Innocent Kirumbuyo
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 4,641
- 4,457
Kumbuka lisu kasema ni serikali ya ccm ndio inawatesa hao mashehe siyo magufuli au kikweteIla usisahau hao Masheikh walishikiliwa tangu enzi za Kikwete! Hivyo ni vyema na yeye akatajwa kuhusika kwa namna fulani kama Rais wa wakati huo.
Kumbe wewe ni muthilamu....?! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Porojo hizo hazina nafasi,waislam tutamchagua Lissu!
Ukitaka kujua kuwa hao jamaa hawakuonewa angalia tu walikamatwa administration ikiwa ipi, moja.Ngoja kwanza awe Rais. Hayo mambo mengine yatajulikana mbele ya safari. Hivyo hakikisha unampa kura yako hata kama hatokani na chama chako.
Mkuu nilikuwa nachunga kauli zangu tu ila wale jamaa ni magaidi , hakuna masihara pale, Lisu anataka kuleta masihara katika mambo ya msingi kama kawaida yake.Hiyo tundulissu anaongea tu. Swala la wale wahuni wanaojiita masheikh si swala la kisiasa kusema wataamua tu watolewe as if ni watu wasio na shida.
Lile ni swala la kiusalama. Jamaa walikuwa wanachanganya maswala ya dini za itikadi kali yaani radicalism zenye elements za fujo za ugaidi ndani yake na kuingiza kwenye shughuli za kisiasa. Huo ni upuuzi ambao hautakiwi kuchekewa maana ukiachiwa una madhara makubwa sana.
Ni vema wamewekwa ndani na kupewa adhabu ya kudhibitiwa.....
Watampigia kura mwakilishi wa shetani duniani maana hata Misikiti anawajengea na wanapokwenda kuhiji madege yasiyo na kazi yatapata kazi ya kuwasafirisha bure. Shetani ampe maisha marefu ajenge Misikiti nchi nzima!Waislamu hawawezi kupigia kura mwakilishi wa Wazungu Tanzania
Watampigia kura mwakilishi wa shetani duniani maana hata Misikiti anawajengea na wanapokwenda kuhiji madege yasiyo na kazi yatapata kazi ya kuwasafirisha bure. Shetani ampe maisha marefu ajenge Misikiti nchi nzima!
Gonga mboga mzee, jamaa aliwakataza kwa masirahi yakeTatizo nyie hamuaminiki
Mkuu nilikuwa nachunga kauli zangu tu ila wale jamaa ni magaidi , hakuna masihara pale, Lisu anataka kuleta masihara katika mambo ya msingi kama kawaida yake.
Hakuna shaka wale masheikh walikua wanaandaa mazingira ya uasi zanzibar, kupitia hile miadhara yao na cd zilizokua zinasambzwa kuwajengea chuki wazanzibar dhidi ya muuangano maandamano waliyokua wanafanya na kama yangetokea machafuko watu wangekufa, wache tuu wakae jela. Kuna kasoro katika muungano wetu hila hile haikua njia sahihi ya kuyatatuaWangekuwa ni magaidi ushahidi ungekuwa umeshatolewa na hao watu kuhukumiwa lakini kila siku ushahidi haujakamilika, haujakamilika vipi kwa miaa sita?
Siku hizi ukiwa Sheikh na ukaipinga Bakwata unawekwa ndani
Huoni kuwa huo ni uonevu?
Wale masheikh wa Zanzibar kosa lao ni kuhoji aina ya muungano tulionao hilo ndo kosa lao, habari za Ugaidi ni za kutunga
Kwako Ndugu Lissu
Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nawe
Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa dhati ya moyo wangu kwa kitendo chako cha Utu na kupenda haki kwako kwa namna unavyotetea Viongozi wa dini ya Kiislamu walioko Jela kiuonevu.
Umekuwa consistent sana kuhusu uonevu huu, umezungumzia kuhusu Masheikh zaidi ya 70 huko Arusha walioko jela, si kwa sababu wana makosa bali eti wanaipinga BAKWATA ambayo umma umeshatambua kuwa siyo chombo chenye kulinda au kutetea maslahi ya waislamu, bali ni mkono wa system kwa ajili ya kuwathibiti waislamu, Hao viongozi wa BAKWATA wakipewa maslahi machache machache ya hapa na pale kutoka serikali ya CCM basi hufanya bidding kwa ajili ya manufaa ya serikali hiyo, hawana mpango kabisa na mustakbali mkubwa wa Waislamu wenzao nchini! .
Lakini pia umezungumzia Masheikh wa Zanzibar ambao kwa uonevu mkubwa, na ukatili mkubwa kutoka kwa serikali ya CCM na viongozi wake wameendelea kusota magerezani kwa miaka zaidi ya Sita sasa bila kuwepo kwa ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani, na pia wakiwa wametekwa kutoka Zanzibar walipokuwepo na kwenye sheria zenye kutoa dhamana kwa makosa waliyoshitaiwa nayo na kisha kuletwa huku bara kwenye sheria ambayo haitoi dhamana kwa makosa yale ili kuwatesa na kuwaumiza.
Tatu umezungumzia kuhusu Masheikh walioko huko mikoa ya kusini, huko Mtwara ambao nao wako ndani kiuonevu.
Kwa hiyo inavyoonekana serikali ya CCM inatesa Watu wa Mungu, kama haiwatesi kwa nini Inaweka Masheikh wake Jela bila haki?. Je serikali hii ya kidhalimu ina utofauti gani na serikali tunazozisoma kwenye maandiko matakatifu ziliziokuwa zinaonea na kutesa watu wa Mungu?
Ndugu Lissu, Unafanya kazi kubwa sana na nzuri kutetea waislamu nchini. Nakufananisha na Mfalme mmoja wa nchi ya Ethiopia aitwaye Najashi(King Negus kwa kiingereza) aliyekuwepo kipindi Mtume Muhammad alipoanza mafundisho yake huko Arabia, Wanafunzi wa mtume walikuwa wakionewa na serikali katili za Wapagani pale Makka, Mtume akawaagiza wanafunzi wake wakimbilie Ethiopia kwa yule Mfalme ili kujinusuru,mtume akawaambia kuwa waende ethiopia huko kuna mfalme, tena ni mkristo na ni muadilifu na atawatendeeni wema. Na kweli yule mfalme aliwapokea vizuri na kuwatendea wema sana, aligoma hata kuwarudisha Makka pindi ile serikali dhalimu ya Arabia ilipotuma ujumbe kwa huyo mfalme wa Ethiopia ili wale watu warudishwe huko Arabia wakateswe! .
Sasa wewe ndugu Lissu unafanya kazi kama ya mfalme Najashi, unawatetea hawa waislamu wanaonyanyasika katika serikali hii ya CCM.
Nakuomba ndugu Lissu uendelee na moyo huohuo, umeonyesha jinsi ulivyo binadamu, mwenye utu kwelikweli. Tofauti yako na watawala wa CCM ni kubwa sana ni kwamba wewe ni Mtu, wao ni makatili, wewe ni mpenda haki wao ni madhulumati, wewe ni hero wao ni cowards.
Mwisho kabisa, ningependa kukujulisha kuwa waislamu wanakerwa na teuzi za serikali ya awamu hii zinazonuka udini, Nakuomba hili suala ulisemee, ulizungumzie bila woga kwa sababu haiwezekani katika nchi hii kufanya teuzi zinazoonekana waziwazi kuwa zina mrengo wa kidini halafu nchi ikakaa kimya. Hii siyo dhana yangu, bali Masheikh wameshalalamika kuhusu hili, Sheikh Halifa amelisemea hili jambo, Sheikh Ponda na Shura ya maimamu wamelisemea hili jambo. Serikali ya Magufuli haijajibu hoja hii zaidi ya kuwatisha Masheikh hao. Nakuomba ndugu Lissu, mteta haki, msema kweli, na shujaa asiyeogopa madhalimu. Simama na ulizungumzie hili.
La Mwisho nakuomba ukiwa rais, uondoe ubaguzi huu wa Udini, utengeneze serikali shirikishi(inclusive) ambayo itawapa nafasi watu kwa fairness kabisa badala ya kuangalia dini zao au majina yao kama yanasound kizungu au Kiarabu
FREEDOM, JUSTICE AND PEOPLE CENTRED DEVELOPMENT.
Masheikh wamemuuwa nani?Wanasheria hutetea hata wauaji
Ninacho kijuwa ni kwanini Waislamu wapo jela jibu ni kwa sababu mfumo wa Dini ya Kiislamu upo huru kuliko Dini nyingine kwa sababu sheria za Kiislamu hazina mkubwa wala mdogo hivyo ni rahisi sana ubongo wa Waislamu kujitambua udhalimu na kutambua haki!!Wanasheria hutetea hata wauaji
Mnafikiri udini utawasaidiaPorojo hizo hazina nafasi,waislam tutamchagua Lissu!
Yeye so ndo yupo madarakani kwa sasa?Ila usisahau hao Masheikh walishikiliwa tangu enzi za Kikwete! Hivyo ni vyema na yeye akatajwa kuhusika kwa namna fulani kama Rais wa wakati huo.
Kwa kipindi cha miaka mitano hakukuwahi kutokea mtu yeyote kuzungumzia dhahama ya hao watumishi wa Mungu. Lazima ungelala segerea tu. Tunamhitaji mtu kama Tundu Lissu tu.Kwako Ndugu Lissu
Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nawe
Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa dhati ya moyo wangu kwa kitendo chako cha Utu na kupenda haki kwako kwa namna unavyotetea Viongozi wa dini ya Kiislamu walioko Jela kiuonevu.
Umekuwa consistent sana kuhusu uonevu huu, umezungumzia kuhusu Masheikh zaidi ya 70 huko Arusha walioko jela, si kwa sababu wana makosa bali eti wanaipinga BAKWATA ambayo umma umeshatambua kuwa siyo chombo chenye kulinda au kutetea maslahi ya waislamu, bali ni mkono wa system kwa ajili ya kuwathibiti waislamu, Hao viongozi wa BAKWATA wakipewa maslahi machache machache ya hapa na pale kutoka serikali ya CCM basi hufanya bidding kwa ajili ya manufaa ya serikali hiyo, hawana mpango kabisa na mustakbali mkubwa wa Waislamu wenzao nchini! .
Lakini pia umezungumzia Masheikh wa Zanzibar ambao kwa uonevu mkubwa, na ukatili mkubwa kutoka kwa serikali ya CCM na viongozi wake wameendelea kusota magerezani kwa miaka zaidi ya Sita sasa bila kuwepo kwa ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani, na pia wakiwa wametekwa kutoka Zanzibar walipokuwepo na kwenye sheria zenye kutoa dhamana kwa makosa waliyoshitaiwa nayo na kisha kuletwa huku bara kwenye sheria ambayo haitoi dhamana kwa makosa yale ili kuwatesa na kuwaumiza.
Tatu umezungumzia kuhusu Masheikh walioko huko mikoa ya kusini, huko Mtwara ambao nao wako ndani kiuonevu.
Kwa hiyo inavyoonekana serikali ya CCM inatesa Watu wa Mungu, kama haiwatesi kwa nini Inaweka Masheikh wake Jela bila haki?. Je serikali hii ya kidhalimu ina utofauti gani na serikali tunazozisoma kwenye maandiko matakatifu ziliziokuwa zinaonea na kutesa watu wa Mungu?
Ndugu Lissu, Unafanya kazi kubwa sana na nzuri kutetea waislamu nchini. Nakufananisha na Mfalme mmoja wa nchi ya Ethiopia aitwaye Najashi(King Negus kwa kiingereza) aliyekuwepo kipindi Mtume Muhammad alipoanza mafundisho yake huko Arabia, Wanafunzi wa mtume walikuwa wakionewa na serikali katili za Wapagani pale Makka, Mtume akawaagiza wanafunzi wake wakimbilie Ethiopia kwa yule Mfalme ili kujinusuru,mtume akawaambia kuwa waende ethiopia huko kuna mfalme, tena ni mkristo na ni muadilifu na atawatendeeni wema. Na kweli yule mfalme aliwapokea vizuri na kuwatendea wema sana, aligoma hata kuwarudisha Makka pindi ile serikali dhalimu ya Arabia ilipotuma ujumbe kwa huyo mfalme wa Ethiopia ili wale watu warudishwe huko Arabia wakateswe! .
Sasa wewe ndugu Lissu unafanya kazi kama ya mfalme Najashi, unawatetea hawa waislamu wanaonyanyasika katika serikali hii ya CCM.
Nakuomba ndugu Lissu uendelee na moyo huohuo, umeonyesha jinsi ulivyo binadamu, mwenye utu kwelikweli. Tofauti yako na watawala wa CCM ni kubwa sana ni kwamba wewe ni Mtu, wao ni makatili, wewe ni mpenda haki wao ni madhulumati, wewe ni hero wao ni cowards.
Mwisho kabisa, ningependa kukujulisha kuwa waislamu wanakerwa na teuzi za serikali ya awamu hii zinazonuka udini, Nakuomba hili suala ulisemee, ulizungumzie bila woga kwa sababu haiwezekani katika nchi hii kufanya teuzi zinazoonekana waziwazi kuwa zina mrengo wa kidini halafu nchi ikakaa kimya. Hii siyo dhana yangu, bali Masheikh wameshalalamika kuhusu hili, Sheikh Halifa amelisemea hili jambo, Sheikh Ponda na Shura ya maimamu wamelisemea hili jambo. Serikali ya Magufuli haijajibu hoja hii zaidi ya kuwatisha Masheikh hao. Nakuomba ndugu Lissu, mteta haki, msema kweli, na shujaa asiyeogopa madhalimu. Simama na ulizungumzie hili.
La Mwisho nakuomba ukiwa rais, uondoe ubaguzi huu wa Udini, utengeneze serikali shirikishi(inclusive) ambayo itawapa nafasi watu kwa fairness kabisa badala ya kuangalia dini zao au majina yao kama yanasound kizungu au Kiarabu
FREEDOM, JUSTICE AND PEOPLE CENTRED DEVELOPMENT.
View attachment 1567784