Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Miaka 10 tena kwa Mama Samia.
 
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndugu Kenani Kihongosi amesikitishwa na kauli ya Mwanasiasa wa Upinzani Godbless Lema kunanga Vijana na Watanzania waliojiajiri kupitia Bodaboda.
CCM ni wataalam wa kubadilisha maneno.

Nilikuwepo uwanjani, nilimsikia Lema akiongea kuhusu bodaboda. Concern ya Lema ni kwamba, baada ya muda mfupi, vijana wa bodaboda wataugua maradhi ya kifua,

Sio njema kutumainia kazi ya bodaboda. Serikali ifungue viwanda, serikali iwawezeshe vijana kwenye kilimo. Sio kuwaacha kutegemea Tsh 7000 kwa siku. Huo ndio ulikuwa ushauri wa Lema.

Sasa kwa vile CCM mnawaona Watanzania ni wajinga, mnabadilisha maneno kuwahadaa ambao hawakuwepo kwenye mkutano. Shame on you.... Muda wa kuwahadaa Watanzania umeshapita.
 
Duu Basi mkalitazame
 
Matapeli wakubwa...Bravo Nabii Lema
 
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndugu Kenani Kihongosi amesikitishwa na kauli ya Mwanasiasa wa Upinzani Godbless Lema kunanga Vijana na Watanzania waliojiajiri kupitia Bodaboda.
Vipi ile migao uliyo kuwa una pewa na Sabaya? Kihongosi kaa kimya usitafute watu wfungue file lako kipindi uko Arusha.
 
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndugu Kenani Kihongosi amesikitishwa na kauli ya Mwanasiasa wa Upinzani Godbless Lema kunanga Vijana na Watanzania waliojiajiri kupitia Bodaboda.
Kama akili ya Viongozi wa vijana ndiyo hii ...... No wonder, nimesikia kuwa vijana waliomaliza Vyuo vikuu waende VETA kujifunza....!!
 
Watu wa CCM ni wajinga fullstop yaani wanatakiwa wapanue akili kuhusu ajira bora
 
Lema ana laana ya asili, anafikiri kila mtu anaweza kulelewa bure au kuwa mwizi wa magari
 
1. Ajali
bodaboda wanahusika katika kusababisha ajali nyingi barabarani, tofauti na magari sio rahisi sana kudhibiti bodaboda. Ni bodaboda pekee ambayo utaikuta inaendesha kulia sehemu inatakiwa kuendesha kushoto.

2. Afya
katika bodaboda dereva na abiria wake ndio bodi za chombo, ajali ndogo tu inaweza kusababisha kifo, madhara makubwa kichwani, kukatwa miguu, mikono n.k. Hii inamaanisha kwamba inaleta mzigo mkubwa katika mfumo wa afya ambao umezidiwa kwa uchache wa madaktari.

3. Usalama wa raia na mali zao
Bodaboda zinahusika sana katika matukio ya uhalifu wa silaha na ukwapuaji barabarani kwa sababu ya uwezo mkubwa wa kupenya.

4. Athari kwa sekta muhimu kiuchumi
Kama vile mitumba na nguo za wachina zinavyoendelea kuua na kuzuia kushamiri sekta ya viwanda, Bodaboda ambayo imekuwa kimbilio kwa vijana ni changamoto sana katika kuleta mageuzi ya kiuchumi. Tanzania ina ardhi kubwa ya kulima na kufanya shughuli nyingine ila vijana wanakimbilia kwenye bodaboda tu kwa sababu ni kazi rahisi kuanza nayo.

5. Kutumika vibaya kisiasa
Waendesha magari au ndege huwezi kuwashawishi wakukubali kwa masuala ya hisia tu kwamba umenunua ndege nyingi au umefanya uingizaji wa magari kuwa rahisi. Wao huwa wanaangalia mambo mengine mengi zaidi ya hayo tofauti na bodaboda.

Hata hivyo ukosefu wa fursa na ugumu wa maisha hufanya binadamu wakati mwingine kutokuwa na chaguo zaidi ya kufanya kazi za laana ambazo hajivunii kabisa.
 
Bwana Lema lawama yake ielekezwe kwa ujinga wake wa elimu ndogo aliyonayo kuhuaiana na utajiri mwingi wa nchi zilizo endelea.
Hajui historia ya Canada, USA, UK, Belgium etc na umasikini wa Africa. Anafikiri watanzania wakikataa kazi za Bodaboda, mama lishe, kuuza mkaa, Kulima na jembe la mkono, machinga mara watakuwa matajiri - barabara nzuri, umeme mishahara mikubwa, bei kubwa za bidhaa etc vitaanza kupatikana!
Hakujifunza alipokuwa Canada - ila alikuwa anashangaa tu Canada. Kama angechukua muda Kujifunza na kulinganisha, kazi na mchango unaofanywa na Bodaboda kwa uchumi na maendeleo, angegundua kwamba ni advanced stage ikilinganishwa na process walizopita walioendelea kabla yetu.
Imagine service na kuokoa muda inayo tolewa na Bodaboda sasa, mataifa yaliyo endelea hawakupata service hiyo! Na kama wangeliipata wangekuwa mbali zaidi!
Nafikiri Lema muda aliokaa ulaya hakuutumia Kujifunza vitu vingi. Hivyo, msimlaumu sana - hajui basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…