Wazazi Maskini zaidi ya 2000 ambao watoto wao wanafadhiliwa kimasono katika shule ya St. Jude iliyopo Arumeru mkoa wa Arusha, wameandamana ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha wakitaka shule hiyo yenye mchepuo wa Kiingereza ifunguliwe ili watoto wao waliosimamishwa masomo kwa zaidi ya wiki mbili waweze kuendelea na masomo.
Wazazi hao wamedai kwamba mamlaka ya mapato Tanzania TRA imekausha akaunti yao kwa kuchota fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti ya shule kwa madai kwamba shule hiyo haijalipa kodi ya serikali kwa muda mrefu na hivyo uongozi wa shule hiyo kulazimika kuwasimamisha masomo wanafunzi kwa kushindwa kujiendesha baada ya fedha zilizopo kwenye akaunti kuchukuliwa na TRA.
View attachment 1638958View attachment 1638959