Una mimba yake baada ya kukusokotaSijui kwanini nimepatwa na kichefuchefu baada ya kusoma nusu tu ya huu Uzi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Una mimba yake baada ya kukusokotaSijui kwanini nimepatwa na kichefuchefu baada ya kusoma nusu tu ya huu Uzi.
Tukio lililotokea jana la Mheshimiwa Membe Kutangaza Kujitoa "RASMI" ndani ya chama cha CCM sisi wapenzi wa Demokrasia tumelipokea kwa furaha kubwa, na kwa hakika limethibitisha jambo moja kuhusu Mheshimiwa Membe, nalo ni kwamba Brother Bernard Kammilius Membe hatanii, habeep, Anapiga!. Sisi wapenda demokrasia tunachambua kitendo hicho cha Membe kama ifuatavyo:
1. Membe ameukwepa mtego aliokuwa amewekewa na Jiwe
Sote tunajua wazi, Kufukuzwa kwa uananchama wa Ndugu Membe kulitokana na hofu tu ya Jiwe asipate ushindani ndani ya Chama katika kinyang'anyiro cha kugombea uchaguzi kupitia CCM. Maamuzi ya kumfukuza uanachama hayakuwa halali kwa mujibu wa katiba ya chama chao kwa hiyo kikanuni Membe alikuwa bado ni mwanachama halali kabisa ila kwa mujibu wa Udikteta wa mtu fulani hakuwa mwanachama.
Kikao kinachopaswa kuthibitisha kufukuzwa uanachama wa Membe ni halmashauri kuu ya chama, kwa hiyo ni dhahiri kikao hicho kingeitishwa baada ya zoezi la kuchukua fomu ndani ya chama hicho kufungwa na hivyo kama maamuzi ya kumfukuza yangekubaliwa au kukataliwa na kikao hicho tayari Membe angekuwa ameshapitwa na deadline ndani ya chama ya kuchukua fomu, na pia kwa muda huo tayari angekuwa amechelewa basi la upinzani ambalo by that time lingekuwa limeshaweka tayari options zake!
Kitendo cha Membe kuamua kuchomoka mwenyewe RASMI sasa ni timing nzuri sana, na hii inathibitisha uwezo mkubwa wa Mheshimiwa Membe wa kupiga mahesabu ya kisiasa!. Sasa hivi yupo kwenye better position kisiasa kuliko kama angeendelea kung'ang'ania kusubiri maamuzi ya kikao cha Halmashauri kuu Taifa ya CCM juu ya hatma yake.
2. Membe ana uchungu na nchi hii na ni mzalendo wa kweli
Kitendo cha kupambana akiwa ndani ya chama, wakati kila mtu ndani ya CCM akiwa ameufyata, kuogopa au kujipendekeza kwa Jiwe, hata hivyo Membe aligoma katakata kulamba viatu vya Jiwe. Membe alisimama na kusema ukweli juu ya namna nchi inavyoendeshwa. Membe anakumbukwa kwa kukemea siasa za hofu, siasa za kuumiza wapinzani, siasa za maguvu badala ya kupambana kwa hoja. Wakati Membe anasimama na kuyazungumza haya, hakuna key figure ndani ya CCM aliyekuwa akisimama waziwazi na kuyasemea haya. Kwa muktadha huu namuona Membe kama mtu ambaye enzi za ujana wake alifanya kazi Ikulu ya mwalimu nyerere kwa muda mrefu, Ni dhahiri ameathiriwa sana na falsafa za bosi wake huyo wa zamani katika kusimama bila woga kutetea haki na kupinga na kuchukizwa na vitendo vya uonevu dhidi ya watu wengine. Kwa muktadha huu ni dhahiri Membe ni mzalendo wa kweli sana.
3. Upinzani hauna haja ya kumhofia mheshimiwa Membe
Kuna wale ambao walikuwa dissapointed na Ujio wa Lowasa na kitendo ambacho Lowasa aliwafanyia wapinzani. Kiukweli kabisa siyo sahihi kumlinganisha mheshimiwa Membe na Lowasa. Kwanza Malengo ya kugombea urais kati ya Lowasa na Membe ni tofauti. Drive mojawapo kubwa ya Lowasa ya kugombea uraisi kwa udi na uvumba ilikuwa ni Kusettle score na akina JK. Lowasa alitaka kuwaonyesha kuwa naye anaweza kukalia hicho kiti akawanyoosha kama walivyomnyoosha yeye kwenye Richmond.
Lowasa hajawahi kuwa na Ajenda ya kupanua demokrasia zaidi au kutetea utawala wa sheria na ndiyo maana hajawahi tangu akiwa ndani ya CCM au nje ya CCM kutetea demokrasia pana isipokuwa tu pale maslahi yake yalipoguswa (mfano kutohojiwa kwenye ishu ya richmond, au alipokatwa ndani ya CCM). Tofauti na Membe ambaye kwenye utawala huu, kaonyesha wazi hapendi mambo ya kidiktetadikteta. Kwa muktadha huu, values za Membe zinaalign zaidi na msimamo wa upinzani kuliko Lowasa, hivyo ni sahihi wapinzani kumpokea na kushirikiana naye kulichomoa Jiwe kwenye uchaguzi unaokuja.
4. Kama CCM inanunua wapinzani, kuna ubaya gani upinzani ukachukua Majembe yanayoikacha CCM bure?
Siasa ni watu na mikakati. Kitendo chochote kinachochochea mgogoro su dissatisfaction kwenye kambi ya mwenzio basi kwako ni faida. Kitendo chochote kinachopelekea kuondoka kwa mwanachama au waunga mkono wa chama hicho na kuja kambi yako kisiasa ni jambo zuri cha msingi liwe managed vizuri!. Kama CCM inanunua wapinzani, kwa nini upinzani uone haya kuchukua watu potential waliomo ndani ya CCM?
Membe siyo mtu mdogo, ni mtu mzito, ana watu wengi mikoa ya kusini waliochoshwa na kuonewa kwao kwenye ishu nyingi ikiwemo korosho. Utamuachaje mtu kama huyu?, Yaani chance ya kupata kura za kusini uiachie hivi hivi wewe utakuwa mwanasiasa gani?. Najua hofu ni Lowasa, lakini kimsingi Namna issue ya Lowasa ilivyokuwa handled toka mwanzo ilikosewa. Lowasa alitakiwa apewe terms siyo yeye kudictate terms all tje time. Naamini Membe atakuwa teamworker zaidi kuliko kujiinua na kutaka chama na upinzani kumtumikia yeye badala ya yeye kushirikiana na wenzie as a team kuleta mabadiriko chanya ndani ya nchi.
5. Wananchi wanangoja kwa hamu maamuzi ya upinzani
Kiukweli kabisa kabisa kuna kundi la wana CCM wanaujuua ukweli kuwa upinzani kwa sasa ni kama volcano iliyodormant, wanajua kuwa upinzani upo na una nguvu isipokuwa kwa utaratibu wa kidikteta uliofanywa na utawala huu uko dormant temporarily. Nguvu hii ya Upinzani inahitaji Spark ili ilipuke, Spark kubwa ni kuonyesha Umoja, Mshikamano na kuwapa wananchi mtu aliyepikwa akapikika kiuongozi, mtu ambaye ana uwezo wa ushawishi na kujenga hoja, mtu ambaye akili yake ni inacharge.
Kwa hakika upinzani utanufaika sana na uwepo wa Membe katika rank za majemedari wao wa kulichomoa jiwe kwenye uchaguzi ujao. Hebu fikiria vichwa kama Lissu, Zitto, Mnyika, Mbowe, Maalim, Membe, Nyalandu vishirikiane kuzunguuka nchi nxima kupiga kampeni ya kulichomoa jiwe hali ya kisiasa nchini itakuwaje?. Mumi naona Patachimbika aisee, CCM watakuwa na wakati mgumu sana.
Hitimisho
Kitendo alichokifanya Membe cha kukataa kulamba viatu, na kusimama ndani ya chama kutaka mtawala anayekuwa amemaliza mhula wake wa kwanza awe challenged ni kitendo kizuri sana kwa mustakbali wa demokrasia na maendeleo yetu. Kitendo hicho kinasaidia mtawala asijione yuko entitled kutawala miaka kumi, bali aone kuwa kazi yake itakuwa evaluated kila baada ya miaka mitano na asipotosha chama kitamtoa.
Kwa muktadha huu Membe kapigania haki za wana CCM wengi kwenye suala la haki ya kuchagua au kuchaguliwa, haki ambayo pia inalindwa na katiba ya nchi. Kwa mitendo hiki tu ni dhahiri pia kuwa kama Membe atakuwa raisi, atatawala kwa mujibu wa sheria na katiba na hivyo hatokuwa dikteta!
Kwa maana hiyo kama ukinipa uchaguzi leo kati ya Membe na Magufuli, Membe anaweza kuwa booonge la raisi
Membe yuko vizuri
Membe anafaa!
Hivi nyie wenzetu huwa mnapata wapi hela za kina Membe? Maana hela ya Lowassa sikuipata, na hii ya Membe pia sijaipata. Naona nyie wenzetu mnaopata hela za hawa wazee wa ccm, mna nguvu za kuandika makala za kuwapamba, lakini matokeo yote yanafahamika. Ila somo la Lowassa liko vizuri kwenye kichwa cha kila mpinzani wa kweli asiye na maslahi binafsi na hao wazee wasaka madaraka toka ccm. Mleta uzi angalia pesa za Membe zisikufanye uchafue taswira ya upinzani, kwa sababu ya maslahi yako binafsi.
Aagh acha kupiga ramli!Wanaojishtukia ni chadema, wampe membe au wasimpe?
Mbona umeongea kwa jazba Sana? Wewe utakuwa mke mkubwa wa Membe bila Shaka.Una mimba yake baada ya kukusokota
Una haki ya kuwa skeptical
Lakini siyo alli situations are the same.
Siasa siyo linear kwamba lazima points zote zikae ndani ya msitari mmoja, kwa hiyo huwezi kutabiri upinzani utakuwaje nyakati za Membe kwa kuangalia ulikuwaje nyakati za Lowasa!
Membe na Lowasa ni watu wawili tofauti!
Chama chochote cha siasa mtaji wake ni watu, hivyo mimi naona chama kukataa kupokea mtu fulani kwa sababu nyepesi nyepesi ni udhaifu wa hali ya juu.Hivi nyie wenzetu huwa mnapata wapi hela za kina Membe? Maana hela ya Lowassa sikuipata, na hii ya Membe pia sijaipata. Naona nyie wenzetu mnaopata hela za hawa wazee wa ccm, mna nguvu za kuandika makala za kuwapamba, lakini matokeo yote yanafahamika. Ila somo la Lowassa liko vizuri kwenye kichwa cha kila mpinzani wa kweli asiye na maslahi binafsi na hao wazee wasaka madaraka toka ccm. Mleta uzi angalia pesa za Membe zisikufanye uchafue taswira ya upinzani, kwa sababu ya maslahi yako binafsi.
Kama unafahamu ayo tulia mgombea wenu yupo salamaMembe anakuzwa sana, jamaa ni under dog tu
Hata kwny cabinet ya kwanza ya Jk iliyojaa vingunge 2005 alikuwa Naibu Waziri na kilichomuibua ni shavu alilopata Migiro
JK Kamtumia kama chambo cha kuwaingiza maboya kina Lowasa miaka ile wakajikuta wanatumia nguvu kupambana na kivuli na kumuacha Mgombea wa Chama salama
'…Wewe ( JPM) nenda kachukue fomu, …kufaa kwako au kutokufaa tutajua sie…'_Jk 2015
Siku ya kukabidhiwa Tausi kwa Ma Rais wastaaf…Jpm alijikuta anaropoka kuwa Jakaya alianza kumtembeza Ikulu na kumkabidhi Ofisi kidogo kidogo hata kabla kampen hazijaanza…
Membe kasahau kuwa Seif alishindwa kuwa Rais 1984, JAN6 mpaka leo ni mwaka wa 36 anamaliza soli za viatu
Umeshindwa kuwa Rais ukiwa Ccm ndo utaweza kupitia ACT?
Mimba changa na kufukunyuliwa tope.Sijui kwanini nimepatwa na kichefuchefu baada ya kusoma nusu tu ya huu Uzi.
Uongo wa CCM police ipo uko uko jeshi na vifaru bado na membe basi uo upinzani ni noma sanaMembe ni kazi maalum..kea kuuwa upinzani tusidanganike
Ona hii takataka inamshauri membe[emoji23]Amsehindwa nini kusubiri mkutano mkuu?
Mbona alisema yeye bado ni mwanachama na ansubili mkutano mkuu ndo apate maamuzi ya mwisho?
Mfa maji haishi kutapatapa, jana kasema hili leo kaja na lingine, hayo yote anahangaika ili vyama pinzani vimuone anafaa, mara arudishe kadi na kuandika barua kwa kushukuru, kwani angekaa kimya bila kushukuru ingekuwaje?
1 anataka siku akishindwa huo arudi CCM?
2anataka kuonyesha upinzani kuwa kahama CCM?
Membe hataaminika kama anavyodhni na upinzani,
kinachotakiwa ale nao mkataba kuwa endapo atawaongezea wabunge basi wawe wanamlipa sehemu ya ruzuku kwa kazi aliyofanya.
Chama chochote cha siasa mtaji wake ni watu, hivyo mimi naona chama kukataa kupokea mtu fulani kwa sababu nyepesi nyepesi ni udhaifu wa hali ya juu.
B.M ana uhuru kikatiba kujiunga na chama chochote cha siasa.
Suala la kupewa nafasi fulani kwenye chama husika, hapo inategemeana na Falsasa & misimamo ya chama.
Ona hii takataka inamshauri membe[emoji23]
Kama wewe unavyomwabudu magufuli na wengine wanamuita yesuKwani membe ni nani katika dunia hii?
Wajinga kama wewe ndo unamwabudu,
Wewe unadhani membe hawezi kukosea?
Endeleeni kumdanyanya na yeye anajifanya kipofu.
Tafsiri mkuuIs this the end of the beginning or the beginning of the end? Au yote kwa pamoja?