Uchaguzi 2020 Asante sana Tundu Lissu kwa kutetea Waislamu walioko jela kwa uonevu, Mungu akulipe kheri nyingi sana

Ni bora akachaguliwa mwakilishi wa mabeberu walau tutendelea kuishuhudia demokrasia ila siyo mwakilishi wa BAHIMA EMPIRE, halafu mwaka 2025 tukaishia kutawaliwa kidikteta kama ilivyo Rwanda na Uganda.
marekani kwenyewe hakuna demokrasia sasa sijui unazungumzia demokrasia gani
 
Kama mahakama ya juu imeshaamuru mtu aachiliwe. Mahakama ya chini inaona kigugumizi gani ?!

Je mahakimu hawapo huru kufanya kazi zao ?! Au nini !!

Maelekezo kutoka juu!

Watawala wanaweza kuingilia mahakama ngazi zote, ila mahakimu wa chini wanawamudu zaidi kwa sababu zinaongozwa na mahakimu ambao hawana kinga ya kazi zao!

Kule mahakama za juu zenye majaji huwa wanapenyeza misimamo yao lakini wakati mwingine majaji husimamia haki bila hofu kwa sababu wana kinga za ajira na pia kulinda heshima ya kazi zao kwa sababu hukumu zao husomwa na majaji wengine duniani!
 
Kama JPM ameweza kuwaachia akina babu Seya ambao walikutwa na hatia ya kulawiti na kubaka vitoto,iweje masheikh ambao hakuna ushahidi dhidi yao wanaendelea kusota rumande!!!!?
Waislam mchagueni Lissu akatende haki kwa waumini na viongozi wenzenu!
KWa mujibu wa sheria zetu, rais hana uwezo wa kumuachilia mtu aliyeko rumande, yule aliyefungwa hata maisha, yaani maadamu kahukumiwa na mahakama, rais anayo HAKI ya either kumpunguzia makosa au hata kumuachilia. KWa case ya ma sheikh, rais angeweza kushurutisha vyombo vyake hivyo vinavyo fanya uchunguzi, vifanye haraka ili viongozi wale wa dini wapewe HAKI yao kwa mujibu wa sheria zetu na hapa ndio Tundu anapopaongelea. In fact hata mimi nina amini wale masheikh hawana makosa au kama wanayo makosa basi USHAHIDI serikali HAINA na ndio maana haiwapeleki mahakamani, sawa tu na kina Rugemalulila; tukachague kiongozi anae penda HAKI ili AMANI idumu
 
 
Ubaguzi wa kidini unaousema kwanza haupo huku bara bali upo Zanzibar. Pili nionyeshe mgombea ubunge au uwakilishi huko Zanzibar ambaye ni mkristo. Je Zanzibar hakuna wakristo hata kama wachache?
Hao masheikh, Lissu anaowatumia kama chambo ili kupata kura za waislamu hawana tuhuma za makosa ya jinai? Kumbuka kule zanzibar padre amewahi kuuawa mlangoni kanisani, watalii kumwagiwa tindikali yote hiyo kutokana na mahubiri ya chuki katika nyumba za ibada, kanda zilizorekodiwa.

Huku bara kuna wakati makanisa yalichomwa, mengine mipango ya kuyashambulia iliwahiwa ndio ikawa salama. Ugaidi wa Kibiti yeye Lissu aliufurahia.

Serikali yeyote makini haiwezi kukaa kimya wakati kuna watu wanapanga na kutekeleza ugaidi ndani ya nchi. Lissu anaweza kuwa na uchungu na waislamu kuliko waislamu wenyewe ea Zanzibar walioamua kuwachukulia hatua baada ya kuona vitendo vyao vya kigaidi vimezidi licha ya kuonywa mara kadhaa? Hivi yaliyokuwa yakiendelea kule Zanzibar na Kibiti wakati ule kabla hawajawekwa ndani yeye Lissu alikuwa hayaoni au ndio cheap politics?

Kama kuna mtu anataka nafasi za uteuzi ziwe nusu kwa nusu baina ya ukristo na uislamu basi kwanza aanzie Zanzibar kabla hajazungumzia bara .
 
Ni bora akachaguliwa mwakilishi wa mabeberu walau tutendelea kuishuhudia demokrasia ila siyo mwakilishi wa BAHIMA EMPIRE, halafu mwaka 2025 tukaishia kutawaliwa kidikteta kama ilivyo Rwanda na Uganda.
Saudi Arabia demokrasia hakuna ila ana urafiki mzuri tu na hao mabeberu(wapenda demokrasia).
 
Ila usisahau hao Masheikh walishikiliwa tangu enzi za Kikwete! Hivyo ni vyema na yeye akatajwa kuhusika kwa namna fulani kama Rais wa wakati huo.
Mbona babu Seya alishikiliwa tangu enzi za Kikwete ameachiwa na Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…