Kuna mahojiano aliyafanya ibenge hivi karibuni kuwa mechi hii atotumia nguvu kubwa na angewapumzisha wachezaji wake muhimu kwakuwa tiyali alishafuzu robo fainali!
Alichokiongea ibenge na kilichotokea pale uwanjani ni vitu viwili tofauti,,alipanga full mkoko na walicheza utadhani bado awajafuzu robo fainali,,yanga wangeingia kwenye mtego wa ibenge ilikuwa imekula kwao wangejikuta kwenye hali ngumu sana!
Al hilal walitoa jasho lao lote kuakikisha wanapata point pale na alipoona sasa mambo yamegoma ndio akaanza kuwapumzisha wachezaji wake kuanzia dk ya 70,,
Nawapongeza yanga kwa kuikwepa mind game ya ibenge na mmekipata tulichowatuma kazi iliyobaki ni kumkaanga mwarabu pale kwa mkapa na kutinga robo fainali kibabe!