Arusha: Wazazi Shule ya St. Jude waandamana kwa RC, TRA yakausha akaunti ya shule

Arusha: Wazazi Shule ya St. Jude waandamana kwa RC, TRA yakausha akaunti ya shule

Hiyo shule ni ya msaada kwa wanafunzi wenye vipaji na wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha kwenye shule za vipaji maalumu.

Wanafunzi hao hulipa zero school fees.

Body ya shule hiyo iliyoanzishwa. na mama raia wa Australia Gemma na mumewe Bob Rich ndio hutafuta ufadhili huko nje na pesa hizo hulipia gharama kama umeme, chakula, mishahara, vitabu vyote, madaftri, vifaa vya maabara ya kufundishia, usafiri na kadhalika.

Sasa kodi ipi inayopaswa kulipiwa?

Mtu anakusaidia kazi ya kufuta ujinga kwako for free then unamdai kodi?

Hata kama ni mimba inayotaka kodi ila hali hii imekuwa too much.

Kodi kodi kodi mpaka aibu.

Keshokutwa usishangae ukiona wamwfungasha na kuhamia nchi ingine ambayo iko willing and able kusaidiwa bila masharti kama hayo.

Kisa cha yote haya ni siku ya kampeni jijini Arusha, shule zote ziliambiwa zitoe watoto wavalishwe mavazi ya CCM na kwenda kwenye mkutano aliokuwa anagutubia JPM hiyo shule pekee ikakataa kwa kigezo kuwa wanafunzi walikuwa wanaendelea na masomo.

Kauli iliyofuata ni kuwa tutawaonesha!

Na kweli wamewaonesha
Kwani wana exemption ya kodi mkuu?? Kama hawana basi wanatakiwa kulika kodi no way ndiyo sheria zetu za kodi zinasema hivyo hivyo hatuwezi kuwalaumu TRA kwa hilo.
 
Endelea kusomeshewa mwanao na walipa kodi wa Australia
Endelea kulambishwa alamba alamba.
EmnTYwKXUAErZPf.jpg
 
Nadhani wanaweza kutoa instruction kwa benki ku freeze account kwa muda wakati wanafanya calculation zao ,au mpaka kodi fulani ilipwe, hawana uwezo kuchota hela kwenye account ila watafreeze mpaka ulipe hiyo kodi then account zitaachiwa
Kamishna wa TRA anauwezo wakuiamuru Benki yoyote nchini kutoa pesa kutoka kwenye akaunti ya mdaiwa wa kodi na kuiweka kwenye akaunti ya TRA. Ipo kwenye sheria ya TRA
 
Hii shule kosa ililofanya ni kugoma kupeleka wanafunzi kwenye kampeni kipindi Cha uchaguzi sasa wameandikiwa Deni kubwa kuwakomoa. Ila nchi hii siasa imekuwa upumbavu wa kukomoana hyo shule ya mama mzungu Ina ethics zake sasa kuikaushia hela ni kukomoa wanafunzi waliokuwa wananufaika nayo

Asante, Kumbe unajua chanzo
 
Hivi hyo st jude ndo ile pale njiani ukiwa unatokea njia ya babati nzurii mazingira yake mazuri au nimekosea
 
Kosa la hawa watu ni kutodeclare tu kua wao ni charity.... yani mamlaka imekaa kuvizia vizia tu...... kisheria ni kweli kama ni charity lazma udeclare mwanzo, kutodeclare ni kosa.. lakini kama taasisi ikiweza kujustify kua ni kweli ni charity, kwanini wasisikilizwe na kupunguziwa adhabu kuliko kulimwa fine ambazo zinasababisha shule kufungwa???? Very painful....
 
I see. Kukwepa kodi ni kosa la jinai. Imekuwaje badala ya wahusika kufikishwa mahakamani TRA ikaushe akaunti ya Shule? Kuna tatizo mahali
Hapo sasa, ila shule kwanini haikuwapa vielelezo wazazi ionyeshwe kweli TRA imechukuwa hizo fedha?! Litakuwa kosa la jinai kwa kweli, hata kama shule haijalipa kodi...
Na kama ni kweli, je TRA inaweza mbele zaidi na kukausha hela zetu airtel money, tigopesa, Mpesa, Tpesa n.k. n.k. Kama tunadaiwa kodi????!!!
 
Tetesi Ni kushindwa kutoa Magari kusafirisha watu wa Kuongeza vichwa kwenye Kampeni.
 
Je hao watoto ni kweli wanatoka katika familia zilizokusudiwa kweli?Nakumbuka hata compassion ilikuwa hivi hivi lakini waliokuwa wansomeshwa ni watu au familia ambazo mke na mume wameajiriwa,watoto wao wakubwa wana ajira na hao wanaolipiwa sio wenye shida au uhitaji(nina rafiki yangu alikuwa boss wangu watoto wake walikuwa wanalipiwa adaKwa nini wasitembelee hizo familia masikini waone kama ni maskini?
Nimeongelea kuhusu hili kuna mtu amenipinga sana wakati tunao ushahidi wa kutosha, asilimia kubwa ya watoto waliopo kwenye hizo shule wazizi wao sio masikini
 
Ila kwa St Jude wanajitahidi sana kulenga Watoto wenye uhitaji ila tatizo ni nyie Wabongo maana Wasimamizi wa hiyo Shule ni Wazungu sasa kama mnawadanganya wao watafanyeje?.

Wanaotakiwa pale ni Watoto wanaotoka familia masikini na wanaotakiwa kufanya huo uthibitisho ni jamii wenyewe, na kwa vyovyote nafasi haziwezi kuwatosha kila wanaohitaji.
Hi ndio bongoland mambo ya nyuma ya pazia ni mengi sana, mambo ya kunyoosha mkono
 
unasema Hivyo sababu hayajakukuta Ila TRA wana tatizo.
Atakua anakatwa P.A.Y.E huyo hajui TRA kwamba ni akili matope?

Ni kweli watu wana arrears na zingine zinakwenda way back 10 years wakitumia nguvu nyingi kudai arrears kuliko kumfanya mlipa kodi astawi waweze pata zaidi mbeleni?

Na ni kweli sheria yao ya arrears haijafanyiwa marekebisho, kwani inamtaka mlipa kodi kulipa kodi once established within 6 months kitu ambacho hakiwezekani kama walimwacha mlipa kodi akabaki na arrears for ten years.
 
Hii shule kosa ililofanya ni kugoma kupeleka wanafunzi kwenye kampeni kipindi Cha uchaguzi sasa wameandikiwa Deni kubwa kuwakomoa. Ila nchi hii siasa imekuwa upumbavu wa kukomoana hyo shule ya mama mzungu Ina ethics zake sasa kuikaushia hela ni kukomoa wanafunzi waliokuwa wananufaika nayo
Kama ndivyo basi laana itawatafuna wahusika!!!
 
Hiyo shule ni ya msaada kwa wanafunzi wenye vipaji na wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha kwenye shule za vipaji maalumu.

Wanafunzi hao hulipa zero school fees.

Body ya shule hiyo iliyoanzishwa. na mama raia wa Australia Gemma na mumewe Bob Rich ndio hutafuta ufadhili huko nje na pesa hizo hulipia gharama kama umeme, chakula, mishahara, vitabu vyote, madaftri, vifaa vya maabara ya kufundishia, usafiri na kadhalika.

Sasa kodi ipi inayopaswa kulipiwa?

Mtu anakusaidia kazi ya kufuta ujinga kwako for free then unamdai kodi?

Hata kama ni mimba inayotaka kodi ila hali hii imekuwa too much.

Kodi kodi kodi mpaka aibu.

Keshokutwa usishangae ukiona wamwfungasha na kuhamia nchi ingine ambayo iko willing and able kusaidiwa bila masharti kama hayo.

Kisa cha yote haya ni siku ya kampeni jijini Arusha, shule zote ziliambiwa zitoe watoto wavalishwe mavazi ya CCM na kwenda kwenye mkutano aliokuwa anagutubia JPM hiyo shule pekee ikakataa kwa kigezo kuwa wanafunzi walikuwa wanaendelea na masomo.

Kauli iliyofuata ni kuwa tutawaonesha!

Na kweli wamewaonesha
Mungu wangu.,Kama ndivyo laana itawatafuna wahusika wote !!!!
 
Back
Top Bottom