Uchaguzi 2020 Asante sana Tundu Lissu kwa kutetea Waislamu walioko jela kwa uonevu, Mungu akulipe kheri nyingi sana

Uchaguzi 2020 Asante sana Tundu Lissu kwa kutetea Waislamu walioko jela kwa uonevu, Mungu akulipe kheri nyingi sana

Ila usisahau hao Masheikh walishikiliwa tangu enzi za Kikwete! Hivyo ni vyema na yeye akatajwa kuhusika kwa namna fulani kama Rais wa wakati huo.
Babu Seya na mwanawe nao walishikiliwa tokea kipindi gani? Wako wapi saa hizi??
 
Mfumo tu sheria na mahakama zetu si huru. Majuzi tu mahakama kuu Dodoma waliamuru vijana wa Bavicha T (Nusrat Hanje na wenzie) waachiliwe kwa dhamana.

Lakini walipo rudishwa mahakama za chini kwa taratibu za dhamana imekuwa danadana.

Mifumo yetu ya sheria inaangalia utashi wa nani aliye hapo juu

Nafananisha na hili la ma sheikh
Kiboko ya yote hiyo ni Lissu, anaenda kufumulia mbali na kusuka upya, kuanzia katiba mpya mpaka kufutilia mbali masheria kandamizi yote yaliyopitishwa kwa mwendo kasi na wale wapiga meza mjengoni.
 
Mkuu nilikuwa nachunga kauli zangu tu ila wale jamaa ni magaidi , hakuna masihara pale, Lisu anataka kuleta masihara katika mambo ya msingi kama kawaida yake.
Tukikumbuka maneno ya mwanafalsafa mahiri na baba wa taifa, mwalimu Julius Kambarage nyerere, alishasema bayana kuwa mtu au kiongozi yoyote aliyefilisika sera na ambaye anajitambua kuwa amekosa uhalali katika jamii aliyopo basi atatafuta hoja au ajenda yoyote ambayo ataweza kuitumia ili apate uhalali wa kutambulika katika hiyo jamii.

Kuna ambao watatumia dini kama ndio ajenda yao, kwakusema dini fulani inapendelewa na nyingine inaonewa ili wakijinasibu kuwa wao watakuwa wakombozi.

Wapo watakao tumia jinsia kusema jinsia fulani inahitaji ukombozi kutoka jinsia fulani, wapo watakaosema tabaka fulani la watu sijui kabila..... Yote hiyo ni kufilisika sera.

Mtu mwenye nia nzuri huwa anasema atakachofanya..... Atanyoosha maelezo...
 
Wangekuwa ni magaidi ushahidi ungekuwa umeshatolewa na hao watu kuhukumiwa lakini kila siku ushahidi haujakamilika, haujakamilika vipi kwa miaa sita?

Siku hizi ukiwa Sheikh na ukaipinga Bakwata unawekwa ndani

Huoni kuwa huo ni uonevu?

Wale masheikh wa Zanzibar kosa lao ni kuhoji aina ya muungano tulionao hilo ndo kosa lao, habari za Ugaidi ni za kutunga
Unajua kuna watu huwa wanawekwa kizuizini kwasababu wao hukaa kwenye nafasi ya uchochezi na kufanya vitu kimya kimya. Hao watu wakishabainika huwa wanapewa onyo ama kutiwa kizuizini.

Mfano ni yule mzee alipigwa ban na nyerere hadi juzi anafariki. Alipigwa ban kuwa asivuke kigamboni hapo wala kwenda zanzibar. Akija mjini ni kwasababu za msingi kama kujiuguza...
 
Hakuna shaka wale masheikh walikua wanaandaa mazingira ya uasi zanzibar, kupitia hile miadhara yao na cd zilizokua zinasambzwa kuwajengea chuki wazanzibar dhidi ya muuangano maandamano waliyokua wanafanya na kama yangetokea machafuko watu wangekufa, wache tuu wakae jela. Kuna kasoro katika muungano wetu hila hile haikua njia sahihi ya kuyatatua
Unajua unaweza kudai haki huku ukiheshimu ustawi wa jamii na kuna kudai haki ukiharibu ustawi wa jamii husika.....

Hawa walikuwa wanadai haki wanazozijua wao binafsi.....
 
lissu anataka kuwaudhi waliomtuma
kama hao mashekhe wangeonewa ubalozi wa Us na Uk wasingekaa kimya
Toka hao mashekhe wawekwe ndani,zanzibar mapdri hawauawi,wakristo hawachomewi nyumba
lissu ni mtu hatari sana,yupo tayari kufanya lolote ili apewe kura
Mtu kama huyu anaweza hata kuiuza nchi kwa wachina sababu anatamia za umalaya wa kidiplomasia....

Kesho na kesho kutwa amepewa nchi, ataenda kutukabidhisha kwa wamarekani, wakishamtumia wakamchoka ataanza kukinzana nao mwisho wasiku unasikia kahamia kwa wachina huko ndipo anatuuza kabisa..... Wachina watakuja hadi kuwa machinga Dar.
 
Ninacho kijuwa ni kwanini Waislamu wapo jela jibu ni kwa sababu mfumo wa Dini ya Kiislamu upo huru kuliko Dini nyingine kwa sababu sheria za Kiislamu hazina mkubwa wala mdogo hivyo ni rahisi sana ubongo wa Waislamu kujitambua udhalimu na kutambua haki!!
Na kuongea kwa uwazi kwa kufahamu kuwa kusema uwongo ni dhambi na dhambi iliyo kubwa!
Hao mashekhe hawataweza kuachiwa huru labda kama CCM inahitaji kufika ukomo!!
Hao mashekhe ukiwaachia leo wata kuambia tume dhulumiwa haki yetu ila Mungu ata tulipa sio rahisi waombe msamaha kama hawana makosa maana kuomba msamaha kwa jambo la uwongo ni kukufuru ! Maisha ya Duniani ni mafupi kuliko ya Akhera hivyo sio rahisi hao mashekhe ku mwangukia shetani na kumuomba msamaha!!
Kwa imani yao watabaki ndani adi watakapo pata haki yao iwe apa Duniani ama Akhera lakini sio kwa kumtaka radhi Sheitwan
Umeongea kwa muktadha wa dini wakati huu mjadala ni wa kijamii na kisiasa...
 
Muuaji si anahukumiwa aidha kifo au kifungo cha maisha?? Anawekwa tuu mahabusu miaka dahari?
Hawa wapo kizuizini..... Ndio ile ukisikia mtu anakwambia nitakupoteza ndio hiyo sasa..... Unawekwa ndani miaka.
 
Waislamu hawawezi kupigia kura mwakilishi wa Wazungu Tanzania
kichwa yako ipo hivi
IMG_20200822_093254.jpg
 
Jamani ebu tuweke record vizuri, hao masheikh, walikamatwa enzi za Kikwete, na sio Rais Magufuli jamani, mm napenda tuwe wakweli, Mh. Magufuli hakukamata Sheikh hata mmoja, ulizeni vizuri, hili halimuhusu Mh. Magufuli kabisa
 
Jamani ebu tuweke record vizuri, hao masheikh, walikamatwa enzi za Kikwete, na sio Rais Magufuli jamani, mm napenda tuwe wakweli, Mh. Magufuli hakukamata Sheikh hata mmoja, ulizeni vizuri, hili halimuhusu Mh. Magufuli kabisa
acha kupiga propaganda kwenye suala linalohusu haki na maisha ya watu wewe; mashekhe walikamatwa na kikwte au na serikali ya ccm? na huyo magufuli anaongoza serikali inayoundwa na chama gan kama siyo hayo hayo makijani?

ma ccm achen kukandamiza watanzania.
 
acha kupiga propaganda kwenye suala linalohusu haki na maisha ya watu wewe; mashekhe walikamatwa na kikwte au na serikali ya ccm? na huyo magufuli anaongoza serikali inayoundwa na chama gan kama siyo hayo hayo makijani?

ma ccm achen kukandamiza watanzania.
We ulishaona gaidi anahukumiwa tanzania, hao watavutwa vutwa mpaka waishe mmoja mmoja, hizo nenda rudi ni wengine kama waone kama wakijaribu nini kitawakuta, hila kuachiwa sahau. Hata aiingie nani madarakani hawatoachiwa huru. Hakuna siasa kwenye national security.
 
We ulishaona gaidi anahukumiwa tanzania, hao watavutwa vutwa mpaka waishe mmoja mmoja, hizo nenda rudi ni wengine kama waone kama wakijaribu nini kitawakuta, hila kuachiwa sahau. Hata aiingie nani madarakani hawatoachiwa huru. Hakuna siasa kwenye national security.
ni mahakama ipi imedhibitisha wao ni magaidi? au ni mtu mmoja tu kaamua kumpa mbwa jina baya ili auwawe? hata mandela kuna serikali ilimuita gaidi. na kama ni suala tu la mtu kuamua huyu ni gaidi na huyu si gaidi pasipo mahakama kuthibitisha basi hata wewe unaweza kuitwa gaidi muda wowote na ukafungwa au kuuwawa kama mbwa tu na hakuna atakayehoji. kataa dhulumati na ubaya hata kama anayetendewa ubaya ni mtu hukubaliani naye kiitikadi..usisubiri mpaka yakufike wewe mana hutakuwa na wa kutetea. binadam haachi kuwa binadamu kwa kuwa tu umetofautiana naye itikadi au mawazo na tena kutofautiana kimitizamo ni jambo la kawaida sana kibinadam..kikubwa ni hoja yenye nguvu. mtu kuhoji Muungano anakuwa gaidi kivip?
 
ni mahakama ipi imedhibitisha wao ni magaidi? au ni mtu mmoja tu kaamua kumpa mbwa jina baya ili auwawe? hata mandela kuna serikali ilimuita gaidi. na kama ni suala tu la mtu kuamua huyu ni gaidi na huyu si gaidi pasipo mahakama kuthibitisha basi hata wewe unaweza kuitwa gaidi muda wowote na ukafungwa au kuuwawa kama mbwa tu na hakuna atakayehoji. kataa dhulumati na ubaya hata kama anayetendewa ubaya ni mtu hukubaliani naye kiitikadi..usisubiri mpaka yakufike wewe mana hutakuwa na wa kutetea. binadam haachi kuwa binadamu kwa kuwa tu umetofautiana naye itikadi au mawazo na tena kutofautiana kimitizamo ni jambo la kawaida sana kibinadam..kikubwa ni hoja yenye nguvu. mtu kuhoji Muungano anakuwa gaidi kivip?
Hacha kuongea kwa hisia, tafuta video youtube za hizo harakati za "uhamsho" sikiliza kwa umakini halafu wewe mwenyewe tafakari, lengo la hile movement ilikua ni nn, au ilikuja kwa malengo gani, unapojaribu kupambana na serikali iliyopo madarakani kihalali kwa maandamo, kusambaza speech recorded za chuki kwa wananchi kwa serikali yao, kutumia majukwaa ya dini kuingiza kuhubiri siasa za chuki ni uhaini au ugaidi tu kwa sheria zetu.
 
Hacha kuongea kwa hisia, tafuta video youtube za hizo harakati za "uhamsho" sikiliza kwa umakini halafu wewe mwenyewe tafakari, lengo la hile movement ilikua ni nn, au ilikuja kwa malengo gani, unapojaribu kupambana na serikali iliyopo madarakani kihalali kwa maandamo, kusambaza speech recorded za chuki kwa wananchi kwa serikali yao, kutumia majukwaa ya dini kuingiza kuhubiri siasa za chuki ni uhaini au ugaidi tu kwa sheria zetu.
wewe ndiye unayesema walihubiri ugaidi, embu thibitisha tuwekee hiyo video.

vinginevyo tambua serikali yoyote iliyopo duniani ni ya wanadamu tu na si malaika hivyo kukosolewa na hata kupingwa ni lazima. na ukizuia kimabavu kupingwa na kukosolewa kwa njia za halali zilizopo kisheria basi utapingwa hata kwa njia zisizo za kisheria na hiyo ni duniani kote ndivyo ilivyo. hata chauma cuf au chadema wakiingia madarakani leo watakosolewa/watapingwa vilevile na hiyo si dhambi; kubwa ni hoja na ni katika kupingana na kukosoana ndiko maendeleo ya kweli yanakotokea. ccm ilipingwa/ilikosolewa jana, itakosolewa leo na itakosolewa kesho; almradi ipo haijafutika juu ya uso wa Tanzania itakosolewa tu hata kama haipo madarakani..acheni mawazo finyu ya kuwaita wakosoaji wenu magaidi mara vibaraka wa mabeberu; hizo ni siasa muflisi na haziwapi credit yoyote zaidi ya kuwashusha tu. huo muungano kama haukubaliki kwa sehemu moja ya nchi utaendelea kupingwa tu daima dumu. ingekuwa kufunga watu, kuwaua au kuwatesa kunawarudisha watu nyuma basi Afrika kusini ingekuwa bado chini ya makaburu na watu weusi marekani leo wangekuwa hata kufutwa juu ya uso wa marekan wameshafutwa. huwez kuzuia haki kwa njia haramu daima; sana sana utaichelewesha tu kwa muda flani lakin mwisho haki itafika tu hata kama ni kwa kuchelewa.
 
Ukitaka kujua kuwa hao jamaa hawakuonewa angalia tu walikamatwa administration ikiwa ipi, moja.

Mbili, je vile vitendo vinaendelea sasa.

Swala la kumpa kura Lisu hilo ni nje ya uhalisia , hana qualities kwa nafasi ya Urais, anafaa kuendela kuwa mwanaharakati na ndio maana akasomea sheria, aendelee tu ila kuongoza nchi hawezi.

Chama chake pia hakina dira, hakijawa tayari kushika dola.
Mwanzo kama ukitaka kuongea kitu Fulani cha kufikirisha but nilivyoendelea mbele nikaona rangi yako..
 
Kwako Ndugu Lissu

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nawe
Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa dhati ya moyo wangu kwa kitendo chako cha Utu na kupenda haki kwako kwa namna unavyotetea Viongozi wa dini ya Kiislamu walioko Jela kiuonevu.

Umekuwa consistent sana kuhusu uonevu huu, umezungumzia kuhusu Masheikh zaidi ya 70 huko Arusha walioko jela, si kwa sababu wana makosa bali eti wanaipinga BAKWATA ambayo umma umeshatambua kuwa siyo chombo chenye kulinda au kutetea maslahi ya waislamu, bali ni mkono wa system kwa ajili ya kuwathibiti waislamu, Hao viongozi wa BAKWATA wakipewa maslahi machache machache ya hapa na pale kutoka serikali ya CCM basi hufanya bidding kwa ajili ya manufaa ya serikali hiyo, hawana mpango kabisa na mustakbali mkubwa wa Waislamu wenzao nchini! .

Lakini pia umezungumzia Masheikh wa Zanzibar ambao kwa uonevu mkubwa, na ukatili mkubwa kutoka kwa serikali ya CCM na viongozi wake wameendelea kusota magerezani kwa miaka zaidi ya Sita sasa bila kuwepo kwa ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani, na pia wakiwa wametekwa kutoka Zanzibar walipokuwepo na kwenye sheria zenye kutoa dhamana kwa makosa waliyoshitaiwa nayo na kisha kuletwa huku bara kwenye sheria ambayo haitoi dhamana kwa makosa yale ili kuwatesa na kuwaumiza.

Tatu umezungumzia kuhusu Masheikh walioko huko mikoa ya kusini, huko Mtwara ambao nao wako ndani kiuonevu.

Kwa hiyo inavyoonekana serikali ya CCM inatesa Watu wa Mungu, kama haiwatesi kwa nini Inaweka Masheikh wake Jela bila haki?. Je serikali hii ya kidhalimu ina utofauti gani na serikali tunazozisoma kwenye maandiko matakatifu ziliziokuwa zinaonea na kutesa watu wa Mungu?

Ndugu Lissu, Unafanya kazi kubwa sana na nzuri kutetea waislamu nchini. Nakufananisha na Mfalme mmoja wa nchi ya Ethiopia aitwaye Najashi(King Negus kwa kiingereza) aliyekuwepo kipindi Mtume Muhammad alipoanza mafundisho yake huko Arabia, Wanafunzi wa mtume walikuwa wakionewa na serikali katili za Wapagani pale Makka, Mtume akawaagiza wanafunzi wake wakimbilie Ethiopia kwa yule Mfalme ili kujinusuru,mtume akawaambia kuwa waende ethiopia huko kuna mfalme, tena ni mkristo na ni muadilifu na atawatendeeni wema. Na kweli yule mfalme aliwapokea vizuri na kuwatendea wema sana, aligoma hata kuwarudisha Makka pindi ile serikali dhalimu ya Arabia ilipotuma ujumbe kwa huyo mfalme wa Ethiopia ili wale watu warudishwe huko Arabia wakateswe! .
Sasa wewe ndugu Lissu unafanya kazi kama ya mfalme Najashi, unawatetea hawa waislamu wanaonyanyasika katika serikali hii ya CCM.

Nakuomba ndugu Lissu uendelee na moyo huohuo, umeonyesha jinsi ulivyo binadamu, mwenye utu kwelikweli. Tofauti yako na watawala wa CCM ni kubwa sana ni kwamba wewe ni Mtu, wao ni makatili, wewe ni mpenda haki wao ni madhulumati, wewe ni hero wao ni cowards.

Mwisho kabisa, ningependa kukujulisha kuwa waislamu wanakerwa na teuzi za serikali ya awamu hii zinazonuka udini, Nakuomba hili suala ulisemee, ulizungumzie bila woga kwa sababu haiwezekani katika nchi hii kufanya teuzi zinazoonekana waziwazi kuwa zina mrengo wa kidini halafu nchi ikakaa kimya. Hii siyo dhana yangu, bali Masheikh wameshalalamika kuhusu hili, Sheikh Halifa amelisemea hili jambo, Sheikh Ponda na Shura ya maimamu wamelisemea hili jambo. Serikali ya Magufuli haijajibu hoja hii zaidi ya kuwatisha Masheikh hao. Nakuomba ndugu Lissu, mteta haki, msema kweli, na shujaa asiyeogopa madhalimu. Simama na ulizungumzie hili.

La Mwisho nakuomba ukiwa rais, uondoe ubaguzi huu wa Udini, utengeneze serikali shirikishi(inclusive) ambayo itawapa nafasi watu kwa fairness kabisa badala ya kuangalia dini zao au majina yao kama yanasound kizungu au Kiarabu

FREEDOM, JUSTICE AND PEOPLE CENTRED DEVELOPMENT.

View attachment 1567784
Mheshimiwa Tundu Lisu Mungu akupe afya njema. kura zote za familia yangu 45 nimeshakuhakikishia utazipta zote. tutakupa kura zote kwa sababu kuu tatu. moja unatetea kuachiwa kwa masheikh wetu wa UAMSHO. mbili unajiamini na hiyo ndo hulka ya mwanammne. tatu. you call a spade, a spade sio jembe.
 
Back
Top Bottom