Arusha: Wazazi Shule ya St. Jude waandamana kwa RC, TRA yakausha akaunti ya shule

Arusha: Wazazi Shule ya St. Jude waandamana kwa RC, TRA yakausha akaunti ya shule

Achana na hayo .swali kwanini TRA wabebe mpunga wa hyo shule?
Tatizo lingine katika hizo shule vigisuvigisu ni vyingi sana kwa watoto kupata nafasi katika shule hizo. Wengi wa watoto wanaosoma huko wazazi wao au walezi wao wanakipato kizuri tu, ila zinaitwa shule za watoto wa masikini.
 
Naomba kuelimishwa ndugu zangu, TRA ina mamlaka gani ya kuchukua hela kwenye akaunti ya shule bila ya kutoa taarifa kwa wahusika? Ina maana serikali ina mamlaka hadi kwenye akaunti zetu binafsi?

Mwenye kuelewa hili naomba anielimishe na mimi.
Kwa utawala huu hiyo inawezekana kabisa.!
Nasikia hata Polisi anaweza kukusachi mfukoni akikuta hela anachukua anaenda kununua "Kiwi"
 
TRA warekebishe taratibu zao za kudai kodi ili kuepuka taasis kulimbikiza deni! Inakuwaje miaka yote hiyo hawajachukuwa hatua hadi kufikia deni la kukomba akaunti nzima ya shule?

Nafkiri tatizo hapa lipo TRA wajitathmini katika utendaji wao!
 
IMG_5193.jpg
 
Wanafunzi wanaofadhiliwa na shule ya St. Jude, Arusha wamesimamishwa masomo baada ya shule kudai imeshindwa kujiendesha kutokana na TRA kufungia akaunti zake ikidaiwa limbikizo la kodi. Awali shule ilisema haiwezi kulipa sababu haifanyi biashara lakini mahakama imeiamuru kulipa. https://t.co/YX4s0xtLjJ
 
Nikuulize swali rahisi tu.

Pesa zilizochukuliwa kwny yale ma bureau de exchange zilirudishwa?

Ukipata jibu la swali hilo ndipo utajua uwezo/mabavu ya TRA/govt agencies khs pesa zozote zile zilizoko ndani ya jamhuri.
N Jumlisha na zile benki zilizofungiwa, mf Meru community bank n.k.
 
Endelea kusomeshewa mwanao na walipa kodi wa Australia
Nani kakuambia inaendeshwa na Walipa kodi wa Australia?.

Walioanzisha wazo ndio raia wa Australia, wao huomba michango kwa yeyote hata Mtanzania kama wewe...Kwenye mabango yao, Mabasi, Website utaona wanavyosisitiza sana Watu muwatembelee pale shuleni bila kujali hali yako. wanapokea chochote hata mia tano.

Cha kujiuliza ni Watanzania wangapi mnachangia hata kwa hizo mia tano mia tano? Sehemu kubwa ya Wafadhili kutoka nje ni nani wa kulaumiwa? hivi mkisema leo hamtaki michango ya nje muachiwe muichangie Waswahili wenyewe nani atawakatalia?.

Sidhani kama kuna Mtanzania anayezuiwa kuja na utaratibu kama wa huyo Mama na mumewe.

Hata kina Gajima, Jodevi, Mzeeupako, Mwaposa n.k wangeweza pia kuanzisha taasisi kama hiyo na wakatumia michango/sadaka za Waumini wao kuendesha...na wao wakiwaambia mtoe pesa mnatoa mpaka mnaishiwa na wanazila zote wao na familia zao na wala hawaulizwi kulipa kodi.
 
Daah unatonesha kidonda mzee baba.
Wiki chache nyuma tulikuwa na Mama mmoja alianzisha kiwanda cha maziwa kule Meru akawa anaweka kila cent anayopata kwenye hiyo benki kwa nia ya kupanua shughuli zake hatimae nae amiliki Kiwanda kikubwa.

Aliweka hata pesa za baadhi Wanakijiji Waliokuwa wanamuuzia maziwa, maana nao walimuomba awe kama "kibubu' chao ili baadae waje wachukua pesa anayoeleweka ingawa hataki kutaja kiasi alichokuwa amefikisha ila mwishowe aliambulia milioni moja na nusu tu, na pale ndio ikawa mwisho wa juhudi zake zote alizowekeza kwa miaka kadhaa, jumlisha muda na rasilimali zake zote. Kiwanda ndio kikafa maana aliingia kwenye madeni ya Wauza maziwa na oda za Wateja akalazimika kuuza kila kilichoweza kuuzika.

Watoto wake wanasema Mama yao alichanganyikiwa kwa siku kadhaa na huwa hawapendi kabisa akumbushwe huo msiba.
 
Tatizo lingine katika hizo shule vigisuvigisu ni vyingi sana kwa watoto kupata nafasi katika shule hizo. Wengi wa watoto wanaosoma huko wazazi wao au walezi wao wanakipato kizuri tu, ila zinaitwa shule za watoto wa masikini.
Acha uongo wako huo na upotoshaji!
 
Hii issue ya wafanyakazi kujitegemea Tin number itayaumbua makampuni mengi kufika Jan. Wengi walikuwa wanafanya michezo ya kuigiza kukata wafanyakazi Kodi na kuchanganya na Kodi yao ndogo, na hao Jude mwanzo walianza kuchanganya Private na Charity Sasa Kodi ya huko nyuma walilipa?

Na Kama kweli Kuna fungu la kushomesha kwanini hawawalipii hao wanafunzi kwenye shule moja kwa moja? Kingine watoto wenye shida wapo government tunawaona, ifike sehemu kwenye kuwajibika tuwaache wazazi wafanye majukumu yao Tena na Sheria ziwekewe mkazo kuondoa uzembe kwenye taifa, hao wazazi 2000 wote hao kweli waliondama walishindwa kubeba majukumu yao?

Ni aibu kabisa, Mimi nilitegemea kusikia watoto Yatima au wazee wasionanguvu wameandama kuomba wajukuu wao wasome maana hata Mimi niyatima najua ilivyongumu kusoma lakini siyo hao wazazi wenye nguvu wanafanya hayo maigizo bwana.
TRA wamefanya kazi yao kila mtoto pale analipiwa ada japokuwa inatokana na msaada ,na walimu na wafanyakazi wengine wanapata mishahara sasa unaikwepa wapi serikali inapodai asilimia 20 ya kilichozidi baada ya kutoa gharama za shule ?shule zote private zinalipa kodi ,tofauti yao na wengine ni chanzo cha makusanyo ,hilo la wazazi sio big issue kwa sababu wanaowafuatiliaji wazuri wanaojiridhisha wanafunzi tena mmoja tu anatoka familia isiyojiweza,na elimu inayotolewa hapo ni ya hali ya juu kweli kweli sio ya kuunga unga pengine hauwezi kuipata hata shule nyingi binafsi
 
Tatizo lingine katika hizo shule vigisuvigisu ni vyingi sana kwa watoto kupata nafasi katika shule hizo. Wengi wa watoto wanaosoma huko wazazi wao au walezi wao wanakipato kizuri tu, ila zinaitwa shule za watoto wa masikini.
Acha kushabikia kitu usichokijua
 
Je hao watoto ni kweli wanatoka katika familia zilizokusudiwa kweli?Nakumbuka hata compassion ilikuwa hivi hivi lakini waliokuwa wansomeshwa ni watu au familia ambazo mke na mume wameajiriwa,watoto wao wakubwa wana ajira na hao wanaolipiwa sio wenye shida au uhitaji(nina rafiki yangu alikuwa boss wangu watoto wake walikuwa wanalipiwa adaKwa nini wasitembelee hizo familia masikini waone kama ni maskini?
Utaratibu wa kutembelea kaya maskini upo. Sema kw watanzania udanganyifu ni mkubwa mnoo
Kuna story zilikuwepo kipindi flani kwamba mtu kama kwao wapo vizur kiasi, wanahamia kwa ndugu au majirani wenye hali duni kwa muda ili kuwadanganya wazungu wakija kuwatembelea nyumbani(sijawahi shuhudia)
 
Back
Top Bottom