Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Vicoba sio kuhifadhi pesa. Wanakopeshana na riba inakuwepo, kuna faini ndogo ndogo pia. Ni kanuni ya Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Kama vicoba havina kazi, basi mfumo wa kukopa pesa nyingi benki na kurudisha nyingi kuliko uliyokopa haina maana pia.
Inaonesha Godiblesi yeye haheshimu complexity ya maisha.
 
Asilimia zote nakubal. Angalia wenzetu wanzungu kama wana vikoba. Wenzetu mshaara unapangwa na serkar unajikimu na kuweza ku save. Shida ya sisi uwez save
 
Nenda jeshi la Polisi ukapate takwimu za ajali za bodaboda. Hakuna hata siku moja inayopita bila ya vifo vilivyosababishwa na ajali za bodaboda.

Ajali zipo kwenye shughuli zote, za usafirishaji, uzalishaji, hata kwenye starehe. Lakini ajali kugeuka kuwa janga ni pale idadi yake inapokuwa ya kupindukia.

Uliwahi kusikia kuna hospitali imetenga wodi maalum kwaajili ya waliopata ajali za mabasi? Lakini kwa bodaboda, zipo. Mpaka hapo, hupati tu ujumbe, hata kama huna access ya takwimu za ajali nchini?
 
Huko Vicoba Wana source vitu gani? Hayo unayosema kwani hayafanyiki Veta na sido?
 
Asilimia zote nakubal. Angalia wenzetu wanzungu kama wana vikoba. Wenzetu mshaara unapangwa na serkar unajikimu na kuweza ku save. Shida ya sisi uwez save

Hata Tanzania mbona watu wanasave tu pesa
 
Ni mropokaji haelewi chochote,eti huyu ndio anataka Kugombea na Kuna watu watamchagua 🤪🤪
 

Ndivyo ilivyokuwa mantiki ya kile alichokuwa anakiongea kuanzia mwanzo mpaka mwisho hasa alipogusa hoja ya Hali duni ya Maisha ya mtanzania,

Lema Adili na serikali na CCM, wananchi kwao atake uungwaji mkono.
Nilifurahi aliposema kuwa Wananchi wamelala, wanatetewa lakini wao wapo kimya, akatoa mfano Lissu mpaka anapigwa RISASI wananchi wapo kimya. Badala ya ku-react.
Angesema kuwa Lisuau au yeye alikimbia Nchi akiwa anawatetea wapate Haki zao ikiwemo Haki ya kufanya kile wakipenacho, sio ajabu wapo wanaopendahuo ubodaboda, Ila angewawekea mazingira mazuri wafanye bila Kupata madhara ya ajali za Uzembe, Haki za Kupata bima na kuweka Akiba katika mifuko ya hifadhi n.k
 
Vikoba ni umasikini.
Vimevunja ndoa nyingi.

Mashamba yameuzwa.
NYumba zimeuzwa.
Fanicha ndio usiseme.
 
Kwa hiyo hapa Tanzania Kuna upungufu wa ma operator wa matrekta si ndio? Hiyo unayoita kazi ya kula imewawezesha kuanzisha miradi Mingi tuu
 
Ni kweli
 
Kukosoa na kupinga mambo pasipo kupendekeza njia mbadala wa nini kifanyike ni tatizo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…