Asante Maxence Melo kwa kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan Katiba Mpya LIVE

Asante Maxence Melo kwa kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan Katiba Mpya LIVE

Wananchi tutamlazimisha akikataa,
Kama nyinyi mlivyotaka kumlazimisha dikteta atawale milele, hatma yake ameangamia milele
Mkuu ndani ya chama tupo ambao hatukukubaliana hata kidogo na yaliyokuwa yakifanywa.

Najua tunajumuishwa sote na hatuna budi kupokea lawama hilo.
 
Unaongelea haki yetu?? Mchungaji Mtikila kaondoka hajaipata "haki yake" , unalijua hili???
Kwa hiyo wewe na Mtikila mna tofauti gani?

Akheri ya Mtikila mara mia kuliko wewe.

Andiko lako lote ni la aibu. Hebu jaribu kujisoma tena uone usivyojua unachokitafuta. Huwezi kuwa sehemu mbili zinazopingana katika andiko moja. Watu waelewe lipi!
 
Pamoja mkuu.

Tumuunge mkono Mama na furaha inakuja.

Unaona Umma ulivyofurahi kwa kilio Chao cha muda mrefu juu ya DC Sabaya kusikilizwa na mamlaka na uchunguzi kufanyika???

Halafu mtu kama Kalamu1 anahoji why tunamuomba omba Mtanzania mwenzetu kwa mambo ambayo ni haki yetu??

Anasahau kuonana na Rais ni haki ya kila Mtanzania lakini mtu kama Mbowe imebidi aombe na asubirie pia kwenye foleni.

Huyu Sabaya si alikuwepo wakati wa hayati Magufuli?? Mbona aliangaliwa tu?? Na hatukuwa na cha kufanya!!!!
EeenHeee, kuomba kuonana na rais unakufananisha na kuomba upewe katiba mpya ya nchi?

Mbona hii inasikitisha sana!
 
Hajaingilia dirishani kumbuka wote wawili walizunguka nchi nzima wakiomba kura.
Hata kule US ikitokea Biden mwenye miaka 79 akafariki yule mama anachukua nchi.

Acheni dharau kijana.
Marekani hawana Waziri Mkuu kwa hiyo kazi za Waziri Mkuu zinafanywa na Makamu wa Rais ndo maana wa Marekani pia ndo Mwenyekiti wa Senate tofauti na wa kwetu anayengoja miaka 10 bila kazi mpaka Rais afariki ili aanze kazi ya Urais. Rais asipokufa madarakani, Makamu atakuwa amelipwa mshahara muda wote kumwombea afe ili arithi!
 
Katiba mpya ndio suluhisho la Matatizo mengi ya nchi yetu. Sio matatizo yote, narudia kusema matatizo mengi. Maana katiba ni muongozo tu kama ilivyo Qur an au bible.

Leo Qur an ipo na waislam hawaofuati, bible ipo na wakristo hawaifuati ni kipi kinachokuonyesha watanzania watakuja kuifuata katiba mpya???

Kwahiyo katiba mpya tunaitaka maana itatusaidia kupunguza matatizo mengi yanayotusibu Watanzania.
Yap! ita solve 75% ya matatizo yetu
 
Marekani hawana Waziri Mkuu kwa hiyo kazi za Waziri Mkuu zinafanywa na Makamu wa Rais ndo maana wa Marekani pia ndo Mwenyekiti wa Senate tofauti na wa kwetu anayengoja miaka 10 bila kazi mpaka Rais afariki ili aanze kazi ya Urais. Rais asipokufa madarakani, Makamu atakuwa amelipwa mshahara muda wote kumwombea afe ili arithi!
Makamu anafanya kazi hali mshahara wa bure.

Mama Samia alikuwa anahudhuria mikutano ya UN pia alikwenda Afrika ya kusini kumwakilisha hayati JPM.

Tatizo letu la jumla ni kuwa na fikra za kudharau kazi ngumu wanazofanya viongozi wa nchi.

Urais kuukosoa ni kazi nyepesi lakini ni shughuli nzito sana.
 
Tatizo clouds wanaweza hata kuficha maneno ya melo ili kuhakikisha mama hayasikii , sijawahi kuiamini hii media
 
Katika katiba mpya kiwepo kipengele cha ikitokea Rais amefariki au kushindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu zozote uchaguzi ufanyike ndani ya miezi 3 mambo ya mtu kuingilia dirishani hatutaki tena.
Na wachini anaweza kumuondoa wa juu yake ili akae yeye hii mbaya sana
 
Katika katiba mpya kiwepo kipengele cha ikitokea Rais amefariki au kushindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu zozote uchaguzi ufanyike ndani ya miezi 3 mambo ya mtu kuingilia dirishani hatutaki tena.
Akili imekuruka, akiwa anaomba kura kwa nafasi ya ugombea mwenza ukumuona? Au unajifanya hujui nafasi hiyo inamaana gani? Na kwa taarifa yako, huyu ni bora kuliko huyo uliemwabudu!
 
Makamu anafanya kazi hali mshahara wa bure.

Mama Samia alikuwa anahudhuria mikutano ya UN pia alikwenda Afrika ya kusini kumwakilisha hayati JPM.

Tatizo letu la jumla ni kuwa na fikra za kudharau kazi ngumu wanazofanya viongozi wa nchi.

Urais kuukosoa ni kazi nyepesi lakini ni shughuli nzito sana.
Tatizo kubwa sana hili.

Hata kwenye kampuni tu za kawaida ni kwamba boss anakuwa hana kazi. Hii mentality ndiyo iliyojengeka miongoni mwetu
 
mama alishatoa msimamo wake kuhusu swala la katiba
Na ndio tupo tunasubiria.

Tunamuombea kwa Mungu kila Leo asije akabadilisha au akabadilishwa mawazo yake juu ya suala hili. Lakini pia tunamuombea kwa Mungu ampe umri na uwezo wa kukamilisha azma yake hii.
 
Back
Top Bottom