Uchaguzi 2020 Asante sana Tundu Lissu kwa kutetea Waislamu walioko jela kwa uonevu, Mungu akulipe kheri nyingi sana

Uchaguzi 2020 Asante sana Tundu Lissu kwa kutetea Waislamu walioko jela kwa uonevu, Mungu akulipe kheri nyingi sana

kwan cdm hakuna waru wengine wa kuanzisha threads kila sku wale wale
 
Ni ajabu sana, halafu Anajifanya mcha Mungu wakati akisotesha watu wa Mungu Magerezani
Huyo sio mcha Mungu Bali huwa anaenda kutembea kanisani ili aonekane na watu , soma 6:5 Mathayo
IMG_20200912_123312_1.jpg
 
Ila usisahau hao Masheikh walishikiliwa tangu enzi za Kikwete! Hivyo ni vyema na yeye akatajwa kuhusika kwa namna fulani kama Rais wa wakati huo.
Kwani babu seya alishikiliwa toka lini?
 
Kwako Ndugu Lissu

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nawe
Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa dhati ya moyo wangu kwa kitendo chako cha Utu na kupenda haki kwako kwa namna unavyotetea Viongozi wa dini ya Kiislamu walioko Jela kiuonevu.

Umekuwa consistent sana kuhusu uonevu huu, umezungumzia kuhusu Masheikh zaidi ya 70 huko Arusha walioko jela, si kwa sababu wana makosa bali eti wanaipinga BAKWATA ambayo umma umeshatambua kuwa siyo chombo chenye kulinda au kutetea maslahi ya waislamu, bali ni mkono wa system kwa ajili ya kuwathibiti waislamu, Hao viongozi wa BAKWATA wakipewa maslahi machache machache ya hapa na pale kutoka serikali ya CCM basi hufanya bidding kwa ajili ya manufaa ya serikali hiyo, hawana mpango kabisa na mustakbali mkubwa wa Waislamu wenzao nchini! .

Lakini pia umezungumzia Masheikh wa Zanzibar ambao kwa uonevu mkubwa, na ukatili mkubwa kutoka kwa serikali ya CCM na viongozi wake wameendelea kusota magerezani kwa miaka zaidi ya Sita sasa bila kuwepo kwa ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani, na pia wakiwa wametekwa kutoka Zanzibar walipokuwepo na kwenye sheria zenye kutoa dhamana kwa makosa waliyoshitaiwa nayo na kisha kuletwa huku bara kwenye sheria ambayo haitoi dhamana kwa makosa yale ili kuwatesa na kuwaumiza.

Tatu umezungumzia kuhusu Masheikh walioko huko mikoa ya kusini, huko Mtwara ambao nao wako ndani kiuonevu.

Kwa hiyo inavyoonekana serikali ya CCM inatesa Watu wa Mungu, kama haiwatesi kwa nini Inaweka Masheikh wake Jela bila haki?. Je serikali hii ya kidhalimu ina utofauti gani na serikali tunazozisoma kwenye maandiko matakatifu ziliziokuwa zinaonea na kutesa watu wa Mungu?

Ndugu Lissu, Unafanya kazi kubwa sana na nzuri kutetea waislamu nchini. Nakufananisha na Mfalme mmoja wa nchi ya Ethiopia aitwaye Najashi(King Negus kwa kiingereza) aliyekuwepo kipindi Mtume Muhammad alipoanza mafundisho yake huko Arabia, Wanafunzi wa mtume walikuwa wakionewa na serikali katili za Wapagani pale Makka, Mtume akawaagiza wanafunzi wake wakimbilie Ethiopia kwa yule Mfalme ili kujinusuru,mtume akawaambia kuwa waende ethiopia huko kuna mfalme, tena ni mkristo na ni muadilifu na atawatendeeni wema. Na kweli yule mfalme aliwapokea vizuri na kuwatendea wema sana, aligoma hata kuwarudisha Makka pindi ile serikali dhalimu ya Arabia ilipotuma ujumbe kwa huyo mfalme wa Ethiopia ili wale watu warudishwe huko Arabia wakateswe! .
Sasa wewe ndugu Lissu unafanya kazi kama ya mfalme Najashi, unawatetea hawa waislamu wanaonyanyasika katika serikali hii ya CCM.

Nakuomba ndugu Lissu uendelee na moyo huohuo, umeonyesha jinsi ulivyo binadamu, mwenye utu kwelikweli. Tofauti yako na watawala wa CCM ni kubwa sana ni kwamba wewe ni Mtu, wao ni makatili, wewe ni mpenda haki wao ni madhulumati, wewe ni hero wao ni cowards.

Mwisho kabisa, ningependa kukujulisha kuwa waislamu wanakerwa na teuzi za serikali ya awamu hii zinazonuka udini, Nakuomba hili suala ulisemee, ulizungumzie bila woga kwa sababu haiwezekani katika nchi hii kufanya teuzi zinazoonekana waziwazi kuwa zina mrengo wa kidini halafu nchi ikakaa kimya. Hii siyo dhana yangu, bali Masheikh wameshalalamika kuhusu hili, Sheikh Halifa amelisemea hili jambo, Sheikh Ponda na Shura ya maimamu wamelisemea hili jambo. Serikali ya Magufuli haijajibu hoja hii zaidi ya kuwatisha Masheikh hao. Nakuomba ndugu Lissu, mteta haki, msema kweli, na shujaa asiyeogopa madhalimu. Simama na ulizungumzie hili.

La Mwisho nakuomba ukiwa rais, uondoe ubaguzi huu wa Udini, utengeneze serikali shirikishi(inclusive) ambayo itawapa nafasi watu kwa fairness kabisa badala ya kuangalia dini zao au majina yao kama yanasound kizungu au Kiarabu

FREEDOM, JUSTICE AND PEOPLE CENTRED DEVELOPMENT.
atakuwa amekusikia atajaribu kuwasemea maana hana uwezo wa kuwa rais ili aje awatoe hao watu mnaodhani wamewekwa ndani kwadhuruma mngekuwa na akili kidogo tu mngeanza kumuuliza kikwete ambaye ni muislamu kwanini aliwaweka ndani na hakuwatoa mpakaamemaliza muda wake ujue kuna tatizo na hawa watu msirahisishe mambo
 
Lisu anayatafuta madaraka kwa namna yeyote ile bila kujali madhara ya kauli zake.

Sijui atakuwa kiongozi wa Taifa lipi ambalo tayari keshalisambaratisha kwa kauli za kichochezi.

Toka hao jamaa wa Zanzibar wakamatwe kuna Kanisa limechomwa moto kule ??

How can this man be so blind like this?? Ni Uchu wa madaraka tu.
 
Ubaguzi wa kidini unaousema kwanza haupo huku bara bali upo Zanzibar. Pili nionyeshe mgombea ubunge au uwakilishi huko Zanzibar ambaye ni mkristo. Je Zanzibar hakuna wakristo hata kama wachache?
Hao masheikh, Lissu anaowatumia kama chambo ili kupata kura za waislamu hawana tuhuma za makosa ya jinai? Kumbuka kule zanzibar padre amewahi kuuawa mlangoni kanisani, watalii kumwagiwa tindikali yote hiyo kutokana na mahubiri ya chuki katika nyumba za ibada, kanda zilizorekodiwa.

Huku bara kuna wakati makanisa yalichomwa, mengine mipango ya kuyashambulia iliwahiwa ndio ikawa salama. Ugaidi wa Kibiti yeye Lissu aliufurahia.

Serikali yeyote makini haiwezi kukaa kimya wakati kuna watu wanapanga na kutekeleza ugaidi ndani ya nchi. Lissu anaweza kuwa na uchungu na waislamu kuliko waislamu wenyewe ea Zanzibar walioamua kuwachukulia hatua baada ya kuona vitendo vyao vya kigaidi vimezidi licha ya kuonywa mara kadhaa? Hivi yaliyokuwa yakiendelea kule Zanzibar na Kibiti wakati ule kabla hawajawekwa ndani yeye Lissu alikuwa hayaoni au ndio cheap politics?

Kama kuna mtu anataka nafasi za uteuzi ziwe nusu kwa nusu baina ya ukristo na uislamu basi kwanza aanzie Zanzibar kabla hajazungumzia bara .
Du point zote hizo ulizotoa hamna like hata moja, ni ajabu na kweli.
 
Kwani babu seya alishikiliwa toka lini?

Babu Seya hakushikiliwa kama hao Masheikh wa Uamsho! Yule alihukumiwa kabisa na Wanawe kifungo cha maisha kutokana na makosa ya kuwanajisi watoto kabla ya kupewa huo msamaha wao na Magufuli!

Walitenda makosa yao, hawakutenda! Hili litabakia kuwa fumbo kuu. Na ukweli wa kilichotokea, wanao wenyewe.
 
Hivi Lissu alishawahi kuzungumzia huuu uonevu wa hao masheikh wa uamsho au ndio amekuja kulizungumzia hili suala wakati huu wa kampeni?
 
Lisu anayatafuta madaraka kwa namna yeyote ile bila kujali madhara ya kauli zake.

Sijui atakuwa kiongozi wa Taifa lipi ambalo tayari keshalisambaratisha kwa kauli za kichochezi.

Toka hao jamaa wa Zanzibar wakamatwe kuna Kanisa limechomwa moto kule ??

How can this man be so blind like this?? Ni Uchu wa madaraka tu.

Ngoja kwanza awe Rais. Hayo mambo mengine yatajulikana mbele ya safari. Hivyo hakikisha unampa kura yako hata kama hatokani na chama chako.
 
Back
Top Bottom