Asante sana Bernard Kammilius Membe, Una kichwa kikali na ni mzalendo wa kweli

Umeandika vizuri umejitahidi kuelezea kwa uelewa wako picha ilivyo na kujaribu kuwaaminisha wapinzani nguvu ya Membe ambayo kimsingi mimi binafsi siioni.

Labda nikuulize kitu; hivi Membe angebahatika toka mwanzo wa utawala huu kupewa mojawapo ya teuzi za juu unaamini leo hii angekuwa anafanya na kusema hayo ya demokrasia na mengine?

Kwangu mimi namuona Membe kama mtu mwenye hasira na utawala huu uliopo, kama ilivyokuwa kwa Lowassa na JK, Membe amekuwa msema hovyo zaidi kwenye utawala huu baada ya kuona amekuwa ignored, vinginevyo kama angepewa chochote angekuwa kimya anakula maisha.

Kelele zake za demokrasia alitakiwa azipige toka akiwa serikalini ndio ningemuona anajielewa, lakini kuzipiga leo hana maana.
 
Kwanini anaogopwa sasa?
Weka tume huru tuone nani atachukua nchi.
 
Ni vizuri Membe kuondoka chama Tawala ila sio sawa na haitokuwa sawa kupewa nafasi ya kugombania uraisi.
Akili za mwanadamu sio za kuku ambazo baada ya dk mbili tu zinasahau kila kitu. Upinzani umejifunza mengi sana kwa wanaotoka CCM na kuamia upinzani kwa ndoto tu za kupata Madaraka.

CCM haitaondolewa madarakani na mamruki, CCM itaondolewa madarakani na wapinzani wa kweli wanaojua nini maana ya nguvu ya umma.

Membe hawezi kuhamasisha nguvu ya umma kulinda kura, kupinga wizi wa kura na kukataa matokeo ya kura ya Wizi hadi kieleweke. Ni wapinzani halisi tu aina ya Tundu Lissu na wenye itikadi nae sawa wanaoweza kufanya ivo.

Mwaka huu sio wa bahati nasibu ila ni mwaka wa upinzani halisi kupigania haki yao.

Yaliyotokea uchaguzi wa serikali za mitaa ndiyo yanayopangwa kufanywa kwenye uchaguzi mkuu hapo October. Ni people’s power tu ndo itaweza kuondoa huu udharimu wa CCM na si yeyote mwingine zaidi ya TUNDU ANTIPAS LISSU anayeweza kuhamaisha haya.
 
Mkuu Pohamba nadhani membe ni karata nyingine kwa ccm kumsaidia jpm kwa kugawa kura za wapinzani!!!Kwani Lisu akisimama na jpm pekee bila mtu wa tatu tena mbele ya macho ya mabeberu itakuwa tabu kwa ccm!!!Mwache membe aende ACT,LISU CHADEMA NA JPM CCM ILI HESABU ZA KU BALANSI MATOKEO ZIWE RAHISI!!
 
Umenikuna! An excellent analysis.
 

Membe alishaachana na mambo ya teuzi.
Kwa hadhi na heshima ya Membe, teuzi siyo size yake
Uwezo wa Membe, hekima yake, uzoefu wake ni kuwatumikia wananchi kwenye ngazi kubwa zaidi
 
Comments reserved
 
Umelipwa bei gani kabwela mkubwa wewe
 
We jamaa unamini kabisa kuwa humu watu wapo serious?? Humu watu wanapatumia kujifurahisha tu, kupumzikia.
We hushangai kuwa miezi mitatu nyuma hawahawa ndio waliokuwa wanasema membe ni lazima atagombea kupitia ccm na atashinda
 
Aende ACT kutamfaa
Membe sio lazima kuvifuata vyama vya ACT,Chadema au CUF.
Kama atakuja na wimbi la watu wengi maarufu anaweza akatengeneza CCM B.tokana na vyama ambavyo havina mbunge hata mmoja.
 
Hata Lowassa alipokuja huko mlimsifia sana. Tuone na huyu sijui itakuwaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…