Shida ni kwamba na wanaoleta taarifa za Lema humu wanadokoa statement tata wanaleta hivyohivyo bila maelezo ya ziada au source of information,watu wanaanza kujadili kila mtu na fikra zake.
Mfano kuna Uziuliwekwa humu,Lema kasema kujenga ukuta Mererani ni ushamba(hio ilikuwa heading)ila source haikuwekwa,nilipofualitilia ni kweli alisema hivyo ila kuna maelezo mengi alitoa kuhusu hilo na alitoa ushauri mzuri tu,na akasema kwa kuwa viongozi wote wapo Arusha(semina) atawashauri mawazo yake.
Nadhani tunahitaji media serious imualike kwa mahojiano atoe ufafanuzi juu ya kauli zake hizi,tujue hasa anamaanisha nini.
Leo East Africa radio walikuwa na uongozi wa Bodaboda Dar,wale viongozi nao walilaumu hio kauli wakisema kwamba watu wanasomesha wanajenga na kwa siku boda hakosi 30,000(Siku mbaya) kwamba kwa mwezi hakosi 800,000 na kwamba wanawazidi hata kada fulani ya waajiriwa serikalini.
Baadae mtangazaji akaanza kuwadadisi,kama mna kipato hicho inakuwaje mnakosa bima ya afya ya 600,000 kwa mwaka?wakaanza bla bla kwamba hio tumetaja ni kama ukiweka akiba,wakaambiwa kwa takwimu za muhimbili kila siku wanapokea majeruhi 6 wa bodaboda pale,wakadai eti hao sio bodaboda ila ni vijana wa mikoani wameletwa kubeba mayai kusambaza kitu ambacho ni uongo.
Je unaweza kufanya kazi ya Bodaboda kuanzia ujana hadi uzee?Je utapenda mtoto wako arithi kazi yako? hawakuwa na majibu ya maana.
Ukweli ni kwamba kauli ya Lema kwa juu juuu inakera ila ukiingia ndani ukweli upo,Ilikuwa wamtafute Lema bahati mbaya naona hawakufanikiwa mpaka kipindi kinaisha.