Asafirisha wahamiaji 20 kwa V8 yenye bendera ya CCM

Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma anashikiliwa na Polisi Mkoani Manyara kwa kosa la kusafirisha kinyume na sheria Wahamiaji 20 Raia wa Ethiopia.

Akiongea Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara ACP Lucas Mwakatundu amesema tukio hilo limetokea March 23 2024 ambapo gari hilo limekamatwa katika kizuizi barabara ya Arusha Babati eneo la Minjingu likiwa na Wahamiaji ishirini Raia wa Ethiopia kwenye gari namba T.774 BDL Land Cruiser likiwa na bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM.

“Gari hili V8 lilikuwa na Bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwenye upekuzi tulipoona sura tofauti na Watanzania ilibidi tuweke gari pembeni na baadae kuwashusha tukakuta wapo Wahamiaji 20 kwenye gari V8 na wote uelekeo wao ni kusini mwa Afrika wakitokea usawa wa Arusha, Dereva wa gari hili ni Mkazi wa Dodoma tunamshikilia mpaka sasa na kesho tunatarajia kuwakabidhi Uhamiaji”

Chanzo: Ayo TV

Ni kawaida ya ccm, na huyo ni mwenzao.
 
Una uhakika gani i kama ni mwanachama wa CCM

Bendera inafungwa kwenye gari ya kiongozi wa CCM tu tena mkubwa sio kada yaani huyo kazi anayo guu
Gari inaondoka hiyo

Sheria inatamka wazi ukihifadhi wahamiaji haramu hata kwenye nyumba yako.Nyumba inataifishwa
Chawa wa mama huyo atatoka tu
 
Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma anashikiliwa na Polisi Mkoani Manyara kwa kosa la kusafirisha kinyume na sheria Wahamiaji 20 Raia wa Ethiopia.

Akiongea Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara ACP Lucas Mwakatundu amesema tukio hilo limetokea March 23 2024 ambapo gari hilo limekamatwa katika kizuizi barabara ya Arusha Babati eneo la Minjingu likiwa na Wahamiaji ishirini Raia wa Ethiopia kwenye gari namba T.774 BDL Land Cruiser likiwa na bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM.

“Gari hili V8 lilikuwa na Bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwenye upekuzi tulipoona sura tofauti na Watanzania ilibidi tuweke gari pembeni na baadae kuwashusha tukakuta wapo Wahamiaji 20 kwenye gari V8 na wote uelekeo wao ni kusini mwa Afrika wakitokea usawa wa Arusha, Dereva wa gari hili ni Mkazi wa Dodoma tunamshikilia mpaka sasa na kesho tunatarajia kuwakabidhi Uhamiaji”

Chanzo: Ayo TV
Siyo Jambo jipya Hilo, kuna mambo mabaya zaidi ya hili yanafanyika kwa kutumia magari hayo.
 
Kwa ccm hiyo imekuwa kawaida na wananchi tumeizoea kabisa.imeanza muda mrefu lakini Kwa Sasa imekithiri maradufu kuliko ilivyokuwa awali.
 
Moja ya biashara kubwa Duniani ni hii
imetajirisha watu hii hata huko europe pesa yake ni ndefu mfano wa dhahabu.

imagine kuna mwamba alinunua suti kumi za gharama,sehemu ngumu kupita hao jamaa wanaveshwa suti kali,koti jeupe la udaktari na kile kipima moyo shingoni na wanapita vizuri😁,mambo ni moto.
 
Niliwahi kuambia hao jamaa wahabeshi unaeza kuta hapo katoa dola karibu elf 3 ili kufika anakotaka ..maana ni biashara ya mtandao mkubwa..
 
Back
Top Bottom