Asante Maxence Melo kwa kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan Katiba Mpya LIVE

Asante Maxence Melo kwa kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan Katiba Mpya LIVE

Ila katoa mapendekezo mazuri sana,Raisi ikitokea kafariki uitishwe uchaguzi baada ya miezi miwili,mitatu mingi sana anaweza nogewa

Maoni si haba taabu yao hawana nia njema. Anasema hivi sasa kwa sababu yamewakuta.

Wamekumbuka shika sasa, kumekucha.
 
KIJA YUNNUS akaanza ujinga wake wa kusema"Mama kasema tusubiri kwanza"..ndio Mama kasema hivyo ila Maxence anachoshauri/anachosisitiza ni kuwa mchakato ufanyike haraka..

Mello alitisha sana that day..
Kabisa.

Max alifanya ile interview vizuri sana. Hongera kwake.
 
Katiba mpya inaweza kuandikwa lakini ikawa mbovuuuu kuliko hata iliyopo sasa hivi.

Katiba nzuri ya wananchi haiwezi kuandikwa na wanasiasa.
Sawa mkuu.

Tumuachieni mama alifanyie kazi hilo. Tunamuamini na tunajua Mama atatupatia tunalolitaka.
 
Wanajulikana kwa majina ya vyawa. Walikuwa vinara wa kupinga uwepo wa katiba mpya. Hawakujua rais madarakani anaweza kutangulia pia.

Kundi lile lile la kikabila lililopanga kumzimia mama urais kwa mujibu wa katiba iliyopo.
Na taarifa tunazo kwamba wamepanga kumfelisha mama katika hili.

Wajue tu kwamba mama ni mpango wa Mungu. Atakaejaribu kumfanyia baya lolote lile basi litakalomkuta atajua mwenyewe
 
Kwa wananchi: Tunaendelea kusisitiza kwamba, Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.

Viva Mama Samia! Muda ni sasa!
Tatizo la watu kama wewe ni kuwa mnajichanganya, pengine kwa kutojua.

Unamwomba mtu Katiba mpya. Hiyo pekee inakuonyesha kwamba anaweza akakataa au akaendelea kuykdanganya, hasa kwa mtu uliyejipambanua mbele kabisa jinsi unavyomsifia hapa.

Kesho utakuja na visingizio chungu nzima, akishakudanganya au kukatalia ombi lako.

Hatuwezi kuwa tunabaki kuwa omba omba kwa hawa waTanzania wenzetu. Tena tunaomba kitu ambacho ni HAKI yetu kukipata!
 
Katiba mpya ndio suluhisho la Matatizo mengi ya nchi yetu. Sio matatizo yote, narudia kusema matatizo mengi. Maana katiba ni muongozo tu kama ilivyo Qur an au bible.

Leo Qur an ipo na waislam hawaofuati, bible ipo na wakristo hawaifuati ni kipi kinachokuonyesha watanzania watakuja kuifuata katiba mpya???

Kwahiyo katiba mpya tunaitaka maana itatusaidia kupunguza matatizo mengi yanayotusibu Watanzania.
Ndiyo itapunguza matatizo mengi ya watanzania, muda wote katiba inafatwa tena kwa ukubwa sana hata pale kwenye mwanya mdogo pasipofatwa watu wanajulisha serikali mapungufu hayo na yasipofatwa kelele za kuikumbusha serikali zinaendelea.
 
Kwenye kuuzwa hapana... Alichokiongea ni muhimu sana... Yes, tutaingia gharama za uchaguzi, lakini ndo gharama za demokrasia
Mkuu,

Wakati wa kampeni unajua kwanini tunapigia kura rais na makamo wake??

Hivi Watanzania, mimi nlidhani mnachagua sera?? Badala ya kulilia mifumo iweke sawa ili yoyote atakaefanikiwa kuingia iwe tu ni mifumo ipo nyinyi ndio kwanza mnaongelea sijui kuingilia dirishani.
 
Ila katoa mapendekezo mazuri sana,Raisi ikitokea kafariki uitishwe uchaguzi baada ya miezi miwili,mitatu mingi sana anaweza nogewa

Maoni si haba taabu yao hawana nia njema. Anasema hivi sasa kwa sababu yamewakuta.

Wamekumbuka shuka sasa, kusha kucha.
 
Ni wazo zuri lakini sio wakati sahihi.Panahitajika political willingness ya hali ya juu sana kufanikisha wazo hili.Nazungumzia utayari wa watu Ku sacrifice masilahi yao ya sasa kwa ajili ya manufaa ya vizazi vijavyo,siuoni utayari huo katika taifa hili kwa sasa.
Kabla sijajibu mkuu, tafadhali naomba ongezea maelezo zaidi.

Hebu tuonyeshe hiyo willingness haipo kivipi?? Indicators ni zipi.?

Maana wenye maslahi daima hawatokubali kupoteza maslahi yao. Mbona mzee kikwete aliuanzisha mchakato vizuri tu na tulikuwa tunakwenda??? Inahitaji kiongozi kukaza tu kwamba katiba lazima ipatikane.

Hebu please ongezea maelezo kwa faida ya wengi.

Angalizo: Mama ataupitia huu uzi, kwa hiyo tumsaidieni Mama mawazo hapo please.
 
Ile interview niliipenda Sana na nilipata kujifunza kutoka kwake ya kwamba tusiogope chochote Wala yeyote ilimradi tu sheria haivunjwi.

Akasisitiza kitu Cha kuogopa ni woga peke yake!

Asante sama maxence melo
 
Back
Top Bottom