Uchaguzi 2020 Asante sana Tundu Lissu kwa kutetea Waislamu walioko jela kwa uonevu, Mungu akulipe kheri nyingi sana

Uchaguzi 2020 Asante sana Tundu Lissu kwa kutetea Waislamu walioko jela kwa uonevu, Mungu akulipe kheri nyingi sana

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Kwako Ndugu Lissu

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nawe
Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa dhati ya moyo wangu kwa kitendo chako cha Utu na kupenda haki kwako kwa namna unavyotetea Viongozi wa dini ya Kiislamu walioko Jela kiuonevu.

Umekuwa consistent sana kuhusu uonevu huu, umezungumzia kuhusu Masheikh zaidi ya 70 huko Arusha walioko jela, si kwa sababu wana makosa bali eti wanaipinga BAKWATA ambayo umma umeshatambua kuwa siyo chombo chenye kulinda au kutetea maslahi ya waislamu, bali ni mkono wa system kwa ajili ya kuwathibiti waislamu, Hao viongozi wa BAKWATA wakipewa maslahi machache machache ya hapa na pale kutoka serikali ya CCM basi hufanya bidding kwa ajili ya manufaa ya serikali hiyo, hawana mpango kabisa na mustakbali mkubwa wa Waislamu wenzao nchini! .

Lakini pia umezungumzia Masheikh wa Zanzibar ambao kwa uonevu mkubwa, na ukatili mkubwa kutoka kwa serikali ya CCM na viongozi wake wameendelea kusota magerezani kwa miaka zaidi ya Sita sasa bila kuwepo kwa ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani, na pia wakiwa wametekwa kutoka Zanzibar walipokuwepo na kwenye sheria zenye kutoa dhamana kwa makosa waliyoshitaiwa nayo na kisha kuletwa huku bara kwenye sheria ambayo haitoi dhamana kwa makosa yale ili kuwatesa na kuwaumiza.

Tatu umezungumzia kuhusu Masheikh walioko huko mikoa ya kusini, huko Mtwara ambao nao wako ndani kiuonevu.

Kwa hiyo inavyoonekana serikali ya CCM inatesa Watu wa Mungu, kama haiwatesi kwa nini Inaweka Masheikh wale Jela bila haki?. Je serikali hii ya kidhalimu ina utofauti gani na serikali tunazozisoma kwenye maandiko matakatifu ziliziokuwa zinaonea na kutesa watu wa Mungu?

Ndugu Lissu, Unafanya kazi kubwa sana na nzuri kutetea waislamu nchini. Nakufananisha na Mfalme mmoja wa nchi ya Ethiopia aitwaye Najashi(King Negus kwa kiingereza) aliyekuwepo kipindi Mtume Muhammad alipoanza mafundisho yake huko Arabia, Wanafunzi wa mtume walikuwa wakionewa na serikali katili za Wapagani pale Makka, Mtume akawaagiza wanafunzi wake wakimbilie Ethiopia kwa yule Mfalme ili kujinusuru,mtume akawaambia kuwa waende ethiopia huko kuna mfalme, tena ni mkristo na ni muadilifu na atawatendeeni wema. Na kweli yule mfalme aliwapokea vizuri na kuwatendea wema sana, aligoma hata kuwarudisha Makka pindi ile serikali dhalimu ya Arabia ilipotuma ujumbe kwa huyo mfalme wa Ethiopia ili wale watu warudishwe huko Arabia wakateswe! .
Sasa wewe ndugu Lissu unafanya kazi kama ya mfalme Najashi, unawatetea hawa waislamu wanaonyanyasika katika serikali hii ya CCM.

Nakuomba ndugu Lissu uendelee na moyo huohuo, umeonyesha jinsi ulivyo binadamu, mwenye utu kwelikweli. Tofauti yako na watawala wa CCM ni kubwa sana ni kwamba wewe ni Mtu, wao ni makatili, wewe ni mpenda haki wao ni madhulumati, wewe ni hero wao ni cowards.

Mwisho kabisa, ningependa kukujulisha kuwa waislamu wanakerwa na teuzi za serikali ya awamu hii zinazonuka udini, Nakuomba hili suala ulisemee, ulizungumzie bila woga kwa sababu haiwezekani katika nchi hii kufanya teuzi zinazoonekana waziwazi kuwa zina mrengo wa kidini halafu nchi ikakaa kimya. Hii siyo dhana yangu, bali Masheikh wameshalalamika kuhusu hili, Sheikh Halifa amelisemea hili jambo, Sheikh Ponda na Shura ya maimamu wamelisemea hili jambo. Serikali ya Magufuli haijajibu hoja hii zaidi ya kuwatisha Masheikh hao. Nakuomba ndugu Lissu, mteta haki, msema kweli, na shujaa asiyeogopa madhalimu. Simama na ulizungumzie hili.

La Mwisho nakuomba ukiwa rais, uondoe ubaguzi huu wa Udini, utengeneze serikali shirikishi(inclusive) ambayo itawapa nafasi watu kwa fairness kabisa badala ya kuangalia dini zao au majina yao kama yanasound kizungu au Kiarabu

FREEDOM, JUSTICE AND PEOPLE CENTRED DEVELOPMENT.

 
Kama JPM ameweza kuwaachia akina babu Seya ambao walikutwa na hatia ya kulawiti na kubaka vitoto,iweje masheikh ambao hakuna ushahidi dhidi yao wanaendelea kusota rumande!!!!?
Waislam mchagueni Lissu akatende haki kwa waumini na viongozi wenzenu!
 
Kama JPM ameweza kuwaachia akina babu Seya ambao walikutwa na hatia ya kulawiti na kubaka vitoto,iweje masheikh ambao hakuna ushahidi dhidi yao wanaendelea kusota rumande!!!!?
Waislam mchagueni Lissu akatende haki kwa waumini na viongozi wenzenu!

Ni ajabu sana, halafu Anajifanya mcha Mungu wakati akisotesha watu wa Mungu Magerezani
 
Mfumo tu sheria na mahakama zetu si huru. Majuzi tu mahakama kuu Dodoma waliamuru vijana wa Bavicha T (Nusrat Hanje na wenzie) waachiliwe kwa dhamana.

Lakini walipo rudishwa mahakama za chini kwa taratibu za dhamana imekuwa danadana.

Mifumo yetu ya sheria inaangalia utashi wa nani aliye hapo juu

Nafananisha na hili la ma sheikh
 
Mfumo tu sheria na mahakama zetu si huru. Majuzi tu mahakama kuu Dodoma waliamuru vijana wa Bavicha T (Nusrat Hanje na wenzie) waachiliwe kwa dhamana. Lakini walipo rudishwa mahakama za chini kwa taratibu za dhamana imekuwa danadana.
Mifumo yetu ya sheria inaangalia utashi wa nani aliye hapo juu

Nafananisha na hili la ma sheikh

DPP yuko chini ya serikali husika, kama serikali ikitaka kufuta kesi za kidhalimu ni ndani ya sekunde moja tu.

Tatizo ni kwamba serikali ya CCM siyo serikali ya haki, hususan ya awamu hii ndo siyo ya haki zaidi!
 
Kauli za wafa maji hizo, bahati nzuri sana Chadema mwisho ni October

Mzungu hana nafasi Tanzania,
Ni bora akachaguliwa mwakilishi wa mabeberu walau tutendelea kuishuhudia demokrasia ila siyo mwakilishi wa BAHIMA EMPIRE, halafu mwaka 2025 tukaishia kutawaliwa kidikteta kama ilivyo Rwanda na Uganda.
 
DPP yuko chini ya serikali husika, kama serikali ikitaka kufuta kesi za kidhalimu ni ndani ya sekunde moja tu.

Tatizo ni kwamba serikali ya CCM siyo serikali ya haki, hususan ya awamu hii ndo siyo ya haki zaidi!
Kama mahakama ya juu imeshaamuru mtu aachiliwe. Mahakama ya chini inaona kigugumizi gani ?!

Je mahakimu hawapo huru kufanya kazi zao ?! Au nini !!
 
Wewe kuangalia udini... Umeshawaka udini tiyari.. Yani nashangaa kwanini Waafrika wanakuwa na shahuku wakisia mtu wa dini flani dini zenyewe zote zilituletea utumwa na mateso leo tume kuwa wafia dini [emoji24][emoji24][emoji24].. Wakristu walileta utumwa na ukoloni waislamu waarabu walileta utumwa na mateso kwa Waafrika sasa kutaka kuifia dini isiyokujali ni kuvurugwa akili
 
Back
Top Bottom