Asante Maxence Melo kwa kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan Katiba Mpya LIVE

Wananchi tutamlazimisha akikataa,
Kama nyinyi mlivyotaka kumlazimisha dikteta atawale milele, hatma yake ameangamia milele
Mkuu ndani ya chama tupo ambao hatukukubaliana hata kidogo na yaliyokuwa yakifanywa.

Najua tunajumuishwa sote na hatuna budi kupokea lawama hilo.
 
Unaongelea haki yetu?? Mchungaji Mtikila kaondoka hajaipata "haki yake" , unalijua hili???
Kwa hiyo wewe na Mtikila mna tofauti gani?

Akheri ya Mtikila mara mia kuliko wewe.

Andiko lako lote ni la aibu. Hebu jaribu kujisoma tena uone usivyojua unachokitafuta. Huwezi kuwa sehemu mbili zinazopingana katika andiko moja. Watu waelewe lipi!
 
EeenHeee, kuomba kuonana na rais unakufananisha na kuomba upewe katiba mpya ya nchi?

Mbona hii inasikitisha sana!
 
Hajaingilia dirishani kumbuka wote wawili walizunguka nchi nzima wakiomba kura.
Hata kule US ikitokea Biden mwenye miaka 79 akafariki yule mama anachukua nchi.

Acheni dharau kijana.
Marekani hawana Waziri Mkuu kwa hiyo kazi za Waziri Mkuu zinafanywa na Makamu wa Rais ndo maana wa Marekani pia ndo Mwenyekiti wa Senate tofauti na wa kwetu anayengoja miaka 10 bila kazi mpaka Rais afariki ili aanze kazi ya Urais. Rais asipokufa madarakani, Makamu atakuwa amelipwa mshahara muda wote kumwombea afe ili arithi!
 
Yap! ita solve 75% ya matatizo yetu
 
Makamu anafanya kazi hali mshahara wa bure.

Mama Samia alikuwa anahudhuria mikutano ya UN pia alikwenda Afrika ya kusini kumwakilisha hayati JPM.

Tatizo letu la jumla ni kuwa na fikra za kudharau kazi ngumu wanazofanya viongozi wa nchi.

Urais kuukosoa ni kazi nyepesi lakini ni shughuli nzito sana.
 
Tatizo clouds wanaweza hata kuficha maneno ya melo ili kuhakikisha mama hayasikii , sijawahi kuiamini hii media
 
Katika katiba mpya kiwepo kipengele cha ikitokea Rais amefariki au kushindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu zozote uchaguzi ufanyike ndani ya miezi 3 mambo ya mtu kuingilia dirishani hatutaki tena.
Na wachini anaweza kumuondoa wa juu yake ili akae yeye hii mbaya sana
 
Katika katiba mpya kiwepo kipengele cha ikitokea Rais amefariki au kushindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu zozote uchaguzi ufanyike ndani ya miezi 3 mambo ya mtu kuingilia dirishani hatutaki tena.
Akili imekuruka, akiwa anaomba kura kwa nafasi ya ugombea mwenza ukumuona? Au unajifanya hujui nafasi hiyo inamaana gani? Na kwa taarifa yako, huyu ni bora kuliko huyo uliemwabudu!
 
Yap! ita solve 75% ya matatizo yetu
Kabisa mkuu.

Na naamini Mama ameliona hili na analifanyia kazi tayari.

Watanzania tujue kwamba hili suala haliwezi kufanyika tu ghafla bin vuup
 
Tatizo kubwa sana hili.

Hata kwenye kampuni tu za kawaida ni kwamba boss anakuwa hana kazi. Hii mentality ndiyo iliyojengeka miongoni mwetu
 
mama alishatoa msimamo wake kuhusu swala la katiba
Na ndio tupo tunasubiria.

Tunamuombea kwa Mungu kila Leo asije akabadilisha au akabadilishwa mawazo yake juu ya suala hili. Lakini pia tunamuombea kwa Mungu ampe umri na uwezo wa kukamilisha azma yake hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…