TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 25,225
- 25,488
'Ukitumia ukabila au udini badala ya sera za chama chako kupata madaraka, huko ni kufilisika kisiasa na utufai katika kuongoza' Kwa sauti ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere (R.I.P)
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
inategemea wengi wanatakaje mkuu. kama wengi wanautaka muungano wala usihofu ila kama wanaoutaka ni wachache kuliko wasioutaka hapo ni kujisumbua tu maana ni suala la muda tu hapo...wengi watadhinda tu siku moja hata kama ni kwa kuchelewa...ndivyo ilivyo duniani kote. mambo hayo hayalazimishwagi kwa mtutu wa bunduki mkuu wangu; ukifanya hivyo utapata matokeo ya mda mfupi tu tena kwa gharama kubwa na ambayo hayadumuNenda kasome kwenye historia elewa kwanini kulikua na mapinduzi ya zanzibar? majibu kamiri. Ilipinduliwa serikali ya kina nani? na wakaingia madarakani kina nani ?na kwanini ukafanyika muungano? na hao wanaotaka muungano uvunjwe ni kina nani na kwanini wanataka muungano uvunjwe? wana malengo yapi na Zanzibar?
Ni sawa mkuu tuone itakavyokua, hila nataka nikuambie mivutano mingi ya kisiasa ya zanzibar ina sababu nyingi za ndani ya zanzibar yenyewe na watu wake kuliko kutoka nje. Na ina chimbuko lake la muda mrefu tuu huu ni muendelezo tuu.inategemea wengi wanatakaje mkuu. kama wengi wanautaka muungano wala usihofu ila kama wanaoutaka ni wachache kuliko wasioutaka hapo ni kujisumbua tu maana ni suala la muda tu hapo...wengi watadhinda tu siku moja hata kama ni kwa kuchelewa...ndivyo ilivyo duniani kote. mambo hayo hayalazimishwagi kwa mtutu wa bunduki mkuu wangu; ukifanya hivyo utapata matokeo ya mda mfupi tu tena kwa gharama kubwa na ambayo hayadumu
Unajua tumeamua kuchagua vya kufuata, tukiona hili linatupendeza then tunachagua kuacha au kufanya; kwa ufupi hatufuati sheria, to answer you question, tunaruhusiwa kufanya siasa, wana siasa ndio hawataki tufanye siasa na wanatumia vyombo vya DOLA kinyume na sheria kutuzuia tusifanye siasaKwa mujibu wa sheria zetu vyama vya siasa hairuhusiwi kufanya kazi za siasa???
Kwa nini sheria isichukue mkondo wake?Mkuu nilikuwa nachunga kauli zangu tu ila wale jamaa ni magaidi , hakuna masihara pale, Lisu anataka kuleta masihara katika mambo ya msingi kama kawaida yake.
Hiyo tundulissu anaongea tu. Swala la wale wahuni wanaojiita masheikh si swala la kisiasa kusema wataamua tu watolewe as if ni watu wasio na shida.
Lile ni swala la kiusalama. Jamaa walikuwa wanachanganya maswala ya dini za itikadi kali yaani radicalism zenye elements za fujo za ugaidi ndani yake na kuingiza kwenye shughuli za kisiasa. Huo ni upuuzi ambao hautakiwi kuchekewa maana ukiachiwa una madhara makubwa sana.
Ni vema wamewekwa ndani na kupewa adhabu ya kudhibitiwa.....
Unajua kuna watu huwa wanawekwa kizuizini kwasababu wao hukaa kwenye nafasi ya uchochezi na kufanya vitu kimya kimya. Hao watu wakishabainika huwa wanapewa onyo ama kutiwa kizuizini.
Mfano ni yule mzee alipigwa ban na nyerere hadi juzi anafariki. Alipigwa ban kuwa asivuke kigamboni hapo wala kwenda zanzibar. Akija mjini ni kwasababu za msingi kama kujiuguza...
Sio lazima aseme maalim seif anaweza akasema mwingine pia.swala la haki nijukumu la kila binadamu mwenye akili timamu.Huyo ‘Maalim Seif’ mwenyewe aliekuwa akipata political mileage kupitia siasa za uhamsho ajawahi tamka hadharani kuwatetea ao masheikh walioko jela.
Ni mtu mpuuzi tu ndio anaweza tetea uhamsho ukizingatia walichokua wanachochea huko Zanzibar.
Bakwata wanatakiwa kumshukuru Paulo makonda kwa kuwasaidiaKwako Ndugu Lissu
Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nawe
Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa dhati ya moyo wangu kwa kitendo chako cha Utu na kupenda haki kwako kwa namna unavyotetea Viongozi wa dini ya Kiislamu walioko Jela kiuonevu.
Umekuwa consistent sana kuhusu uonevu huu, umezungumzia kuhusu Masheikh zaidi ya 70 huko Arusha walioko jela, si kwa sababu wana makosa bali eti wanaipinga BAKWATA ambayo umma umeshatambua kuwa siyo chombo chenye kulinda au kutetea maslahi ya waislamu, bali ni mkono wa system kwa ajili ya kuwathibiti waislamu, Hao viongozi wa BAKWATA wakipewa maslahi machache machache ya hapa na pale kutoka serikali ya CCM basi hufanya bidding kwa ajili ya manufaa ya serikali hiyo, hawana mpango kabisa na mustakbali mkubwa wa Waislamu wenzao nchini! .
Lakini pia umezungumzia Masheikh wa Zanzibar ambao kwa uonevu mkubwa, na ukatili mkubwa kutoka kwa serikali ya CCM na viongozi wake wameendelea kusota magerezani kwa miaka zaidi ya Sita sasa bila kuwepo kwa ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani, na pia wakiwa wametekwa kutoka Zanzibar walipokuwepo na kwenye sheria zenye kutoa dhamana kwa makosa waliyoshitaiwa nayo na kisha kuletwa huku bara kwenye sheria ambayo haitoi dhamana kwa makosa yale ili kuwatesa na kuwaumiza.
Tatu umezungumzia kuhusu Masheikh walioko huko mikoa ya kusini, huko Mtwara ambao nao wako ndani kiuonevu.
Kwa hiyo inavyoonekana serikali ya CCM inatesa Watu wa Mungu, kama haiwatesi kwa nini Inaweka Masheikh wale Jela bila haki?. Je serikali hii ya kidhalimu ina utofauti gani na serikali tunazozisoma kwenye maandiko matakatifu ziliziokuwa zinaonea na kutesa watu wa Mungu?
Ndugu Lissu, Unafanya kazi kubwa sana na nzuri kutetea waislamu nchini. Nakufananisha na Mfalme mmoja wa nchi ya Ethiopia aitwaye Najashi(King Negus kwa kiingereza) aliyekuwepo kipindi Mtume Muhammad alipoanza mafundisho yake huko Arabia, Wanafunzi wa mtume walikuwa wakionewa na serikali katili za Wapagani pale Makka, Mtume akawaagiza wanafunzi wake wakimbilie Ethiopia kwa yule Mfalme ili kujinusuru,mtume akawaambia kuwa waende ethiopia huko kuna mfalme, tena ni mkristo na ni muadilifu na atawatendeeni wema. Na kweli yule mfalme aliwapokea vizuri na kuwatendea wema sana, aligoma hata kuwarudisha Makka pindi ile serikali dhalimu ya Arabia ilipotuma ujumbe kwa huyo mfalme wa Ethiopia ili wale watu warudishwe huko Arabia wakateswe! .
Sasa wewe ndugu Lissu unafanya kazi kama ya mfalme Najashi, unawatetea hawa waislamu wanaonyanyasika katika serikali hii ya CCM.
Nakuomba ndugu Lissu uendelee na moyo huohuo, umeonyesha jinsi ulivyo binadamu, mwenye utu kwelikweli. Tofauti yako na watawala wa CCM ni kubwa sana ni kwamba wewe ni Mtu, wao ni makatili, wewe ni mpenda haki wao ni madhulumati, wewe ni hero wao ni cowards.
Mwisho kabisa, ningependa kukujulisha kuwa waislamu wanakerwa na teuzi za serikali ya awamu hii zinazonuka udini, Nakuomba hili suala ulisemee, ulizungumzie bila woga kwa sababu haiwezekani katika nchi hii kufanya teuzi zinazoonekana waziwazi kuwa zina mrengo wa kidini halafu nchi ikakaa kimya. Hii siyo dhana yangu, bali Masheikh wameshalalamika kuhusu hili, Sheikh Halifa amelisemea hili jambo, Sheikh Ponda na Shura ya maimamu wamelisemea hili jambo. Serikali ya Magufuli haijajibu hoja hii zaidi ya kuwatisha Masheikh hao. Nakuomba ndugu Lissu, mteta haki, msema kweli, na shujaa asiyeogopa madhalimu. Simama na ulizungumzie hili.
La Mwisho nakuomba ukiwa rais, uondoe ubaguzi huu wa Udini, utengeneze serikali shirikishi(inclusive) ambayo itawapa nafasi watu kwa fairness kabisa badala ya kuangalia dini zao au majina yao kama yanasound kizungu au Kiarabu
FREEDOM, JUSTICE AND PEOPLE CENTRED DEVELOPMENT.
View attachment 1567784
Mwenye akili timamu hawezi wasemea ndio maana ‘Maalim Seif’ ujamsikia akizungumzia maswala ya uhamsho labda puppet wake Jussa.Sio lazima aseme maalim seif anaweza akasema mwingine pia.swala la haki nijukumu la kila binadamu mwenye akili timamu.
Hacha kuongea kwa hisia, tafuta video youtube za hizo harakati za "uhamsho" sikiliza kwa umakini halafu wewe mwenyewe tafakari, lengo la hile movement ilikua ni nn, au ilikuja kwa malengo gani, unapojaribu kupambana na serikali iliyopo madarakani kihalali kwa maandamo, kusambaza speech recorded za chuki kwa wananchi kwa serikali yao, kutumia majukwaa ya dini kuingiza kuhubiri siasa za chuki ni uhaini au ugaidi tu kwa sheria zetu.
We ulishaona gaidi anahukumiwa tanzania, hao watavutwa vutwa mpaka waishe mmoja mmoja, hizo nenda rudi ni wengine kama waone kama wakijaribu nini kitawakuta, hila kuachiwa sahau. Hata aiingie nani madarakani hawatoachiwa huru. Hakuna siasa kwenye national security.