ARV uzisikie kwa wenzako, tutumie condom

Anko wangu alipopima tu akakutwa na maambukizi na alikuwa ameshaanza kuumwa, akaanzishiwa dawa haraka na akakubali matokeo na haikuwa siri kwenye familia, ilikuwa akija kwetu muda wa dawa ananiambia ankoo niletee vitu vyangu anameza fresh...alishafariki lakini haikuwa kwa mateso ya enzi zile dawa za kupunguza makali ya huu ugonjwa....!
 
Daaa JF unaweza uonekane wewe una roho ya kifashisti kuchekelea matatizo ya wenzako, kumbe unacheka jinsi tatizo lilivyoelezewa...

Kuna shughuli nyingne inaitwa PEP 72HRS, ile unaweza ukainywa, baada ya masaa kadhaa unatafuta dawa uitapike,
Niliwahi kuuza mechi nikaenda pharmacy wakasema hawana hizo PEP wakaniambia niende Palestina Hospital aisee kufika pale nikalazimishwa kupima kwa nguvu. Baadae ndio nikaenda kuchukua dawa nikapewa 3 kwanza nikaambiwa nyingine nizifuate kesho Yake aisee kufika nakutana na "wadau wa maendeleo" kliniki wamekondeana mpaka aibu.
 
Huu ugonjwa kama umesahaulika vile kwenye kampeni za kinga....mkazo umewekwa kwenye hizo dawa za kufubaza makali.

Habari za radio mbao zinasema vijana wengi sana wanao kwa sasa wanapata huduma katika kliniki mbalimbali, wale wenye majina majina mjini ndio dooh....hatari sana.

Ukimwi upo na siku hizi hauonekani kwa macho walionao wamenawiri shauri ya dawa na 'dayati'.
 
Kwahyo mkuu unatumia pep kumbe? Sio full dose
 
kheri hizo dawa maana unaweza kuishi hata 20 years ila kuna magonjwa kama cancer yakishakutafuna, chances za kutoboa ni ndogo mkuu.

Kula tu njugu zako in peace mkuu #chaMsingiUhaiTu

Usisahau sukari
 
Mkuu kama umeupata moto kwa PISI kai kama binti wa Kagame sikulaumu ila kama umeukwaa kwa baa medi we utakua ni bonge la fa,la!!

 
Matendo kivipi mkuu Kuna ngono hatarishi kukwepa ni ngumu ukiwa makini hupati sasa imagine wafukua tope 95% chance ya kuukwaa ni kubwa mno au ukiwa mlevi ni kuparamiana na kuchubuana had damu unategemea Nini?
I agree with u. we are on the same point.
 
Hivi kwenye hayo madirisha huwa Kuna watu wengi kiasi hicho aisee hadi watengewe sehemu, dah ndio maana Mimi nyegezi sina kabisa kwa mtindo huo wallah
Kuna hosp nilikuaapo wakat nipo Internship , Kwa siku wagonjwa wapya wa huu ugonjwa walikua wakigundulika 20--30 kila siku.


Kwa CTC sasa ndo usiseme


Muhim watu watumie ndom, na hata ukigundulika Ni vema Uanze dawa, dawa zinaongeza maisha marefu na kupunguza usambazaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…