Uchaguzi 2020 Asante sana Tundu Lissu kwa kutetea Waislamu walioko jela kwa uonevu, Mungu akulipe kheri nyingi sana

Ila usisahau hao Masheikh walishikiliwa tangu enzi za Kikwete! Hivyo ni vyema na yeye akatajwa kuhusika kwa namna fulani kama Rais wa wakati huo.
Babu Seya na mwanawe nao walishikiliwa tokea kipindi gani? Wako wapi saa hizi??
 
Kiboko ya yote hiyo ni Lissu, anaenda kufumulia mbali na kusuka upya, kuanzia katiba mpya mpaka kufutilia mbali masheria kandamizi yote yaliyopitishwa kwa mwendo kasi na wale wapiga meza mjengoni.
 
Mkuu nilikuwa nachunga kauli zangu tu ila wale jamaa ni magaidi , hakuna masihara pale, Lisu anataka kuleta masihara katika mambo ya msingi kama kawaida yake.
Tukikumbuka maneno ya mwanafalsafa mahiri na baba wa taifa, mwalimu Julius Kambarage nyerere, alishasema bayana kuwa mtu au kiongozi yoyote aliyefilisika sera na ambaye anajitambua kuwa amekosa uhalali katika jamii aliyopo basi atatafuta hoja au ajenda yoyote ambayo ataweza kuitumia ili apate uhalali wa kutambulika katika hiyo jamii.

Kuna ambao watatumia dini kama ndio ajenda yao, kwakusema dini fulani inapendelewa na nyingine inaonewa ili wakijinasibu kuwa wao watakuwa wakombozi.

Wapo watakao tumia jinsia kusema jinsia fulani inahitaji ukombozi kutoka jinsia fulani, wapo watakaosema tabaka fulani la watu sijui kabila..... Yote hiyo ni kufilisika sera.

Mtu mwenye nia nzuri huwa anasema atakachofanya..... Atanyoosha maelezo...
 
Unajua kuna watu huwa wanawekwa kizuizini kwasababu wao hukaa kwenye nafasi ya uchochezi na kufanya vitu kimya kimya. Hao watu wakishabainika huwa wanapewa onyo ama kutiwa kizuizini.

Mfano ni yule mzee alipigwa ban na nyerere hadi juzi anafariki. Alipigwa ban kuwa asivuke kigamboni hapo wala kwenda zanzibar. Akija mjini ni kwasababu za msingi kama kujiuguza...
 
Unajua unaweza kudai haki huku ukiheshimu ustawi wa jamii na kuna kudai haki ukiharibu ustawi wa jamii husika.....

Hawa walikuwa wanadai haki wanazozijua wao binafsi.....
 
Mtu kama huyu anaweza hata kuiuza nchi kwa wachina sababu anatamia za umalaya wa kidiplomasia....

Kesho na kesho kutwa amepewa nchi, ataenda kutukabidhisha kwa wamarekani, wakishamtumia wakamchoka ataanza kukinzana nao mwisho wasiku unasikia kahamia kwa wachina huko ndipo anatuuza kabisa..... Wachina watakuja hadi kuwa machinga Dar.
 
Umeongea kwa muktadha wa dini wakati huu mjadala ni wa kijamii na kisiasa...
 
Muuaji si anahukumiwa aidha kifo au kifungo cha maisha?? Anawekwa tuu mahabusu miaka dahari?
Hawa wapo kizuizini..... Ndio ile ukisikia mtu anakwambia nitakupoteza ndio hiyo sasa..... Unawekwa ndani miaka.
 
Jamani ebu tuweke record vizuri, hao masheikh, walikamatwa enzi za Kikwete, na sio Rais Magufuli jamani, mm napenda tuwe wakweli, Mh. Magufuli hakukamata Sheikh hata mmoja, ulizeni vizuri, hili halimuhusu Mh. Magufuli kabisa
 
Jamani ebu tuweke record vizuri, hao masheikh, walikamatwa enzi za Kikwete, na sio Rais Magufuli jamani, mm napenda tuwe wakweli, Mh. Magufuli hakukamata Sheikh hata mmoja, ulizeni vizuri, hili halimuhusu Mh. Magufuli kabisa
acha kupiga propaganda kwenye suala linalohusu haki na maisha ya watu wewe; mashekhe walikamatwa na kikwte au na serikali ya ccm? na huyo magufuli anaongoza serikali inayoundwa na chama gan kama siyo hayo hayo makijani?

ma ccm achen kukandamiza watanzania.
 
We ulishaona gaidi anahukumiwa tanzania, hao watavutwa vutwa mpaka waishe mmoja mmoja, hizo nenda rudi ni wengine kama waone kama wakijaribu nini kitawakuta, hila kuachiwa sahau. Hata aiingie nani madarakani hawatoachiwa huru. Hakuna siasa kwenye national security.
 
ni mahakama ipi imedhibitisha wao ni magaidi? au ni mtu mmoja tu kaamua kumpa mbwa jina baya ili auwawe? hata mandela kuna serikali ilimuita gaidi. na kama ni suala tu la mtu kuamua huyu ni gaidi na huyu si gaidi pasipo mahakama kuthibitisha basi hata wewe unaweza kuitwa gaidi muda wowote na ukafungwa au kuuwawa kama mbwa tu na hakuna atakayehoji. kataa dhulumati na ubaya hata kama anayetendewa ubaya ni mtu hukubaliani naye kiitikadi..usisubiri mpaka yakufike wewe mana hutakuwa na wa kutetea. binadam haachi kuwa binadamu kwa kuwa tu umetofautiana naye itikadi au mawazo na tena kutofautiana kimitizamo ni jambo la kawaida sana kibinadam..kikubwa ni hoja yenye nguvu. mtu kuhoji Muungano anakuwa gaidi kivip?
 
Hacha kuongea kwa hisia, tafuta video youtube za hizo harakati za "uhamsho" sikiliza kwa umakini halafu wewe mwenyewe tafakari, lengo la hile movement ilikua ni nn, au ilikuja kwa malengo gani, unapojaribu kupambana na serikali iliyopo madarakani kihalali kwa maandamo, kusambaza speech recorded za chuki kwa wananchi kwa serikali yao, kutumia majukwaa ya dini kuingiza kuhubiri siasa za chuki ni uhaini au ugaidi tu kwa sheria zetu.
 
wewe ndiye unayesema walihubiri ugaidi, embu thibitisha tuwekee hiyo video.

vinginevyo tambua serikali yoyote iliyopo duniani ni ya wanadamu tu na si malaika hivyo kukosolewa na hata kupingwa ni lazima. na ukizuia kimabavu kupingwa na kukosolewa kwa njia za halali zilizopo kisheria basi utapingwa hata kwa njia zisizo za kisheria na hiyo ni duniani kote ndivyo ilivyo. hata chauma cuf au chadema wakiingia madarakani leo watakosolewa/watapingwa vilevile na hiyo si dhambi; kubwa ni hoja na ni katika kupingana na kukosoana ndiko maendeleo ya kweli yanakotokea. ccm ilipingwa/ilikosolewa jana, itakosolewa leo na itakosolewa kesho; almradi ipo haijafutika juu ya uso wa Tanzania itakosolewa tu hata kama haipo madarakani..acheni mawazo finyu ya kuwaita wakosoaji wenu magaidi mara vibaraka wa mabeberu; hizo ni siasa muflisi na haziwapi credit yoyote zaidi ya kuwashusha tu. huo muungano kama haukubaliki kwa sehemu moja ya nchi utaendelea kupingwa tu daima dumu. ingekuwa kufunga watu, kuwaua au kuwatesa kunawarudisha watu nyuma basi Afrika kusini ingekuwa bado chini ya makaburu na watu weusi marekani leo wangekuwa hata kufutwa juu ya uso wa marekan wameshafutwa. huwez kuzuia haki kwa njia haramu daima; sana sana utaichelewesha tu kwa muda flani lakin mwisho haki itafika tu hata kama ni kwa kuchelewa.
 
Mwanzo kama ukitaka kuongea kitu Fulani cha kufikirisha but nilivyoendelea mbele nikaona rangi yako..
 
Mheshimiwa Tundu Lisu Mungu akupe afya njema. kura zote za familia yangu 45 nimeshakuhakikishia utazipta zote. tutakupa kura zote kwa sababu kuu tatu. moja unatetea kuachiwa kwa masheikh wetu wa UAMSHO. mbili unajiamini na hiyo ndo hulka ya mwanammne. tatu. you call a spade, a spade sio jembe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…