TANZIA Arusha Wing tumepata msiba wa mwenzetu Freetown

Roho ya marehemu ipate rehema kwa Mungu, apumzike kwa amani! Tumepata pigo sana Arusha Wing kwa kuwapoteza member wawili chini ya mwaka mmoja! Tunamuomba Mungu atujalie utulivu kustahimili haya mapito!
 
Apumzike kwa Amani.
Msiba upo wapi?
 
Write your reply...
Nilipigiwa simu jana alfajiri na Jamaangu anayeishi eneo la UsaRiver akaniambia kuwa wako Kilimanjaro International Airport muda wa saa 1.00

Akaniambia kuwa wamefika hapo kuupokea mwili wa Rafiki yetu Freetown ambao umeletwa na Ndege ya Emirates.

Freetown alikuwa mfanyakazi wa UN na alikuwa akiishi Pakistan na kufanyia kazi huko kwa muda mrefu

Taarifa zinasema kuwa Freetown alifariki katikati ya mwezi wa 6, na suala la kuusafirisha mwili wake kumrudisha nyumbani lilikuwa tata kutokana na hali ya usafiri wa ndege lilivyo kwa sasa.

Mwili wa Freetown ulisafirishwa hiyohiyo jana kuelekea kwao Mkoa wa Njombe

Mungu aiweke pema peponi roho ya mwenzetu Freetown.
 

Aaaaah Aiseee, So Saaad yani. Toke mwezi wa 6???
 

Daaah! Namkumbuka sana huyu Muheshimiwa. Mungu ampe pumziko la milele, Amen
 
Duh! Poleni sana Arusha Wing, pole kwa familia na JF kwa ujumla!
 
Safari umeikamalisha, Mungu ampe pumziko la milele, panapomstahili, pema peponi.
 
Poleni wafiwa
Apumzike kwa Amani Ndugu Yetu
 
Reactions: amu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…