Uchaguzi 2020 Asante sana Tundu Lissu kwa kutetea Waislamu walioko jela kwa uonevu, Mungu akulipe kheri nyingi sana

Uchaguzi 2020 Asante sana Tundu Lissu kwa kutetea Waislamu walioko jela kwa uonevu, Mungu akulipe kheri nyingi sana

ni mahakama ipi imedhibitisha wao ni magaidi? au ni mtu mmoja tu kaamua kumpa mbwa jina baya ili auwawe? hata mandela kuna serikali ilimuita gaidi. na kama ni suala tu la mtu kuamua huyu ni gaidi na huyu si gaidi pasipo mahakama kuthibitisha basi hata wewe unaweza kuitwa gaidi muda wowote na ukafungwa au kuuwawa kama mbwa tu na hakuna atakayehoji. kataa dhulumati na ubaya hata kama anayetendewa ubaya ni mtu hukubaliani naye kiitikadi..usisubiri mpaka yakufike wewe mana hutakuwa na wa kutetea. binadam haachi kuwa binadamu kwa kuwa tu umetofautiana naye itikadi au mawazo na tena kutofautiana kimitizamo ni jambo la kawaida sana kibinadam..kikubwa ni hoja yenye nguvu. mtu kuhoji Muungano anakuwa gaidi kivip?
wewe ndiye unayesema walihubiri ugaidi, embu thibitisha tuwekee hiyo video.

vinginevyo tambua serikali yoyote iliyopo duniani ni ya wanadamu tu na si malaika hivyo kukosolewa na hata kupingwa ni lazima. na ukizuia kimabavu kupingwa na kukosolewa kwa njia za halali zilizopo kisheria basi utapingwa hata kwa njia zisizo za kisheria na hiyo ni duniani kote ndivyo ilivyo. hata chauma cuf au chadema wakiingia madarakani leo watakosolewa/watapingwa vilevile na hiyo si dhambi; kubwa ni hoja na ni katika kupingana na kukosoana ndiko maendeleo ya kweli yanakotokea. ccm ilipingwa/ilikosolewa jana, itakosolewa leo na itakosolewa kesho; almradi ipo haijafutika juu ya uso wa Tanzania itakosolewa tu hata kama haipo madarakani..acheni mawazo finyu ya kuwaita wakosoaji wenu magaidi mara vibaraka wa mabeberu; hizo ni siasa muflisi na haziwapi credit yoyote zaidi ya kuwashusha tu. huo muungano kama haukubaliki kwa sehemu moja ya nchi utaendelea kupingwa tu daima dumu. ingekuwa kufunga watu, kuwaua au kuwatesa kunawarudisha watu nyuma basi Afrika kusini ingekuwa bado chini ya makaburu na watu weusi marekani leo wangekuwa hata kufutwa juu ya uso wa marekan wameshafutwa. huwez kuzuia haki kwa njia haramu daima; sana sana utaichelewesha tu kwa muda flani lakin mwisho haki itafika tu hata kama ni kwa kuchelewa.
Mkuu..umeongea vizuri sana..yaani maoni yangu yote umenisemea!
 
Kura za Waislamu wenye uchungu wa mateso na madhila ya kunyanyaswa Masheikh wao watampa kura Lissu maana ameonyesha utu na kupenda haki!

Lissu aendelee kulizungumzia hili suala maana linahusu haki za watu walioonewa!
 
acha kupiga propaganda kwenye suala linalohusu haki na maisha ya watu wewe; mashekhe walikamatwa na kikwte au na serikali ya ccm? na huyo magufuli anaongoza serikali inayoundwa na chama gan kama siyo hayo hayo makijani?

ma ccm achen kukandamiza watanzania.
Endeleeni kubweka 🗣️, nchi haiwezi kuendeshwa kijinga hivyo Kama mnavyotaka.Kuongoza nchi sio kujua Sheria tu.
 
wewe ndiye unayesema walihubiri ugaidi, embu thibitisha tuwekee hiyo video.

vinginevyo tambua serikali yoyote iliyopo duniani ni ya wanadamu tu na si malaika hivyo kukosolewa na hata kupingwa ni lazima. na ukizuia kimabavu kupingwa na kukosolewa kwa njia za halali zilizopo kisheria basi utapingwa hata kwa njia zisizo za kisheria na hiyo ni duniani kote ndivyo ilivyo. hata chauma cuf au chadema wakiingia madarakani leo watakosolewa/watapingwa vilevile na hiyo si dhambi; kubwa ni hoja na ni katika kupingana na kukosoana ndiko maendeleo ya kweli yanakotokea. ccm ilipingwa/ilikosolewa jana, itakosolewa leo na itakosolewa kesho; almradi ipo haijafutika juu ya uso wa Tanzania itakosolewa tu hata kama haipo madarakani..acheni mawazo finyu ya kuwaita wakosoaji wenu magaidi mara vibaraka wa mabeberu; hizo ni siasa muflisi na haziwapi credit yoyote zaidi ya kuwashusha tu. huo muungano kama haukubaliki kwa sehemu moja ya nchi utaendelea kupingwa tu daima dumu. ingekuwa kufunga watu, kuwaua au kuwatesa kunawarudisha watu nyuma basi Afrika kusini ingekuwa bado chini ya makaburu na watu weusi marekani leo wangekuwa hata kufutwa juu ya uso wa marekan wameshafutwa. huwez kuzuia haki kwa njia haramu daima; sana sana utaichelewesha tu kwa muda flani lakin mwisho haki itafika tu hata kama ni kwa kuchelewa.
Kuwa kiongozi sio tuu kufuata sheria, kuna muda unatakiwa kufanya maamuzi magumu nje ya sheria.
 
KWa mujibu wa sheria zetu, rais hana uwezo wa kumuachilia mtu aliyeko rumande, yule aliyefungwa hata maisha, yaani maadamu kahukumiwa na mahakama, rais anayo HAKI ya either kumpunguzia makosa au hata kumuachilia. KWa case ya ma sheikh, rais angeweza kushurutisha vyombo vyake hivyo vinavyo fanya uchunguzi, vifanye haraka ili viongozi wale wa dini wapewe HAKI yao kwa mujibu wa sheria zetu na hapa ndio Tundu anapopaongelea. In fact hata mimi nina amini wale masheikh hawana makosa au kama wanayo makosa basi USHAHIDI serikali HAINA na ndio maana haiwapeleki mahakamani, sawa tu na kina Rugemalulila; tukachague kiongozi anae penda HAKI ili AMANI idumu
Kwa mujibu wa sheria zetu vyama vya siasa hairuhusiwi kufanya kazi za siasa???
 
Mheshimiwa Tundu Lisu Mungu akupe afya njema. kura zote za familia yangu 45 nimeshakuhakikishia utazipta zote. tutakupa kura zote kwa sababu kuu tatu. moja unatetea kuachiwa kwa masheikh wetu wa UAMSHO. mbili unajiamini na hiyo ndo hulka ya mwanammne. tatu. you call a spade, a spade sio jembe.
Hizi kura mnazopiga kifamilia huwa mnapigaje.
Kwamba kuna mtu anamuongelea mtu mwingine atampigia kura flani. Au huwa anapiga mmoja halafu zinahesabiwa kwa idadi ya wanafamilia.
Uzuri wa kura hata mkeo anaweza asikupigie ila Kama unamshurutisha kusema mimi na familia yangu tutampigia flani atakubali ili akuridhishe na udikteta wako ila siku ya kura inabaki siri yake.
Nakumbuka kuna mgombea alipata kura moja yakwake tu akalalamika kwamba Inamaana hata mkewe hakumpigia.
Mimi simuongelei mwingine ila mimi Kama Mimi bado nawatazama wagombea kwa makini itakapofika tarehe 27 nitakua namaamuzi ili tarehe 28 nitumie haki yangu. Sijui wanafamilia wengine watampigia nani maana ni mwendo wa demokrasia kuanzia ngazi ya familia.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
s
Kuwa kiongozi sio tuu kufuata sheria, kuna muda unatakiwa kufanya maamuzi magumu nje ya sheria.
siyo kila maamuzi magumu mi maamuzi magumu kweli. Mhe Jakaya aliwaambia mapema kuwa hoja haipigwi rungu, hoja ya kisiasa hukabiliwa kwa hoja kinzani ya kisiasa. uamuzi mgumu wa kumuua kwa bunduki mbu aliyetua usoni kwako ni uamuzi usio na tija.
 
Kubali kataa approach ya mashekh wa "uhamsho" haikua sahihi ilikua to hostile, wengetumia approach nyingine, kuna kesi zinaendelea kwenye mahakama za africa kuhusu muungano, njia hizo zimetumiwa na watu muda wote, huwezi kutishia dola halafu ukaachwa haiwezekani, dola ipo wajibu na maisha zanzibar kuna watu 2ml. Lolote lingewakuta, ungekuja hapa kulalmika kuwa serikali imeshindwa kulinda watu na mali zao
 
Waislam wote tunamchagua Tundu Lissu. Huyu ndiye atayetetea maslahi yetu. Tulivyojipanga safari hii ni kuwa tunakula hela zao ila kura ni kwa Lissu. Lissu ni wa Watanzania wote.
 
Waislam wenzangu kama tulivyokubaliana, this time tunaleta mabadiliko ya kweli nchini kwetu. Nchi tunampa Tundu Lissu.
 
Ila usisahau hao Masheikh walishikiliwa tangu enzi za Kikwete! Hivyo ni vyema na yeye akatajwa kuhusika kwa namna fulani kama Rais wa wakati huo.

Mavi ya jana hayanuki; kikwete sio raisi hivisasa.
 
Kubali kataa approach ya mashekh wa "uhamsho" haikua sahihi ilikua to hostile, wengetumia approach nyingine, kuna kesi zinaendelea kwenye mahakama za africa kuhusu muungano, njia hizo zimetumiwa na watu muda wote, huwezi kutishia dola halafu ukaachwa haiwezekani, dola ipo wajibu na maisha zanzibar kuna watu 2ml. Lolote lingewakuta, ungekuja hapa kulalmika kuwa serikali imeshindwa kulinda watu na mali zao
vip siku hiz baada ya kuwa dhoofu khali cuf hawaingizagi tena majambia zanzibar? Kwa kuwa sasa ACT ndo wenye nguvu Zanzibar muda si mrefu tutasikia ACT ni magaidi na wameingiza shehena ya majambia Zanzibar..ahahaaaa
mnafanya siasa za ulaghai karne hii ya 21 mnategemea mtaeleweka kweli kwa kizazi hiki cha smartphone za tachi?!!!
 
Waislam wenzangu kama tulivyokubaliana, this time tunaleta mabadiliko ya kweli nchini kwetu. Nchi tunampa Tundu Lissu.
hili ni muhimu sana. na tunawaomba ndugu zetu wakristu wa bara wasimame na sisi ndugu zao waislamu wa zanzibar kwa khali na mali..sisi sote bara na visiwani adui yetu ni mmoja tu..maccm.
 
vip siku hiz baada ya kuwa dhoofu khali cuf hawaingizagi tena majambia zanzibar? Kwa kuwa sasa ACT ndo wenye nguvu Zanzibar muda si mrefu tutasikia ACT ni magaidi na wameingiza shehena ya majambia Zanzibar..ahahaaaa
mnafanya siasa za ulaghai karne hii ya 21 mnategemea mtaeleweka kweli kwa kizazi hiki cha smartphone za tachi?!!!
Hii mada nyingine tena, hila nachotaka kukuambia muungano kuvunjika zanzibar ikawa kivyake hilo sahau, hila tegemea zaidi zanzibar kumezwa ndani ya serikali moja halafu hizi kelele za muungano zikawa zimefika mwisho. Hilo litegemee sana siku zijazo hasa ndani ya utawala huu wa awamo ya tano.
 
kama ni kwa khiari ya wazanzibari sawa ila kwa nguvu ya dola hilo sahau Mkuu. Tafuteni namna ya kuipata khiari ya Wazanzibari vinginevyo ni mchezo wa kujitekenya na kujicheka. ndoa ya kulazimishana ni maigizo tu ya muda mfupi. utamu wa tendo la ndoa ni mwanamke akhiari, ukilazimisha utaambulia michubuko tu na zaidi sana miaka 30 jela yaweza kukusomba.
 
Wanasheria hutetea hata wauaji
Kwa "sheria" na tamaduni za ccm, serikali yao ikimtuhumu mtu kwa koaa lolote, tayari ni guilty , na anatendewa kama mkosaji. Lakini kwa mujibu wa sheria halali za Tanzania , mamlaka pekee yenye uwezo wa kutamka fulani ana hatia ya mauaji, ni mahakama, baada ya kuendesha kesi na kutoa hukumu.

Mtuhumiwa wa kosa lolote ana haki, pamoja na haki ya kupata utetezi makini. Ila kwa kuwa mmezoea ukandamizaji, unyanyasaji na uonevu, mambo ya HAKI kwako ni kumpigia mbuzi gitaa
 
kama ni kwa khiari ya wazanzibari sawa ila kwa nguvu ya dola hilo sahau Mkuu. Tafuteni namna ya kuipata khiari ya Wazanzibari vinginevyo ni mchezo wa kujitekenya na kujicheka. ndoa ya kulazimishana ni maigizo tu ya muda mfupi. utamu wa tendo la ndoa ni mwanamke akhiari, ukilazimisha utaambulia michubuko tu na zaidi sana miaka 30 jela yaweza kukusomba.
Nenda kasome kwenye historia elewa kwanini kulikua na mapinduzi ya zanzibar? majibu kamiri. Ilipinduliwa serikali ya kina nani? na wakaingia madarakani kina nani ?na kwanini ukafanyika muungano? na hao wanaotaka muungano uvunjwe ni kina nani na kwanini wanataka muungano uvunjwe? wana malengo yapi na Zanzibar?
 
Kwako Ndugu Lissu

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nawe
Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa dhati ya moyo wangu kwa kitendo chako cha Utu na kupenda haki kwako kwa namna unavyotetea Viongozi wa dini ya Kiislamu walioko Jela kiuonevu.

Umekuwa consistent sana kuhusu uonevu huu, umezungumzia kuhusu Masheikh zaidi ya 70 huko Arusha walioko jela, si kwa sababu wana makosa bali eti wanaipinga BAKWATA ambayo umma umeshatambua kuwa siyo chombo chenye kulinda au kutetea maslahi ya waislamu, bali ni mkono wa system kwa ajili ya kuwathibiti waislamu, Hao viongozi wa BAKWATA wakipewa maslahi machache machache ya hapa na pale kutoka serikali ya CCM basi hufanya bidding kwa ajili ya manufaa ya serikali hiyo, hawana mpango kabisa na mustakbali mkubwa wa Waislamu wenzao nchini! .

Lakini pia umezungumzia Masheikh wa Zanzibar ambao kwa uonevu mkubwa, na ukatili mkubwa kutoka kwa serikali ya CCM na viongozi wake wameendelea kusota magerezani kwa miaka zaidi ya Sita sasa bila kuwepo kwa ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani, na pia wakiwa wametekwa kutoka Zanzibar walipokuwepo na kwenye sheria zenye kutoa dhamana kwa makosa waliyoshitaiwa nayo na kisha kuletwa huku bara kwenye sheria ambayo haitoi dhamana kwa makosa yale ili kuwatesa na kuwaumiza.

Tatu umezungumzia kuhusu Masheikh walioko huko mikoa ya kusini, huko Mtwara ambao nao wako ndani kiuonevu.

Kwa hiyo inavyoonekana serikali ya CCM inatesa Watu wa Mungu, kama haiwatesi kwa nini Inaweka Masheikh wale Jela bila haki?. Je serikali hii ya kidhalimu ina utofauti gani na serikali tunazozisoma kwenye maandiko matakatifu ziliziokuwa zinaonea na kutesa watu wa Mungu?

Ndugu Lissu, Unafanya kazi kubwa sana na nzuri kutetea waislamu nchini. Nakufananisha na Mfalme mmoja wa nchi ya Ethiopia aitwaye Najashi(King Negus kwa kiingereza) aliyekuwepo kipindi Mtume Muhammad alipoanza mafundisho yake huko Arabia, Wanafunzi wa mtume walikuwa wakionewa na serikali katili za Wapagani pale Makka, Mtume akawaagiza wanafunzi wake wakimbilie Ethiopia kwa yule Mfalme ili kujinusuru,mtume akawaambia kuwa waende ethiopia huko kuna mfalme, tena ni mkristo na ni muadilifu na atawatendeeni wema. Na kweli yule mfalme aliwapokea vizuri na kuwatendea wema sana, aligoma hata kuwarudisha Makka pindi ile serikali dhalimu ya Arabia ilipotuma ujumbe kwa huyo mfalme wa Ethiopia ili wale watu warudishwe huko Arabia wakateswe! .
Sasa wewe ndugu Lissu unafanya kazi kama ya mfalme Najashi, unawatetea hawa waislamu wanaonyanyasika katika serikali hii ya CCM.

Nakuomba ndugu Lissu uendelee na moyo huohuo, umeonyesha jinsi ulivyo binadamu, mwenye utu kwelikweli. Tofauti yako na watawala wa CCM ni kubwa sana ni kwamba wewe ni Mtu, wao ni makatili, wewe ni mpenda haki wao ni madhulumati, wewe ni hero wao ni cowards.

Mwisho kabisa, ningependa kukujulisha kuwa waislamu wanakerwa na teuzi za serikali ya awamu hii zinazonuka udini, Nakuomba hili suala ulisemee, ulizungumzie bila woga kwa sababu haiwezekani katika nchi hii kufanya teuzi zinazoonekana waziwazi kuwa zina mrengo wa kidini halafu nchi ikakaa kimya. Hii siyo dhana yangu, bali Masheikh wameshalalamika kuhusu hili, Sheikh Halifa amelisemea hili jambo, Sheikh Ponda na Shura ya maimamu wamelisemea hili jambo. Serikali ya Magufuli haijajibu hoja hii zaidi ya kuwatisha Masheikh hao. Nakuomba ndugu Lissu, mteta haki, msema kweli, na shujaa asiyeogopa madhalimu. Simama na ulizungumzie hili.

La Mwisho nakuomba ukiwa rais, uondoe ubaguzi huu wa Udini, utengeneze serikali shirikishi(inclusive) ambayo itawapa nafasi watu kwa fairness kabisa badala ya kuangalia dini zao au majina yao kama yanasound kizungu au Kiarabu

FREEDOM, JUSTICE AND PEOPLE CENTRED DEVELOPMENT.

View attachment 1567784

Yani udini ukabila umetamalaki
 
Back
Top Bottom