Kupata samli unaweza kununua butter ukaichemsha hadi mafuta yakajitenga na solid milk,au machicha then unachuja na kupata samli(ghee).ila sasa sijui kama butter ya supermarket yaweza kuwa natural.
Zamani zilikuwepo mashine tukiziita mashine za shagi,zina mfumo kama wa centrifuge ambamo maziwa huwekwa na kuwa spinned hadi yanajitenga na ile cream ambayo ndo butterfat japo inakuwa bado na kiasi cha water na solidmilk,sasa ili upate samli ile butter kwa kiswahili sijui ndo siagi inapikwa,kipindi kile tukipikia kwenye mapipa,mpaka mafuta yanapatikana then unakamua kwa kitambaa kutenganisha samli na machicha.
Localy zaidi mabibi walikua wanagandisha maziwa then wanayaweka kwenye kibuyu na kuyasuka(kuspin )kibuyu kisha watamwaga maziwa kwenye sufuria ambapo ile cream huja juu,wanaengua cream na kuipika hadi wanapata samli.