Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Bodaboda 😍 wanatuwahisha sana site
Wanasaidia sana japo ni very risky, jana usiku ilikuwa nimuue moja na abiria wake Morogoro road. Anakuja site ambayo gari zinaenda namie ndio nimechomoa gari naikata Eiecher ile narudisha upande wangu tu huyu hapa nikapiga brake ghafla ndio pona yake. 🀣🀣🀣
 
Ndio madhara ya kwenda abroad kuishi haya,ukirudi kila mtu unamwona mshamba,kapitwa na wakati,ananuka,hana elimu wala hana future[emoji28][emoji28].

Kama ana watu wa karibu aambiwe apunguze speed barabara sio ndefu mbele na haijanyooka sana.
 
Faamasiala nini πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ sasa utachagua ukabebe makreti kwa Mo au uendeshe boda boda kwa masaa hayo hayo upate elfu 30.
Lema anasema zinatakiwa winchi kubeba makreti, sio watu,, maana huo mi utwana,

Je, utakuwa tayari mtoto wake akabebe kreti mchana kutwa pale kiwandani coca cola, au utampa pikipiki awe delivery boy
 
Solution lipo ndio maana lema anaongea hivyo solution ni kuwa na mifumo sahihi ya kuandaa vijana katika soko la ajira zenye tija sawa suala la ajira ni changamoto lakini je hakuna ujuzi ambao unaweza kutolewa ili kijana aweze pambania kombe hata nje ya mipaka

Hao boda boda anasema tukisema leo waliosoma na wenye sifa za kupata ajira za ofisini ni asilimia 10 tu wengine hata darasa la Saba hawajamaliza umeona, kwakua ni kazi ya kukaa kijiweni basi wengine hawataki kwenda hata shamba kulima wengine hawataki hatakukaa wakajifunza ujuzi
 
Unaposema boda boda ni kazi ya laana, kusajili laini ni kazi ya kipuuzi hutaki mwanao umuone anaifanya utamfukuza kwako, vikoba ni laana sijui hutaki mkeo ajihusishe navyo kabisa.

]
Ukisikiliza maneno ya Lema Unaweza kufikiri siasa ni simple na kila mtu anaweza kufanya siasa anaorodhesha matatizo alafu haji na solutions alafu anajisifu anawasaidia wananchi kuondokana na umasikini
 
Hivi Bado unapoteza mda kufuatilia huyo KIJANA aitwae Lema? Tumuombe Lema atusaidie huko kanada alikua anafanya KAZI gani kwanzaa
 
Hivi wewe na Lema mnajua kwamba kuna watu wanalipwa elf 4 kwa siku na wengine elfu 6 katika viwanda vya the so called matajiri wa kibongo bongo hawa?

Lema anatambua kuwa kuna graduates wanalipwa laki 2 kwa mwezi katika situation hii ambayo nauli zinakaribia buku na bei ya nafaka kwa kilo ni zaidi ya dollar 1?

Mngeanza na kutatua hizi changamoto nadhani hio option mnayoifikiria ingekuwa na maana zaidi!
 
Ndio madhara ya kwenda abroad kuishi haya,ukirudi kila mtu unamwona mshamba,kapitwa na wakati,ananuka,hana elimu wala hana future[emoji28][emoji28].

Kama ana watu wa karibu aambiwe apunguze speed barabara sio ndefu mbele na haijanyooka sana.
Hahahahahah
 
Kaishi Canada mwaka mmoja tu,amekuwa mjuaji kuliko hata Watanzania wanaoshi huko zaidi ya miaka 20.

Ananikumbusha enzi za utotoni tuko shamba huko,mtoto mwenzetu anakuja Dar likizo week 3 tu,akirudi atawasimulieni mwaka mzima uzuri wa Jiji la Dar es salaam hata kama alifikia Mbagara huko na hakuwahi hata kukanyaga mitaa ya Posta mpya.
 
Shida ni kwamba na wanaoleta taarifa za Lema humu wanadokoa statement tata wanaleta hivyohivyo bila maelezo ya ziada au source of information,watu wanaanza kujadili kila mtu na fikra zake.

Mfano kuna Uziuliwekwa humu,Lema kasema kujenga ukuta Mererani ni ushamba(hio ilikuwa heading)ila source haikuwekwa,nilipofualitilia ni kweli alisema hivyo ila kuna maelezo mengi alitoa kuhusu hilo na alitoa ushauri mzuri tu,na akasema kwa kuwa viongozi wote wapo Arusha(semina) atawashauri mawazo yake.

Nadhani tunahitaji media serious imualike kwa mahojiano atoe ufafanuzi juu ya kauli zake hizi,tujue hasa anamaanisha nini.

Leo East Africa radio walikuwa na uongozi wa Bodaboda Dar,wale viongozi nao walilaumu hio kauli wakisema kwamba watu wanasomesha wanajenga na kwa siku boda hakosi 30,000(Siku mbaya) kwamba kwa mwezi hakosi 800,000 na kwamba wanawazidi hata kada fulani ya waajiriwa serikalini.

Baadae mtangazaji akaanza kuwadadisi,kama mna kipato hicho inakuwaje mnakosa bima ya afya ya 600,000 kwa mwaka?wakaanza bla bla kwamba hio tumetaja ni kama ukiweka akiba,wakaambiwa kwa takwimu za muhimbili kila siku wanapokea majeruhi 6 wa bodaboda pale,wakadai eti hao sio bodaboda ila ni vijana wa mikoani wameletwa kubeba mayai kusambaza kitu ambacho ni uongo.

Je unaweza kufanya kazi ya Bodaboda kuanzia ujana hadi uzee?Je utapenda mtoto wako arithi kazi yako? hawakuwa na majibu ya maana.

Ukweli ni kwamba kauli ya Lema kwa juu juuu inakera ila ukiingia ndani ukweli upo,Ilikuwa wamtafute Lema bahati mbaya naona hawakufanikiwa mpaka kipindi kinaisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…