Asante Maxence Melo kwa kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan Katiba Mpya LIVE

Asante Maxence Melo kwa kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan Katiba Mpya LIVE

Kabla sijajibu mkuu, tafadhali naomba ongezea maelezo zaidi.

Hebu tuonyeshe hiyo willingness haipo kivipi?? Indicators ni zipi.?

Maana wenye maslahi daima hawatokubali kupoteza maslahi yao. Mbona mzee kikwete aliuanzisha mchakato vizuri tu na tulikuwa tunakwenda??? Inahitaji kiongozi kukaza tu kwamba katiba lazima ipatikane.

Hebu please ongezea maelezo kwa faida ya wengi.

Angalizo: Mama ataupitia huu uzi, kwa hiyo tumsaidieni Mama mawazo hapo please.
Swala sio tu kupata katiba mpya,,muhimu zaidi ni kupata katiba itakayokidhi matarajio ya nyakati tulizopo.Ni kweli palianzishwa mchakato wakati wa Rais kikwete lakini mchakato uliharibika baada ya mapendekezo muhimu ya tume ya jaji warioba kutupwa pembeni,na hapo ndipo nikasema political willingness ni muhimu sana na bahati mbaya sioni dalili ya hali hii kubadilika miaka ya hivi karibuni.
 
Alichoona Cha Maana huyu jamaa wa Jamiiforum ni kuomba Katiba. Itasaidia vipi Maendeleo ya nchi hii? Wakenya walipata Katiba mpya imewachosha kila mtu ana Sharubu huko

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Ndo tunataka demokrasia ina gharama zake pamoja na hizi,halafu hatutegemei Kifo kitokee mara kwa mara,kuliko kupata Raisi ambaye hakuchaguliwa kuwa Raisi bali Makamu kama ilivyotokea kwa hili libushuti
Mkuu,

Tafadhali uwe na adabu na heshima. Haikugharimu chochote.

Hii inaakisi malezi uliyokulia na inakuondolea utu wako. Tunamzungumzia rais wa JMT hapa.
 
Sawa ila kwa sasa wacheni ujuaji.

Tume ya warioba ilipopita kukusanya maoni hukutoka, ukatuona sisi tuliokwenda kutoa maoni ni wajinga. Leo unajifanya una kimbelembele cha kutoa maoni.

Tulia kwanza mama aliweke sawa hili halafu maoni yako yataanza kupokelewa. Wewe unadhani uchaguzi wa rais unafanyika tu kiholela holela???
The best thread ever; asante sana
 
Tatizo la watu kama wewe ni kuwa mnajichanganya, pengine kwa kutojua.

Unamwomba mtu Katiba mpya. Hiyo pekee inakuonyesha kwamba anaweza akakataa au akaendelea kuykdanganya, hasa kwa mtu uliyejipambanua mbele kabisa jinsi unavyomsifia hapa.

Kesho utakuja na visingizio chungu nzima, akishakudanganya au kukatalia ombi lako.

Hatuwezi kuwa tunabaki kuwa omba omba kwa hawa waTanzania wenzetu. Tena tunaomba kitu ambacho ni HAKI yetu kukipata!
Kuna masuala katika maisha yapo hivyo hivyo yalivyo hata iweje.

Ndivyo historia inavyosema na ndivyo itakavyoendelea kuwa. Miaka na miaka dahari na dahari.

Okey unachotaka kama sio kumuomba, tufanyeje?? Mapambano ya kwanza ya kupatikana katiba mpya yalianzishwa na CUF Habari miaka ya mwanzoni mwa 90 (1994 nadhani). Hiyo ni kutokana na mfumo wa vyama vingi ulivyoonekana ulivyo. Je mapambano hayo yamefikia wapi???

Kumefanyika mangapi ndani ya miaka 30 iliyopita kuhusu kupatikana kwa katiba mpya?? Yapi yamefanikiwa???

Mimi naongea bila mihemko, uwezekano wa hili kufanyika ni kupitia huruma ya Mama na hiyo ndio REALITY. Kama Mzee Kikwete alivyotaka, na mtangulizi wake alivyokataa. Kwahiyo ni maono ya individual (I am sorry).

Unaongelea haki yetu?? Mchungaji Mtikila kaondoka hajaipata "haki yake" , unalijua hili???
 
Ndiyo itapunguza matatizo mengi ya watanzania, muda wote katiba inafatwa tena kwa ukubwa sana hata pale kwenye mwanya mdogo pasipofatwa watu wanajulisha serikali mapungufu hayo na yasipofatwa kelele za kuikumbusha serikali zinaendelea.
Ni kweli mkuu.
 
Ile interview niliipenda Sana na nilipata kujifunza kutoka kwake ya kwamba tusiogope chochote Wala yeyote ilimradi tu sheria haivunjwi.

Akasisitiza kitu Cha kuogopa ni woga peke yake!

Asante sama maxence melo
Hawa watu aina ya Maxence Melo huwa ni very rare kupatikana kwenye jamii.

Umemsikia akisema mamlaka zilivyomuita kupata mawazo yake. Viva JF
 
Swala sio tu kupata katiba mpya,,muhimu zaidi ni kupata katiba itakayokidhi matarajio ya nyakati tulizopo.Ni kweli palianzishwa mchakato wakati wa Rais kikwete lakini mchakato uliharibika baada ya mapendekezo muhimu ya tume ya jaji warioba kutupwa pembeni,na hapo ndipo nikasema political willingness ni muhimu sana na bahati mbaya sioni dalili ya hali hii kubadilika miaka ya hivi karibuni.
Hili mkuu halitoweza kubadilika milele. Lazima tutambue udhaifu wa kibinaadam.

Ila ni kweli usemayo pia.

Muhimu Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.

Hivi unadhani kuchelewa chelewa kwa hili jambo ni kwa sababu mama anatafuta watu ambao hawatomuangusha???
 
Alichoona Cha Maana huyu jamaa wa Jamiiforum ni kuomba Katiba. Itasaidia vipi Maendeleo ya nchi hii? Wakenya walipata Katiba mpya imewachosha kila mtu ana Sharubu huko

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
Toa maoni yako mkuu.

Je unadhani katiba ya sasa inaweza saidia kwa kiasi kikubwa kutufikisha tunakokwenda?
 
The best thread ever; asante sana
Pamoja mkuu.

Tumuunge mkono Mama na furaha inakuja.

Unaona Umma ulivyofurahi kwa kilio Chao cha muda mrefu juu ya DC Sabaya kusikilizwa na mamlaka na uchunguzi kufanyika???

Halafu mtu kama Kalamu1 anahoji why tunamuomba omba Mtanzania mwenzetu kwa mambo ambayo ni haki yetu??

Anasahau kuonana na Rais ni haki ya kila Mtanzania lakini mtu kama Mbowe imebidi aombe na asubirie pia kwenye foleni.

Huyu Sabaya si alikuwepo wakati wa hayati Magufuli?? Mbona aliangaliwa tu?? Na hatukuwa na cha kufanya!!!!
 
Hii iliyopo inatutosha.
Mengine watatuongezea wazungu, hata haina haja ya katiba maana hata hii tunaivunja, tuchanganywe na vitu vingi
 
Back
Top Bottom