguo za kiraia na kwenda kwenye kampeni za mgombea uraisi, sasa ndio wanakomeshwa
Nilidhani ni utani ila naanza kuamini haya maneno baada ya kuona comment zaidi ya moja inazungumza kitu hiki
 
Hiyo shule ni ya msaada kwa wanafunzi wenye vipaji na wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha kwenye shule za vipaji maalumu.

Wanafunzi hao hulipa zero school fees.

Body ya shule hiyo iliyoanzishwa. na mama raia wa Australia Gemma na mumewe Bob Rich ndio hutafuta ufadhili huko nje na pesa hizo hulipia gharama kama umeme, chakula, mishahara, vitabu vyote, madaftri, vifaa vya maabara ya kufundishia, usafiri na kadhalika.

Sasa kodi ipi inayopaswa kulipiwa?

Mtu anakusaidia kazi ya kufuta ujinga kwako for free then unamdai kodi?

Hata kama ni mimba inayotaka kodi ila hali hii imekuwa too much.

Kodi kodi kodi mpaka aibu.

Keshokutwa usishangae ukiona wamwfungasha na kuhamia nchi ingine ambayo iko willing and able kusaidiwa bila masharti kama hayo.

Kisa cha yote haya ni siku ya kampeni jijini Arusha, shule zote ziliambiwa zitoe watoto wavalishwe mavazi ya CCM na kwenda kwenye mkutano aliokuwa anagutubia JPM hiyo shule pekee ikakataa kwa kigezo kuwa wanafunzi walikuwa wanaendelea na masomo.

Kauli iliyofuata ni kuwa tutawaonesha!

Na kweli wamewaonesha
Basi hii inchi inaendeshwa kipmbav sana
 
I see. Kukwepa kodi ni kosa la jinai. Imekuwaje badala ya wahusika kufikishwa mahakamani TRA ikaushe akaunti ya Shule? Kuna tatizo mahali
Kasome sheria ya TRA utajua inasemaje kuhusiana na issue kama hii. Kamishna ana mandate ya kufunga akaunti ama kuiamuru Benki ku debit akaunti ya mdaiwa na ku credit akaunti ya TRA. Na sheria hii almost inatumika duniani kote kuhusiana na mkwepa kodi.
 
Back
Top Bottom