Uchaguzi 2020 Asante sana Tundu Lissu kwa kutetea Waislamu walioko jela kwa uonevu, Mungu akulipe kheri nyingi sana

'Ukitumia ukabila au udini badala ya sera za chama chako kupata madaraka, huko ni kufilisika kisiasa na utufai katika kuongoza' Kwa sauti ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere (R.I.P)
 
inategemea wengi wanatakaje mkuu. kama wengi wanautaka muungano wala usihofu ila kama wanaoutaka ni wachache kuliko wasioutaka hapo ni kujisumbua tu maana ni suala la muda tu hapo...wengi watadhinda tu siku moja hata kama ni kwa kuchelewa...ndivyo ilivyo duniani kote. mambo hayo hayalazimishwagi kwa mtutu wa bunduki mkuu wangu; ukifanya hivyo utapata matokeo ya mda mfupi tu tena kwa gharama kubwa na ambayo hayadumu
 
Ni sawa mkuu tuone itakavyokua, hila nataka nikuambie mivutano mingi ya kisiasa ya zanzibar ina sababu nyingi za ndani ya zanzibar yenyewe na watu wake kuliko kutoka nje. Na ina chimbuko lake la muda mrefu tuu huu ni muendelezo tuu.
 
Huyo ‘Maalim Seif’ mwenyewe aliekuwa akipata political mileage kupitia siasa za uhamsho ajawahi tamka hadharani kuwatetea ao masheikh walioko jela.

Ni mtu mpuuzi tu ndio anaweza tetea uhamsho ukizingatia walichokua wanachochea huko Zanzibar.
 
Kwa mujibu wa sheria zetu vyama vya siasa hairuhusiwi kufanya kazi za siasa???
Unajua tumeamua kuchagua vya kufuata, tukiona hili linatupendeza then tunachagua kuacha au kufanya; kwa ufupi hatufuati sheria, to answer you question, tunaruhusiwa kufanya siasa, wana siasa ndio hawataki tufanye siasa na wanatumia vyombo vya DOLA kinyume na sheria kutuzuia tusifanye siasa
 
Mkuu nilikuwa nachunga kauli zangu tu ila wale jamaa ni magaidi , hakuna masihara pale, Lisu anataka kuleta masihara katika mambo ya msingi kama kawaida yake.
Kwa nini sheria isichukue mkondo wake?
Point ya msingi ya Mh. Lissu ni hiyo,wafikishwe mahakamani,sheria ichukue mkondo.
 
Acha ujinga.kwani nchi haina sheria za watu wanaofanya makosa kama hayo?.Kinachozungumziwa ni swala la kila mtu kupata haki yake.Kitendo cha kumshikilia mtu bila kumpeleka mahakamani nikosa kubwa lakiuonevu.Kama unachosema ndicho walichofanya kinachoshindikana kuwapeleka mahakamani wakafungwa ni nini?.Kuendelea kufumbia macho huu uonevu jua ata wewe iko siku itakukuta hali kama hiyo kwahiyo usijione uko salama sana,dunia inazunguka ya kesho hatuyajui.
 
Ulifwatilia sababu za huyo mzee kuwekwa kizuizini?.Nenda kajifunze upya.
 
Sio lazima aseme maalim seif anaweza akasema mwingine pia.swala la haki nijukumu la kila binadamu mwenye akili timamu.
 
Bakwata wanatakiwa kumshukuru Paulo makonda kwa kuwasaidia
 
Sio lazima aseme maalim seif anaweza akasema mwingine pia.swala la haki nijukumu la kila binadamu mwenye akili timamu.
Mwenye akili timamu hawezi wasemea ndio maana ‘Maalim Seif’ ujamsikia akizungumzia maswala ya uhamsho labda puppet wake Jussa.

Kwanini kakaa kimya ni kwa sababu wengi wenu mnaotetea hao masheikh wa uhamsho sidhani kama mlikuwa mnafuatilia movement zao kabla ya kuswekwa jela na jinsi walivyokuwa wanajiona above the law huko visiwani.

JK akutaka waletwe bara kwa bahati mbaya jamaa walikuwa tishio kwa usalama wa raia na mali zao huko Zanzibar achilia mbali hate speech zao.

Ni mpuuzi tu mwenye kupenda cheap politics anaweza tetea uhamsho. If you ask me the old reprobates got what they deserve in the end, liwe somo kwa wengine, usichezee serikali.
 
Sheria zetu zipi hizo,mbona hatuoni wakuhukumiwa kwakutumia hizo sheria.Hakuna mtu anayeunga mkono watu kufanya maovu lakini ata kama mtu kafanya si sheria zakumpa adhabu zipo.kwanini tuendeshe mambo kiuni kiuni kwakukomoana bila kufwata taratibu nasheria ambazo zipo.Kutetea udhalimu kama huu nikuhalalisha kutokuwepo kwa utawala wa sheria na utawala bora.Sasa hii sio sawa kwasababu kuna watakaotumia huo mwanya kunyanyasa nakuonea wengine kwasababu tu wana madaraka flani.
 
Aise hiyo sio suluhisho ndugu.Kwasababu ata wanaowaweka nao watakua wanaondoka moja mmoja hivyo hivyo,kifo nichakila mtu lakini mawazo,fikra na haki vinaishi na lazima ujue kua kama kuna uonevu au watu wanakiu ya haki imeminywa mahali hata ipite miaka mingapi itakuja kudaiwa tu.
 
UTAWALA WA JPM UMEZIFANYA DINI NA TAASISI ZAKE NA WANAOITWA WATUMISHI WA IMANI HIZO KUPOTEZA MAANA NA KUWA KITUKO NA PIA KUPOTEZA IMANI KWA WENYE AKILI KUHUSU HUYO MUNGU WANAEMTUMIKIA KWAMBA SIO WA KWELI NA NI MUNGU WA CCM NA SIO WA WOTE!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…