Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Yule baba Prophet katoa pesa zake milioni 100 kusaidia wananchi ambapo si mbunge wala kiongozi yoyote wa serikali, inatokea tu kajamaa ambako kalikuwa kakilipwa mamilioni ya fedha na posho kibao, na hakakuchangia chochote kwa wananchi, halafu kanatoa kashifa mbele ya haohao wananchi ambao kaliwafanya mgongo wa kupandia eti mmelaaniwa kwa sababu ya biashara zenu za kufukuza upepo?

Siasa zingine za kijinga tu!

Tamko la Lema kuwahusu bodaboda, ni msimamo wa Chadema? Na kama siyo, Lema akemewe mara moja!

Mtu amekuwa mbunge zaidi ya miaka 15, bodaboda alizikuta na akaziacha, lakini hakufanya lolote ili tu kuwatoa hao bodaboda kwenye biashara hiyo ya laana kama anavyodai, isitoshe, bodaboda zimekuwa zikitumika sana kwenye mikutano ya Chadema na zimekuwa zikikiheshimisha chama na Viongozi wake

Sisi tukuiteje?

Ni ujingaa au Canada anataka kuihamishia Tanzania kwa maneno tupu?

Bodaboda zimesomesha watoto na wengine wapo vyuoni wazazi wao wakiwasomesha kwa hizo boda, halafu mtu mmoja tu kutoka Kanada tena kwa ukimbizi wa kuhongwa ili tu aitwe mkimbizi aje kutukana kazi zetu?

Lema, ulilpaswa kuwasimanga boda baada ya kuainisha ulichowafanyia wana Arusha miaka 15 ukiwa mbunge na au ungeshuka na mbadala wa kazi hiyo kutokea huko Canada

Lema, Licha ya kukaa ughaibuni miaka zaidi ya miwili bado haikutosha kuondoa upuuzi wa kufikiri?
lema alipigania haki bungeni swala la kuifanyia nin arusha ni jukumu la serikali inayokusanya kodi kupitia TRA so waulize serikali waliifanyia nini arusha kipindi cha lema au hawakupeleka maendeleo kama alivyosema mungu wao kuwa kwa wapinzani hatapeleka maendeleo by the way lema hajakaa bungen miaka 15 kama ulivyoandika kwenye title yako.
 
Kazi karibu zote ni risk. Unataka waache bodaboda ili wafanye kazi kazi? Ya kulelewa bure kama yeye lema?
Risk nyingi za bodaboda ni za kujitakia.
Kwa nini dereva wa gari anafanya mafunzo kabla ya kupewa leseni lakini bodaboda anajifunza kwa saa 3 na kuingia barabarani?
Aslilimia kubwa ya bodaboda hawana leseni. Wewe unatetea huu upuuzi?!
 
Leo nimeshuhuda bodaboda amegonga gari kwa nyuma ... alafu akakimbia fasta...gari ilikuwa imesimama kwenye mataa
 
1. Ajali
bodaboda wanahusika katika kusababisha ajali nyingi barabarani, tofauti na magari sio rahisi sana kudhibiti bodaboda. Ni bodaboda pekee ambayo utaikuta inaendesha kulia sehemu inatakiwa kuendesha kushoto.
Mabasi na malori nayo ni boda boda ?
 
2. Afya
katika bodaboda dereva na abiria wake ndio bodi za chombo, ajali ndogo tu inaweza kusababisha kifo, madhara makubwa kichwani, kukatwa miguu, mikono n.k. Hii inamaanisha kwamba inaleta mzigo mkubwa katika mfumo wa afya ambao umezidiwa kwa uchache wa madaktari.
Kwa vyombo vyote vya moto haya yana asilimia kubwa kutokea kwa wote.
 
3. Usalama wa raia na mali zao
Bodaboda zinahusika sana katika matukio ya uhalifu wa silaha na ukwapuaji barabarani kwa sababu ya uwezo mkubwa wa kupenya.
Noah nyeusi na tax zenye vioo tinted siku hizi hazitumiki ?
 
4. Athari kwa sekta muhimu kiuchumi
Kama vile mitumba na nguo za wachina zinavyoendelea kuua na kuzuia kushamiri sekta ya viwanda, Bodaboda ambayo imekuwa kimbilio kwa vijana ni changamoto sana katika kuleta mageuzi ya kiuchumi. Tanzania ina ardhi kubwa ya kulima na kufanya shughuli nyingine ila vijana wanakimbilia kwenye bodaboda tu kwa sababu ni kazi rahisi kuanza nayo.
Mna wafikia Indonesia na China kwa idadi ya boda boda zilizo katika matumizi ?
Na
je uchumi wenu na wa China na Indonesia katika criteria zote [ e.g industry ] una fanana ?
 
[emoji848] andika na faida zake basi ili tuone kweli làana nadhani hakuna kazi ambayo haina risk na hizo ambazo umeweka hapo zinaingia sehemu nyingi mfn udereva wa basi,malori n.k
 
5. Kutumika vibaya kisiasa
Waendesha magari au ndege huwezi kuwashawishi wakukubali kwa masuala ya hisia tu kwamba umenunua ndege nyingi au umefanya uingizaji wa magari kuwa rahisi. Wao huwa wanaangalia mambo mengine mengi zaidi ya hayo tofauti na bodaboda.
Waendesha boda boda wakusanyika kwa wingi kumpokea Lema, Lissu, mbowe na viongozi wengine wa chadema katika funguzi za mikutano ya hadhara hapa nchini.
 
Mkuu una miaka mingapi? Huenda tunachangia hoja ya kitoto Cha miaka 16 kisivhojua kuwa Lena Hana vipindi vi 3 vya ubunge
 
Faida zake andika wewe
[emoji848] andika na faida zake basi ili tuone kweli làana nadhani hakuna kazi ambayo haina risk na hizo ambazo umeweka hapo zinaingia sehemu nyingi mfn udereva wa basi,malori n.k
 
Hata hivyo ukosefu wa fursa na ugumu wa maisha hufanya binadamu wakati mwingine kutokuwa na chaguo zaidi ya kufanya kazi za laana ambazo hajivunii kabisa.
Nini maana ya laana ?
 
We chawa tu hauna akili,mbona unahangaika na kulamba viatu vya watu na usiende kujiajiri kama ulivojinasibu hautaki kazi kwenye mashairi yako,kucha kutwa umekaa kushindana na chadema mpaka unaibiwa demu wako
 
Mkuu una miaka mingapi? Huenda tunachangia hoja ya kitoto Cha miaka 16 kisivhojua kuwa Lena Hana vipindi vi 3 vya ubunge
Ulivyoandika tu, sihitaji watu dizaini yako kuchangia hii mada!
 
Lema anakusanya kodi? wajinga wakubwa nyie, mbona watoto wenu hawapo kwenye ajira ya bodaboda? kuna mtoto wa Waziri, RC, KM, RAS, DAS, DC, DED, Mbunge ni bodaboda? ukimtaja mmoja najinyea siku nzima
Mkuu,haiwezekana binadamu wakalingana hata kidogo ,nakushauri kama bado ni kijana mdogo pigania maisha yako huyu pimbi LEMA hawezi kukusaidia chochote zaid ya kukutumia wewe ili aende bungeni na aweze kupata ajira.
 
Back
Top Bottom